mshana jr... Unamaanisha kuwa sizitaki mbichi hizi?
Kalume kenge akataa kwenda shule
Hadithi za Alan quarterman na mashimo ya mfalme suleyman
Bulicheka
Hadithi za hesopo (Aesop's fables)
Boramimi
Majitu matatu
Kisiwa chenye hazina
Mmenikumbusha mbali saana
That time primary school nilisoma zaidi ya 200 books
Nakumbuka tukiwa std 5 themi tuliletewa vitabu kama sky jack over africa,Olu and the smuggle,Alibaba and 40 thieves,na vingine nimevisahau,nilivipenda mno,vilinipa hamu ya kupenda shule,vilinishawishi kujifunza kiingereza kwa bidii,kwenye sky jack palikuwa na picha moja naikumbuka,yule mtekaji(hijacker) akimshurutisha pilot ashushe ndege,pilot anamwambia"i cant do that"
Huu uzi nilikuwa naupita tu bila kuufungua nikidhani udaku wa siasa za Tanzania. But nimekuta ni kitu tofauti kabisa ambacho kimenikumbusha mbali saanaa, vitu kama
-Mfalme ana masikio kama ya punda
-Story ya Mzee tola
-Mwamba mwenye nguvu
-Twende tukawinde
-Sizitaki mbichi hizi
-Moyo na ndevu
-Jogoo aliyesema
-Ndoto ya kimweri
-Kambi ya kaboya
-Shairi Maarufu "Kama mkitaka mali"
-Barua kutoka kwa mjomba mdolwa
-Lindu amwokoa kapilima
-Brown ashika tama.
Na nyingine nyingiiii achilia mbali somo la English ambalo vitabu vyake vilikuwa kama movie series yaani unaanza na Mr&Mrs Daudi, Musa,Neema and Baraka na madarsa mengine characters ni hao hao tu. Dah imenikumbusha mbali sana, kipindi hicho tunasoma sayansi kimu,sayansi kilimo ,siasa na baadae uraia. Big up mleta uzi, kweli enzi hizo hazitajirudia tenaa
Twaweza kuvipata wapi Vitabu hivi na watoto wetu waweze faidi uhondo uliokuwa humo!?
Mkuu watoto wenyewe watavisoma basi, wasiangalie Chan. 5 (eatv) na TBC 2 au magazeti ya udaku waje wahangaike na Hekaya za Abunuwas au Alibaba na wezi 40 wapi na wapi? Mkuu hiyo imepita haitorudi
Wangu TV wanakutana nayo jumamosi na jumapili na wanapenda kusoma Vitabu na magazeti kama wafahamu vyapatikana wapi nijulishe!
Labda nikufahamishe tabia hizi za kujisomea hujengwa na wazazi kama wazazi mnatumia muda mwingi kwenye TV nao watatumia mkiwajengea mazingira ya kujisomea Vitabu hakika wajisomea!
Namshukuru Mungu kwakua napenda sana kujisomea vitabu tokea nikiwa mdogo hadi hii leo hua namuomba mdogo wangu vitabu vyake kila mwaka nijisomee hadithi.
Nilijua kusoma nikiwa mdogo sana, hadi leo nazikumbuka hadithi nilizozipenda sana...
1.Pete ya mtemi Ndamanga
2.Hawafu mwenye nguvu
3.Za mwizi arobaini
4.Machungwa ya bibi (sina uhakika na hili ila naikumbuka story yote) n.k
Bila shaka kitabu hiki kilikua cha darasa la 6 na ilikua mwaka 1999 na mimi nilikua chekechea!
Namshukuru Mungu kwakua napenda sana kujisomea vitabu tokea nikiwa mdogo hadi hii leo hua namuomba mdogo wangu vitabu vyake kila mwaka nijisomee hadithi.
Nilijua kusoma nikiwa mdogo sana, hadi leo nazikumbuka hadithi nilizozipenda sana...
1.Pete ya mtemi Ndamanga
2.Hawafu mwenye nguvu
3.Za mwizi arobaini
4.Machungwa ya bibi (sina uhakika na hili ila naikumbuka story yote) n.k
Bila shaka kitabu hiki kilikua cha darasa la 6 na ilikua mwaka 1999 na mimi nilikua chekechea!