Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Namheshimu sana Mh Mnyika kama mmoja wa wabunge makini sana lakini kwa suala la kigamboni, ameharibu. Sera yake ya ngoja ngoja, inawaumiza matumbo ya walipa kodi walio vijijini. Imefikia wakati sasa watumiaji wa kivuko cha kigamboni ndio wawe na wajibu wa kuchangia zaidi katika uendeshaji wa kivuko kile chini ya nauli mpya, sio maskini wa bariadi, maswa, kyela, tandahimba, na kasulu kupitia kodi zao kwa serikali kuu, ambazo huchotwa kama ruzuku. Na maskini hawa, wengi wao hata hawajui kama kuna kivuko kigamboni.