Mkasa wa doctor Mellus Tshube inaumiza sana!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Alikuwa kawaida tu.

Hakuonekana kuwa na msongo wa mawazo.

Aliendelea na shughuli zake za kila siku kama kawaida. Hata, Feb 2 mwaka huu, alipost picha akiwa na mkewe katika hali ya mahaba.

Alikuwa baba wa familia ya watoto wawili; kijana Isago Tshube (7) na binti Entle Tshube (2) na mume wa Bi. Boipelo Gala Tshube.

Tunamzungumzia Dokta Mellus Tshube.
Daktari kijana tu aliyeacha simulizi ya kusikitisha sana kwa wakazi wa jiji la Gabarone, Botswana. Jumamosi ya wiki iliyopita.

ILIKUWAJE?
Inasemwa, kulikuwa na kutokuelewana baina ya wanandoa hawa, Tshube na mkewe, mchana wa siku ya Jumamosi.

Huko kutokuelewana kukazalisha vita ya majibizano iliyoendelea mpaka jioni. Vita baina yao ilipochemka barabara na kuiva wakati huo usiku ukiwa umeshabisha hodi, Tshube alimtimua mkewe ndani ya nyumba kisha yeye akajifungia ndani na watoto wao wawili.

Akiwa huko ndani, Tshube alianza kutuma meseji kwa marafiki, familia na majirani. Meseji za kuwajulisha juu ya uamuzi wake wa kuukatiza uhai wake. Aliingia hadi Facebook akaandika majina ya watu aliowatuhumu kutembea na mkewe, akamalizia na neno I'm out! Yaani kama vile anawasusia huyo mwanamke moja kwa moja.

Huku nje, Bi. Boipelo hali ilikuwa moja haikai mbili haisimami. Alikimbilia kwa majirani kwa mayowe ya kuomba msaada akihofia mumewe anaweza kweli kufanya kitu kibaya kwake na watoto aliojifungia nao ndani, huku akituma meseji za kuigongea hodi akhera.

Wakapiga simu polisi.
Ambapo mpaka wanafika, tayari Dr. Mellus Tshube alikuwa ameshawaua watoto wake wawili na yeye kujinyonga.

Walivunja mlango wakaingia ndani. Wakakuta miili ya watoto imelala chini kama vipande vya kuni, ikiwa haina uhai tena. Mwili wa baba yao ukiwa unaning'inia darini, kwenye kile kisehemu ambacho huwa kinabaki kama kimlango cha kuingilia huko darini. Huku vipande vya kamba viwili vilivyobakia baada ya kukatwa vikiwa vinaning'inia karibu yake.

Kwamba, aliwanyonga watoto wake kwanza, walipokata roho akakata kamba alizowanyongea vikabaki vipisi juu, miili ikaenda sakafuni, akapanda yeye kujimaliza. Pasi huruma wala majuto.

Polisi wanasema, simu yake ya mwisho kupiga ilikuwa saa sita na nusu hivi usiku. Alimpigia mwanafamilia.

Basi, ikabidi Boipelo apelekwe nyumbani kwao kwa ajili ya usalama wake. Ilhali, wale waliotajwa na marehemu katika ile post ya Facebook wakitakiwa kuhojiwa ili kuisaidia polisi. - source gazeti la Botswana Guardian.

TATIZO LILIKUWA NINI HASA?

Wivu wa mapenzi?
Wanasema hivyo. Mwanamke alikuwa na watu. Alikuwa ana-flirt nao. Mwingine mpaka Dr. Tshube alikwenda kumwomba akae mbali na mkewe. Ikawa kama kumpigia mbuzi zumari. Yaani, mke wa mwenzake alikuwa kama mkewe ilhali naye ni mume wa mtu.

Hilo, lilimuuma mno Dr. Tshube. Kudharauliwa na mwanaume mwenzake waziwazi. Ilimchoma tumbo na utumbo.

Katika kusakanya taarifa zaidi. Nikagongana na habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Dr. Tshube ambaye alishare ujumbe wa mazungumzo kati yao. Zilikuwa Meseji za marehemu juu ya hali ya ndoa yake ilivyokuwa.

