Hii hii hii nakudanganya..... KESHAKUFA

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,834
Jamaa kapigiwa simu kuwa mkewe kapata ajali yuko hospitali. Kufika huko kamtafuta akaelekezwa aende emergency kuna daktari anamshughulikia. Akamkuta daktari;
JAMAA: Dokta vipi mke wangu
DOKTA: kwa kweli hali yake si nzuri, kavunjika uti wa mgongo sehemu mbili, kwa hiyo hataweza tena kujitegemea.
JAMAA: Masikini mke wangu...machozi yakaanza kumtoka
DOKTA: Kwa hiyo atakuwa mtu wa kulala tu, na italazimu umgeuze kila baada ya masaa mawili ili asipate madhara ya vidonda. Na utalazimika kumlisha na kwa kuwa hawezi kuamka, atakuwa anajisaidia kitandani ni muhimu kuweka kitanda kiwe safi kila nusu saa, pengine italazimu awe na nepi uwe unambadili kila robo saa....Jamaa sasa alikuwa analia kwa nguvu waziwazi.
DOKTA : Hahahahaha nakudanganyaa, usilie hivyo KESHAKUFA
 
Back
Top Bottom