Radio One nayo yachezesha kamari

Radio One nayo yachezesha kamari

Joined
Jul 3, 2020
Posts
29
Reaction score
65
Hivi masharti ya leseni ya urushaji matangazo ya redio ya TCRA inaruhusu vituo vya redio kuwa na michezo ya kubahatisha/kamari?

Maana kila redio ina kamari yake, Efm ,Clouds FM,Wasafi na sasa Radio One( Mchezo Supa).

Watangazaji wa redio hizo kila kipindi wamekuwa wanachezesha droo mwisho wa kipindi baada ya kuwashawishi wasikilizaji wao watume pesa tsh 1000 kupitia mitandao ya simu.

Baada ya kupatikana mshindi wanampigia simu live redioni na kumtaarifu ameshinda pesa.

Swali langu hivi vituo vya redio imekuwaje vinachezesha kamari havioni vinawakwaza baadhi ya wasikilizaji ambao dini zao kamari ni haramu? Mathalani dini ya Kiislam kamari ni haramu na dhambi kubwa.

Hivi vituo vya redio vijitathmini.
 
Salvation requires perfection!

This is the danger of being a hypocrite; that is - to blame others while yourself being guilty of other deadly sins - lust, gluttony, sloth, envy...
 
Napenda kusikiliza Radio ila haya matangazo ya Kamali kwa kweli imekua kero kwangu, muda mwingi wanaongelea kamari tu..... kidogo kamari kidogo kamari kha!!!
 
Zimegundua ni fursa kama timu za yanga na simba zimeweza kukusanya million hadi 100 kupitia ujenzi wa viwanja kwa kutuma buku buku ndani ya wiki 2. Ata wao wanaweza ikusanya iyo au nusu yake ndani ya wiki mbili.

Ni fursa wameiona
 
Hivi masharti ya leseni ya urushaji matangazo ya redio ya TCRA inaruhusu vituo vya redio kuwa na michezo ya kubahatisha/kamari?

Maana kila redio ina kamari yake, Efm ,Clouds FM,Wasafi na sasa Radio One( Mchezo Supa).

Watangazaji wa redio hizo kila kipindi wamekuwa wanachezesha droo mwisho wa kipindi baada ya kuwashawishi wasikilizaji wao watume pesa tsh 1000 kupitia mitandao ya simu.

Baada ya kupatikana mshindi wanampigia simu live redioni na kumtaarifu ameshinda pesa.

Swali langu hivi vituo vya redio imekuwaje vinachezesha kamari havioni vinawakwaza baadhi ya wasikilizaji ambao dini zao kamari ni haramu? Mathalani dini ya Kiislam kamari ni haramu na dhambi kubwa.

Hivi vituo vya redio vijitathmini
Miswahili bhana wasipofanya hivyo Mishahara yao utawalipa Wewe na Mkeo?
 
aisee kweli kila radio siku hizi inachezesha kamali
 
Back
Top Bottom