Katika moja ya meseji alizotuma Dr. Tshube kwa rafiki yake enzi za uhai wake, ilikuwa ni ya malalamiko juu ya tabia ya mkewe.

Katika meseji hizo inaonekana Tshube aliwahi kufanya usaliti a.k.a ku-cheat na kukamatwa na mkewe. Lakini, akaamua kubadilika, kutulia na kujenga uaminifu ili kuimarisha familia yake. Lakini, mkewe sasa akaamua kufanya kitu kama kisasi. Hakushikika!

Yawezekana ndiyo sababu ya Dr. Tshube kujaribu kuvumilia mengi yanayoonekana kutovumilika.

Kuna sehemu aliongea kwa uchungu sana namna ambavyo anajitahidi kupambana na maisha ili kumpa mahitaji yake ikiwemo kuwa wa kisasa mitandaoni na kwenda kila tukio.

Tshube alilalamika, tatizo kubwa ni simu ya mkewe. Mara nyingi inawekwa Flight Mode akiwa nyumbani, na ikitokea simu ikaingia mkewe hawezi kuongea nayo akiwepo. Akakiri wamekwama kwenye usaliti ambao si ajabu ndiyo utakaowamaliza.

Kuna jamaa alimkamata naye, ghafla akawa haonekani simuni. Tshube alipopeleleza akagundua bibie amembadilisha jina kwenye contacts. Mke akajitetea kuwa ni rafiki tu kwa sasa hawakutani tena kimwili. Dokta akasema hadanganyiki. Akaweka kilugha chao hapo, ke lebile hela yaana. Paparazzi nikatoka kapa.

Inaonekana Tshube aliunganisha whatsapp ya mkewe na simu yake kwa hiyo akawa anajua kinachoendelea moja kwa moja. Rafikiye alimsihi aachane na kumfuatilia kwa njia hiyo, kwani itamuua ikiwa yeye Tshube alikuwa kupambana kujiponya msongo.

Tshube alisema itamfanya ashindwe kujua kinachoendelea. Akakiri kukosea na kujitahidi kujirekebisha kwa alichofanya mwanzo. Kwa kudhihirisha hilo, ameiacha simu yake wazi, jambo ambalo mkewe ameshindwa. Aliitafuta password mpaka kaipata na kuongeza password ya kidole kwenye simu ya mkewe bila mke kujua.

Alisema, anaona jitihada ndogo mno kwa mkewe kumdhihirishia kuwa anarekebisha makosa yake kama yeye alivyojitahidi kujirekebisha baada ya kukosea kwa sababu anajua anahitajika kurejesha ule uaminifu wote. Kwa namna msongo ulivyomtafuna hata Therapy aliiona kama uzushi tu. Hatari sana!

Tshube na watoto wake wamezikwa leo Tar. 4 Machi, 2023
-------------

Ni mkasa ulioacha maswali mengi.
Kwa nini Dr. Mellus Tshube aue watoto?
Amefanya hivyo ili kumwadhibu mkewe, Bi. Boipelo?
Adhabu inayoondoa maisha ya watoto wasio na hatia?
Ameishi na hii hali na msongo huu akiteseka kwa muda gani?

Kila kitu kimezama. Namna hiyo.
Kila kitu kimeenda; ndoto, furaha, mipango na kila alichokipambania.

Aliyeonekana kuwa kawaida, hakuwa kawaida.
Walioonekana kuwa na furaha , hawakuwa na furaha.
Watoto wasiohusika kwenye usaliti, wameadhibiwa pasi na kosa.

Usaliti unauma sana. Usaliti ni kitu rahisi ukitenda si ukitendewa.

Sijui mkewe ana hali gani baada ya tukio hili. Wanaume wenzake wanajisikiaje sasa?

Wanasema mkewe kama alishindwa kusamehe, asingelipa kisasi hivi.
Wanasema wanawake tulieni basi. Hapa wanasema wanapoondoa dhana kuwa mwanaume alicheat. Kuna wanawake utulivu ni sifuri.

