Radio One nayo yachezesha kamari

Jul 3, 2020
30
63
Hivi masharti ya leseni ya urushaji matangazo ya redio ya TCRA inaruhusu vituo vya redio kuwa na michezo ya kubahatisha/kamari?

Maana kila redio ina kamari yake, Efm ,Clouds FM,Wasafi na sasa Radio One( Mchezo Supa).

Watangazaji wa redio hizo kila kipindi wamekuwa wanachezesha droo mwisho wa kipindi baada ya kuwashawishi wasikilizaji wao watume pesa tsh 1000 kupitia mitandao ya simu.

Baada ya kupatikana mshindi wanampigia simu live redioni na kumtaarifu ameshinda pesa.

Swali langu hivi vituo vya redio imekuwaje vinachezesha kamari havioni vinawakwaza baadhi ya wasikilizaji ambao dini zao kamari ni haramu? Mathalani dini ya Kiislam kamari ni haramu na dhambi kubwa.

Hivi vituo vya redio vijitathmini.
 
Mnyakyusa Ipinda

JF-Expert Member
Dec 9, 2020
282
1,062
wameiga Kenya, huko Kenya walianza hayo mambo kitambo yani kila Radio ni hiyo.michezo na wanaingiza pesa sanaaaaaaaaa yani ndio miradi mipya ya kuingiza pesa kwa Radio station na zinalipa kuliko unavodhani mkuu, sema washindi wa mchongo utatuma na kutuma ila hakuna siku utashinda.

Ni bahati nasibu hata hivyo jaribuni bahati zenu vijana, huezi jua.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
 
wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
13,157
28,507
Serikali ipige marufuku wkt haina uwezo wa kuzalisha ajira, matokeo ya unemployment rate kua kubwa Ni vijana kuanza kufikiria Kwamba buku Yake inaweza kumpa 1mil.
 
Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
2,410
2,447
Walianza clouds nikaihama....nikarudi kiss fm napo leo nimesikia wameanza matangazo ya kamar sijui nihamie wapi maana TBC taifa napenda kipindi cha pwagu na pwaguzi tu....
 
OllaChuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
18,906
20,665
Hahahah Ile mchongo pesa ya clouds aise wale jamaa wanapiga hela na wamefanikiwa sana ..ngoja tuone hii ya radio one kama itafua dafu.
 
0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
3,418
8,152
Nilijua tu lazima kila redio itakuja kuiga,maana kwenye redio zetu kila kitu wanaigana sahv karibia redio zote zinafanana vipindi

Seeikali haiwez kuzuia kwasababu inapata asilimia 20 kwa kila pesa inayotoka,kumbuka serikali yetu ina zero brain wengi hawajui kubuni mapato ya serikali kwahyo wanapopata gap za kupata hela kama hz hawawez kuziacha
 
alphonce.NET

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,084
1,034
Hivi masharti ya leseni ya urushaji matangazo ya redio ya TCRA inaruhusu vituo vya redio kuwa na michezo ya kubahatisha/kamari?

Maana kila redio ina kamari yake, Efm ,Clouds FM,Wasafi na sasa Radio One( Mchezo Supa).

Watangazaji wa redio hizo kila kipindi wamekuwa wanachezesha droo mwisho wa kipindi baada ya kuwashawishi wasikilizaji wao watume pesa tsh 1000 kupitia mitandao ya simu.

Baada ya kupatikana mshindi wanampigia simu live redioni na kumtaarifu ameshinda pesa.

Swali langu hivi vituo vya redio imekuwaje vinachezesha kamari havioni vinawakwaza baadhi ya wasikilizaji ambao dini zao kamari ni haramu? Mathalani dini ya Kiislam kamari ni haramu na dhambi kubwa.

Hivi vituo vya redio vijitathmini.
Hata kama wasingechezesha kamali hakuna jambo la hekima linalofaa kusikilizwa na muumini wa dini kwenye Radio za Tanzania kwa sasa

Muda wote wanapiga muziki wa matusi
 
Whitney Houston

Senior Member
Jan 5, 2019
168
297
Hata kama wasingechezesha kamali hakuna jambo la hekima linalofaa kusikilizwa na muumini wa dini kwenye Radio za Tanzania kwa sasa

Muda wote wanapiga muziki wa matusi
wewe ndo umejitakia shida.Usisikilize hzo badala yake sikiliza za kidini mf.Radio maria n.K au badili masafa basi usikilize za nje ya tanzaland.Wew hupendi za nyimbo za matusi lakin wanaopenda wapo wengi tu na wao dini haipandi the same kama wew ulivohupendi nyimbo hzo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom