Hii ilikuwa siku ngumu kwangu!!

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
mawazo.JPG


Hii siku kweli ilikuwa ngumu sana....nilikuwa nasubiria mke wangu ajifungue, nilichanganyikiwa...hapa ni ofisini sikuwa najua nilichokuwa nafanya...hii picha nilipigwa na wenzangu bila hata kujua!!! Namshukuru Mungu alijifungua salama.....kweli mtoto anayemdharau Mama yake anafanya kosa kubwa sana!!!
 
Na huo moyo wa kukaa ofisini ulikua nao...!! wengine hatutoki mlango wa Labour
 
mwenzio niliingia labour room mpaka wife alipojifungua, toka siku ile aisee tupo km mapacha, namheshimu sana wife ni vile tu mama yangu alifariki nikiwa mdogo sana kweli ningempa na yeye zawadi kubwa tu. nawaheshimu sana akina mama, yale masaa niliyokaa pale mpaka mtoto anatoka km huna mungu mh! Kweli namtafutia wife surprise ya kufa mtu.
 
Sasa mkuu ulikuwa umekomaa ofisini badala ya kwenda chumba cha labour kumsaidia mwenzio kupush
 
Hongera kwa kupata mtoto kaka. Furaha ya huyo baby ukizubaa mwakani mwezi kama huu unarusha picha nyingine kama hii.
 
kaka pole na hongera sana kwa kupata mtoto. askwambie mtu kuzaa hasa kwa njia ya kawaida jamani kunatisha. yaani mpaka mtoto atoke kazi inakuwa kazi, ukimuona mama yeyote aliye zaa muheshimu sana manake that is the last thing some one can do just for the sake of somebody else. Mothers tend o risk their lives just for the sake of their lovely kids some of them die on the way or some are subjected to physical impairment and some wanapita salama. As a return watoto wengine si wakike wala kiume wana geuka na kuwa mbogo, wakaidi , jeuri na hata kuwapiga na kuwadhaliaalisha mama zao.

anyway maisha ndivyo yalivyo ila ukweli akina mama tunapita pagumu sana, Mungu tu ndiye huwa mlinzi na tegemeo letu.

binafsi hata yale maneno yenye lugha za utusi za kuelekeza kwa mama huwa sizipendi hata kidogo. Bahati mbaya sana akina kaka na baba wanapenda kweli lugha hizi ila laiti mngelijua thamani ya hicho mnachokitukana na kazi yake msinge kitaja hovyo. Yaani kutaja ya mama imekuwa ni kawaida asana kama vile kutaja jicho au mkono cha ajabu ya baba iko sirini inaheshimiwa haitajwi halafu hii hii ya mama ipitishe mtu aje awe raisi wako, mwl wako, dr wako mchungaji nk kweli hii ni haki?

nisamehewe tu kwakua nimeingia chaka na siyo mahali pake ila mtoa mada amenikumbusha mbali sana na naona uchungu sana juu ya hili. Mimi ni mtu poa sana ila ukitaka kuona sura mbaya ya kwangu nitukane kupitia ya mama ama nikuskie ukimtukana mtu ya mama.
 
Mimi vipindi kama hivyo nilikuwa natumbukiza BINGWA kwa wingi kwa tahadhari ya chochote kitakachotokea!
 
Na huo moyo wa kukaa ofisini ulikua nao...!! wengine hatutoki mlango wa Labour

Mkuu ofinisi hapakukalika nikatoka kwenda kukaa mlango la Labor...mtoto alipolia niliruka kama mwenda wazimu!!
 
Katika majukumu ambayo wanandoa wamegawana katika kuipata familia na kuilea familia n.k hili ndiyo jukumu la muhimu na GUMU sana ambalo walipewa na MUNGU kinamama pekee yao walifanye. Hata ukijifnya kumhurumia vipi huwezi kufikia uchungu wa masaa kadhaa wanayokumbana nayo kina mama. Kina MAMA oyeeeeee
 
Sasa mkuu ulikuwa umekomaa ofisini badala ya kwenda chumba cha labour kumsaidia mwenzio kupush

Mkuu Fidel80 hizo nguvu nilikuwa nazo sasa?? halafu kuna jamaa waliniogipesha kuwa nienda wife anaweza anirarue kutokana na maumivu aliyokuwa anapiti...wakanipa mifano mingi...jamaa mmoja alivutwa Pu*mb* na Wife wake kidogo atoke nazo...mwingine aligigwa kibao mpk akadondoka chini....mwingine aling'atwa sikio n.k nikaogopa kwenda!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom