Hii imekaaje? Ushauri unahitajika

Hii imekaaje? Ushauri unahitajika

bahati mbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
578
Reaction score
193
Habari za majukumu wana Jamii forum.

Kuna jirani zangu karibu na maeneo ninayoishi, mwanaume hawajibiki katika familia, ulipoonza mwaka huu mwanamama akamwambia mme kuwa mwaka mpya na mambo mapya. Mwanaume kama kawaida yake anaondoka nyumbani anakwenda kwenye mishemishe zake nyumbani haachi kitu wala kodi ya meza.

Mama akawaambia watoto wapike chakula kidogo na wale mapema maana hata yeye ni mfanyakazi akirudi anakuwa ameishakula maana anajua nyumbani share yake haipo.

1. Siku ya kwanza baba kakuta yamebaki kama matonge mawili ya ubwana na mboga iliyobaki akafakamia na
kuingia kulala.

2. Siku ya pili akawahi kidogo akakuta watoto wanamalizia kupika alivyotoka sebuleni akakuta wameishamaliza kula.

3. Tangu wakati huo ameamua kuwa anakula mtaani anarudi nyumbani kulala tu.

Swali kuu ni kwamba nini kifanyike katika maisha ya namna hii??? Kula mtaani ni suluhisho?

Ushauri wenu unahitajitaka katika hili.
 
Mme kutoacha hela na kula magengeni ni UJI.NGA!
...
Hapo cha kufanya ni kukomoana tu! Ushe.nzi mwengine ukiwa mkali ndio dawa yake!
Ebbos! Kwani huyo me hajui kama anawajibu wa kuacha hela ya kula na matumizi mengine ktk familia yake?
 
Nakuomba sana muite huyo jamaa, polepole mweleze kuwa anapaswa kufanya kazi ailee familia yake na sio amfanye mkewe bread winner daily. Atakuja kula chakula kilichotokana na hongo ya ngono asipoangalia. Asipoelewa wewe pita hivi >> uachane naye.
 
Hapo ndiyo mjue kuwa wanaume wengine ni mizigo ya misumari maana huna pakuuegesha na haubebeki kabisa.
 
Huyo inaonekana ameshaambiwa na kutokusikiliza

Kuna watu wengine bila kuumia hawajifunzi

Huyo dawa yake anatakiwa akirudi akute huyo mkewe ameshaondoka na wanae na kwenda kuanzisha maisha mengine,kuishi na mtu wa aina hiyo ni kujiingiza kwenye dhambi zisizohitajika

Wamuache na kuondoka zao tena wakombe kila kitu halafu waone atafanya nini

Ila kuna wanaume wengine wanatuaibisha kabisa!!
 
Eiyer na Arushaone, wanawake sie viumbe wa ajabu sana. Yaani unakuta kuna mwanamke, anapigwa kila siku na mumewe, cheatings ni serial kama marichui. Ila siku unagundua kumbe mwanaume hachangii ada wala msosi wala maziwa ya mtoto, unabaki kujiuliza alibakia hapo akingojea nini? Huwezi nishawishi hata soul food unaenjoy na mtu ambae unatumia mbinu za msituni kuhakikisha hali ubwabwa wako ulionunua.

Nakubaliana nanyi, ila kabla ya kuhama inabidi wakubaliane na pengine kumhusisha mtu mzima wa karibu. Kusudi huyo bwana asije akadai mke wangu kahama home kwa sababu ana kidumu. Dawa ya huyo mwanaume ni kumtimua yeye, wala sio kuhama. Manake anakuja kulala tu, akasake kitanda kwingine. Ila mkewe sina hakika kama atakubaliana na hilo aisee.
 
Last edited by a moderator:

Wanawake nyie mna tatizo kubwa sana la utegemezi wa hisia,hili ndili linawafanya mnafujwa kila uchao

Kwenye ishu ya huyu mama,ukweli ni kwamba huyo mama ndie msimamizi wa familia na pia ndio kila kitu,sidhani kama kuna haja ya kumshirikisha yoyote yule.Huyo mama ni kusepa tu hakuna kingine na akishasepa huko atakapofika atulie na kama huyo jamaa atasema kuwa amwfanya hivyo kwasababu ana kidumu to hell

Huwezi kumlazimisha yoyote yule kukuamini ila wewe ndio unaejua ukweli na bahati nzuri kuna watu wengine pia wanalishuhudia hilo hivyo sioni tatizo

Kama huyo ----- atakuja kumletea fujo huyo mama kuna vyombo vya kisheria na anaweza kuwajibishwa,ki ukweli dada yangu najisikia vibaya sana kwenye hili suala

Hivi inakuwa je mtu unataka upate K bure ulishwe na kulala pia bure halafu unavaa suruali na kujiita mwanaume
***** zake huyo jamaa ........!!!!!!!
 