Basi walau kama Dokta hakuona mabadiliko kama aliyoyafanya yeye baada ya kukosea, angemtaliki tu.

Wanasema... wanasema... wanasema hivyo lakini ndiyo imeshatokea.

Huu ndiyo mkasa wa Dr. Mellus Tshube.
Mbotswana aliyeua watoto wawili na kujiua sababu ya mkewe.
 
Changamoto ya mambo ya ndoa kila mahali
Sasa jamaa kaamua kujikatisha uhai na watoto wake kisa mwanamke

Ova
 
Pole man!

Just Run!run and restart Life!!

Hiyo Ndio Njia PEKEE ya kujiokoa kwasisi tuliofanya makosa ya kuanzisha familia!!!

Run,Run goo wherever !muache na Watoto uwe unatuma matumizi tu KWA Watoto WAKO!!

Run just Run,are you listening boy!!!

You cant win if she has decided to spoil it!!

Run I say run!!
 
IMG_7914.jpg
 
Ndoa ni changamoto,nilivyoona Mke wangu hatuelewani ugomvi kila siku nilijua kinachofuata ni kama haya ya kuuana,nilimuachia nyumba ikiwa na kila kitu,nikawasha gari na kwenda kukaa sehemu nyingine kuanza maisha upya,leo ni miaka 12 kila mtu na maisha yake
Je mlikuwa na watoto!? Huko Maisha mapya ulioa Tena!? Je Kuna mawasiliano!?
 
Kwa kweli alifanya maamuzi ya ghafla sana. Ni bora hata angempa talaka ,wanawake wamejaa wengi. Licha ya maandiko matakatifu yakituhusia tuishi nao kwa akili,inaonesha dhahiri kuna changamoto kubwa kwa mwanamke katika maamuzi yake.
Sometimes kifo kina miujiza yake mkuu yaani hayo unayoyaongea hakuyawaza kabisa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli alifanya maamuzi ya ghafla sana. Ni bora hata angempa talaka ,wanawake wamejaa wengi. Licha ya maandiko matakatifu yakituhusia tuishi nao kwa akili,inaonesha dhahiri kuna changamoto kubwa kwa mwanamke katika maamuzi yake.
Kuna wengine wanaamini katika hadi kifo kitutenganishe. Wengine talaka haipo katika equations zao .We differ.
 
Ni jambo la kusikitisha na kutia uchungu sana!

Najaribu kutafakari, alipokuwa anawanyonga watoto, je, aliwalaghai kwa kuwasimamisha kwenye viti, na kuwavalisha vitanzi, ndipo akatoa viti na watoto kuning'inia na hatimaye kufa?

Kujiuliza huku kunafuatia kutoamini ukatili ambao sisi wanaume tunaufanya! Huyu Dr alikuwa katili kuliko mnyama simba au chui. Ni kweli alipitia wakati mgumu na kufikia kutoweza kuivumilia hali ile (tolerance limit), lakini kitendo cha kuwaua watoto kinadhihirisha alikuwa na tatizo lingine, tofauti na mgogoro wa ndoa.

Kama mtu ameshindwa kuvumilia tension fulani, si ajiue peke yake? Unaua watoto, wanakosa gani au wanahusika vipi na mgogoro wako? Na mgogoro wenyewe yawekana chanzo chake ni wewe mwenyewe (kama ilivyokuwa kwa Dr Shube), halafu unaua na wasiohusika!

Wengi wamefanya matukio ya kuu nia watoto kabla ya kujimaliza wenyewe. Wamekuwa wakiwaua watoto wao kwa namna tofauti tofauti; wapo wanaowapa sumu watoto wao (hili wanafanya sana akina mama), na wapo wanaowaua watoto wao kwa kuwapiga na vitu vizito.

Tujitahidi kushindana na msongo utokanao na tofauti kwenye ndoa zetu, na tusiwahusishe watoto wetu kwa namna yoyote ile kwenye migogoro ya ndoa zetu! Unanyonga watoto wadogo (malaika) wasiojua lolote! Inatia uchungu sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom