Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,607
- 3,187
Wadau,
Miaka michache iliyo pita, kuna boat ilinunuliwa na tajiri mmoja kufanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba. Boat hii ilileta gumzo kubwa kwani Magufuli kama waziri wa ujenzi alikataa hiyo boat isisafirishwe kupitia barabara zetu kutoka Dar kwenda Mwanza kwa madai ya kulinda barabara. Hatimae boat hii ilisafirishwa kupitia Mombasa na mwisho ilifika Mwanza na kuanza safari zake kati ya Mwanza na Bukoba.
Nani anayejua hii boat ilipatwa na nini na kwa sasa iko wapi?

Kwa ninachokijua, baada ya kuletwa Mwanza zilianza safari kama kawaida, ratiba ilikuwa kutoka Mwanza saa 3 asubuhi mpaka Bukoba saa 9 mchana, nyingine ilikuwa inatoka kwa muda ule Bukoba, baadae ikawa saa 1, then saa 6 mza, thn saa 7, saa1 bkb, i mean go and return
Ajali ya kwanza ilipigwa na dhoruba kali kiasi cha kushindwa kufika kwa wakati, baada ya saa 6 za ratiba ikafka baada ya saa 10, (kumbuka kuletwa kwake kulitawaliwa na figisufigisu nyingi ivo iyo ikawa sababu ya kusimamishwa rasmi), boti ya pili ambayo iliendlea kufanya kazi ilipata tatzo la kuzimika injin ikiwa katikati ya ziwa siku moja mm nimetoka bukoba, ilibaki huko muda mwingi kuanzia asubuh saa 4, ilipata msaada saa 11, jion na abiria walifka mwanza saa 4, usiku, baada ya kuvutwa na mv ukerewe,
Baada ya pale boti zile zikasimamishwa rasmi tatizo jingine lilikuwa ni viwango vya nauli mfano kipindi icho nauli to Bukoba victoria ilikuwa
Daraja la tatu 8600
daraja la pil kukaa 10600
Daraja la pili kulala 12600
daraja la kwanza 23500
cabin ilikuwa 35000
Mabasi kipindi icho hayakuwa meng, mohamed trans na bunda ilkuwa arround 12000~15000, Wakati izo boti naul ilkuwa 23000~35000 kwa madaraja ya kwanza. Kwa hiyo kwa namna fulan kuahirbka kwa boti izo ambazo tuliambiwa zitapunguza muda mwngi wa safari ilikuwa kama kujichimbia kaburi kwa wamiliki.
Kifupi kulikuwa na comftability ya hatari, zilisafiri mchana watu kupata raha na kuangalia mandhari ya ziwa victoria, tofaut na meri ambayo ufanya safari usiku, haikuwa tofauti na kupanda fastjet ukiachilia mbali suala la muda. Boti hizi pia zilipunguza muda wa safari kutoka saa 13 majini ( mv victoria) na saa 14-15 (mv serengeti) mpaka saa 6.