Eiyer na Arushaone, wanawake sie viumbe wa ajabu sana. Yaani unakuta kuna mwanamke, anapigwa kila siku na mumewe, cheatings ni serial kama marichui. Ila siku unagundua kumbe mwanaume hachangii ada wala msosi wala maziwa ya mtoto, unabaki kujiuliza alibakia hapo akingojea nini? Huwezi nishawishi hata soul food unaenjoy na mtu ambae unatumia mbinu za msituni kuhakikisha hali ubwabwa wako ulionunua.

Nakubaliana nanyi, ila kabla ya kuhama inabidi wakubaliane na pengine kumhusisha mtu mzima wa karibu. Kusudi huyo bwana asije akadai mke wangu kahama home kwa sababu ana kidumu. Dawa ya huyo mwanaume ni kumtimua yeye, wala sio kuhama. Manake anakuja kulala tu, akasake kitanda kwingine. Ila mkewe sina hakika kama atakubaliana na hilo aisee.

atizo kubwa hata pale wanapoishi ni nguvu ya mwanamke,&nbsp; mwanaume mchango wake ni mdogo sana katika nyumba hiyo wanayoishi hivyo nakubaliana na King'asti kuwa mwanaume ndiye anatakiwa kuhama maana inawezekana kuna sehemu amewekeza nje ya nyumbani kwake.<br><br>Haiingii akilini ukamtegemea mke kwa kila kitu tena bila kukubali mchango wake kama mme.
 
Kuna jirani zangu karibu na maeneo ninayoishi, mwanaume hawajibiki katika familia, ulipoonza mwaka huu mwanamama akamwambia mme kuwa mwaka mpya na mambo mapya.

Mkuu hapa unahitajika ushauri gani wakati inaonesha hao wanandoa wamepanga na kuamua kuishi hivyo...!!!

Au wamekutonya kuwa kwao hayo maisha wanaona yana kero?
 
Mkuu hapa unahitajika ushauri gani wakati inaonesha hao wanandoa wamepanga na kuamua kuishi hivyo...!!!

Au wamekutonya kuwa kwao hayo maisha wanaona yana kero?

Siyo kuwa wamepanga mama wa watu kachoka na aina hiyo ya maisha ndiyo maana amejaribu kubadili mbinu ili aone kama jamaa atajitambua, kumbe ndiyo anazidi kuongeza matatizo.
 
katika wanaume sidhani kma huyu anaweza jiita mwanaume ,... sio kabisa
 
Siyo kuwa wamepanga mama wa watu kachoka na aina hiyo ya maisha ndiyo maana amejaribu kubadili mbinu ili aone kama jamaa atajitambua, kumbe ndiyo anazidi kuongeza matatizo.

Amekaa na mumewe kutafuta suluhu ya jambo hilo?
 
jamani duniani kuna mambo
hivi mwanaume kweli kwa akili timamu hujui majukumu yako katika familia?
hivi wanaume wengine wana niini jamani au ndo kujiendekeza au ndo kukataa kuwajibika
kilichokupelekea mpaka ukaoa na kumzalisha mwenzio watoto ndo nini huku unakataa
majukumu yako ya kulea hiyo familia yako

Huyyo jamaa anahitaji kufanyiwa uchunguzi huenda kuna ulakini ndani ya ndoa yao
 
Amekaa na mumewe kutafuta suluhu ya jambo hilo?

Wameishapita njia nyingi sana, Wasimamizi wa ndoa, Serikali za mitaa na Kanisani, Jamaa anaonekana kutojitambua kabisa maana kuna kikao kimoja cha usuluhishi aliwahi mwambia mke wake kuwa wewe unawezo wa kuhudumia familia? nikiondoka kwa wiki moja utaweza mudu huduma? wakati ukweli anaujua. Pia ana maneno ya kashifa sana pale wanapogombana na mkewe. Maana akianza matusi anatukana ukoo mzima wakati yeye yupoyupo tu bila msaada wowote katika familia.

Imefikia ikitokea akasafiri watoto wanafurahi maana akiwepo ni kero na vitisho hata kwa watoto ili kujenga Defence mechanism.
 
Kumbe wameshapita kote huko, basi waacheni waendelee hivyo hivyo

Wameishapita njia nyingi sana, Wasimamizi wa ndoa, Serikali za mitaa na Kanisani, Jamaa anaonekana kutojitambua kabisa maana kuna kikao kimoja cha usuluhishi aliwahi mwambia mke wake kuwa wewe unawezo wa kuhudumia familia? nikiondoka kwa wiki moja utaweza mudu huduma? wakati ukweli anaujua. Pia ana maneno ya kashifa sana pale wanapogombana na mkewe. Maana akianza matusi anatukana ukoo mzima wakati yeye yupoyupo tu bila msaada wowote katika familia.

Imefikia ikitokea akasafiri watoto wanafurahi maana akiwepo ni kero na vitisho hata kwa watoto ili kujenga Defence mechanism.
 
Jamaa anaonekana kumganda mama wa watu maana kwa mwanaume aliyekamilika hawezi kuwa na tabia za namna hii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom