Hii imekaaje? Clouds Radio na EFM kuendesha kamari katika vipindi vyao?

Lady Mwali

Senior Member
Nov 15, 2018
147
332
Kumekuwa na tabia watangazaji wa vipindi vya redio Clouds na E.fm kuchezesha kamari katika kila vipindi.

Kwa nyakati tofauti watangazaji hao wamekuwa wanawashawishi wasikilizaji wao wawe mamilionea kwa kuwaambia watume pesa kwa namba wanazozitaja huku wakitaja dau.

Mwisho wa vipindi huwapigia simu washindi baada ya kucheza droo.

Hivi leseni zao zinaruhusu kuchezesha kamari?
 
Sijafahamu hiyo tabia wameitoa wapi, inawezekana wameona wajiongeze kijanja kutokana na mdororo wa kiuchumi uliotokana na Corona.

Matangazo yamekuwa kidogo kutoka kwa wadau walewale, hivyo wameona wajiongeze kwa kuwaibia kijanja watanzania, unampa mshindi milioni moja au laki tano, halafu wewe unabaki na milioni mbili, au mbili na nusu kwa kila kipindi.

Kama mshindi ni wa mchongo basi pesa yote inabaki hapo hapo redioni, watanzania wanachangia mishahara ya wajanja bila kujua, wanaliwa wakiwa wanashangaa.
 
Watu wanajiongeza. Wewe Kama umestuka kausha. Mpaka wakamuliwe wajinga waishe watu washajenga mahekalu mbweni
 
Kumekuwa na tabia watangazaji wa vipindi vya redio Clouds na E.fm kuchezesha kamari katika kila vipindi.

Kwa nyakati tofauti watangazaji hao wamekuwa wanawashawishi wasikilizaji wao wawe mamilionea kwa kuwaambia watume pesa kwa namba wanazozitaja huku wakitaja dau.

Mwisho wa vipindi huwapigia simu washindi baada ya kucheza droo.

Hivi leseni zao zinaruhusu kuchezesha kamari?

Kwan kamali hizo kodi zinalipa?kama ndyo bac kaa kwa kutulia
 
Kumekuwa na tabia watangazaji wa vipindi vya redio Clouds na E.fm kuchezesha kamari katika kila vipindi.

Kwa nyakati tofauti watangazaji hao wamekuwa wanawashawishi wasikilizaji wao wawe mamilionea kwa kuwaambia watume pesa kwa namba wanazozitaja huku wakitaja dau.

Mwisho wa vipindi huwapigia simu washindi baada ya kucheza droo.

Hivi leseni zao zinaruhusu kuchezesha kamari?
Hili hata mimi nilishawahi kumuuliza mke wangu akabaki anashangaa tu,jamaa hawa siku hizi kila kipindi chao chochote kile hadi vya usiku wa manane lazima droo ya kamari ichezeshwe,yaani nimegundua ndio ubunifu mpya walionao,kula yao inapitia kwenye kamari,matangazo yamebuma,hali ngumu
 
Hicho ndo kinanifanya nisiweze kusikiliza hivyo vituo Coz sipendi kamari za namna hiyo ambazo sijui zinavyochezeshwa kupata mshindi
 
Back
Top Bottom