Hii imekaaje ya kuja kulipia daraja la Kigamboni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii imekaaje ya kuja kulipia daraja la Kigamboni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPA, Jan 11, 2012.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Labda mimi sielewi!

  Sijawahi kusikia dunia hii kuna nchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaidi ya kodi, fines. Hii ya daraja la Kigamboni kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwani kodi tunazolipa zinafanya nini? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gani?

  Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana JF naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia?

  Na nini maana ya public goods?

  Nawasilisha
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Usipende vya bure.........daraja linajengwa na NSSF sasa michango yetu unataka irudi vipi?
   
 3. matwi

  matwi JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa hatakama wanajenga NSSF je kuna time limit au inakaa vipi hii kweli bado ni kizungumkuti
   
 4. k

  kaeso JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata mimi nilibaki mdomo wazi baada ya kusikia eti itakuwa ni kulipia kupita hapo darajani. Sielewi!!!
   
 5. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  NSSF wanajenga au wamewakopesha serikali?
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Huyo mtangazaji wa BBC kama kashangaa kweli basi itakuwa kwa sababu nyengine, sio kwa kuwa hajawahi kusikia ama kuona ama kutumia barabara na madaraja ya kulipia. Uingereza barabara hizo zimejaa tele, pamoja na nchi nyengine zilizoendelea.

  Katika nchi zinazoendelea zenye huduma kama hizo ni pamoja na China, Thailand,...

  Asiyeweza kulipia daraja apande pantoni au apige mbizi :]
   
 7. mwanamapinduko

  mwanamapinduko Senior Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 174
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Suala la kulipia hilo daraja, hii imekula kwa nssf sijui kama walifanya upembuzi yakinifu kuhusu huu mradi. Waziri wa ujenzi na mkurugenzi wa nssf wote wana shahada ya uzamivu, je hawkuliona hili?
   
 8. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa hakutakuwa na gharama ya uendeshaji kwa daraja halitakuwepo kama feri labda kuwe na muda maalum wa kulipia ili kurudisha pesa za NSSF
   
 9. k

  kiche JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani kazi ya NSSF ni kujenga madaraja!!!?uwekezaji mwingine NSSF lazima wawe makini!umeme naona kama umewashinda!!wamekimbilia madaraja!si ajabu ukasikia siku moja wanatafuta tenda ya kuingiza vifaa vya kijeshi!!NSSF waelewe kuwa moja ya kazi ya serikali ni kuhakikisha nchi inapitika ikiwa ni pamoja na madaraja,mimi kulipia daraja kabla ujapita siungi mkono.

  Nadhani uelewi matumizi ya kodi tunayolipa,kumbuka kuwa kila unachonunua unalipia kodi hivyo ujenzi unapofanyika ni kodi yetu hata kama wakilipana kwa njia gani mwisho wa yote kodi itatumika,kazi ya ujenzi wa miundombinu (barabara na madaraja) tuiachie serikali,mizunguko hii ya sasa ndiyo inazaa 10% na gharama zinakuwa juu,kumbuka NSSF wapo kibiashara.
   
 10. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa kigamboni waombe posho iongezwe kwasababu gharama za maisha kigamboni zimeongezeka. Mamlaka husika zijiandae kutoa leseni za mbizi na zitangaze mapema mwisho wakupokea maombi ya hizo leseni la sivyo tutaenda kwa azam kuomba lifejacket!!!
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hivi una habari uko kigamboni palishauzwa sasa mkitolewa mnaanza oohh hamna sehemu ya kutupeleka sasa sirikali imeamua kuwaondoa raia kigamboni kiaina bila ya utata mbalatata..
   
 12. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Suala la kulipia madaraja fulani liko kwa baadhi ya nchi, ila kwa hili la nssf nadhani kutakuwa kuna bonge la mkakati wa kifisadi hapa (usimamizi wa mapato ya malipo hayo lzm uwe chini ya mafisadi papa wa nchi hii) Kinachoudhi kwa nchi hii ni pale watawala wanapokomalia kuiga kwa mataifa ya nje inapokuwa tu kwa hasara ya wananchi! Inapokuja kuwaiga kuhusu uwajibikaji na hatua kali dhidi ya viongozi wazembe na wezi, wanakwambia desturi zetu ni tofauti na za hayo mataifa mengine!!
   
 13. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  na wale wanachama wa Nssf ambao hela zao ndio wanajengea ...watalipishwa?
   
 14. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,215
  Likes Received: 1,335
  Trophy Points: 280
  Kodi 2nalipishwa pesa zinafanyiwa nini sasa.SO DARAJA LITAJENGWA NA WANANCHI,NSSF AU SERIKALI
   
 15. +255

  +255 JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Mkuu inamaana wataweka kizuizi sehemu, ukishalipia ndo unapita (ka ilivyo stand ya Mwenge daladala ikiwa inatoka) au huwa kuna utaratibu mwingine wa malipo, manake naona kama ni kwa mtindo huo si utasababisha jam?!
   
 16. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,215
  Likes Received: 1,335
  Trophy Points: 280
  mkuu unatakiwa kutofautisha kati ya inchi iliyoendelea na inayoendelea siyo unaongea tu
   
 17. s

  sawabho JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hivi wanachama wa NSSF wanafaidikaje na hiyo miradi?
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tanzania,tanzaniaaaaaaaa nakupenda kwa moyo woteeeeeeeeeee.......
  nchi yangu tanzaniaaa jina lako ni tamu sanaaaaaaaaaaaaaa x2
  nilalapo nakuwaza weweeeee.
  niamkapo ni heri mama weeee.
  tanzania tanzania jina lako ni tamu sanaaa...........

  nikiukumbuka huu wimbo machozi yananitoka.
  hawa viongozi walikuwa wanaomba mwalimu afe ili waiuze hii nchi?
  je wanafikiri baada ya dhulma hizi dhidi ya wanyonge wao na familia zao wwatapona?

  ee mungu nipe maisha marefu ili niushudie mwisho wao.
   
 19. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tembea duniani uone ndio uanze kupiga kelele.
  Hiyo dunia uliyotembea ni ipi?>
  Nchi nyingi sana zina huu utaratibu na wewe ndio wa kwanza kushangaa.
  Kweli ushamba ni mzigo mkubwa.
  OTIS
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kile ni kitega uchumi cha NSSF na wala si suala la miundombinu ya serikali unless NSSF inajitoa basi suala la kulipia halitakuwepo......sehemu nyingi tu duniani mabao haya yapo......suala ni kiasi gani tutalipia
   
Loading...