Watu wengi sana wanawaza "kuwahi" kufika wanakokwenda. Nimesema muda mfupi kabla ya ajali tulikuwa tunaongea na Inspekta wa gari kuhusu ubovu wa gani lao.Poleni sana wakuu,lakini abiria mmoja angejitokeza kumsema dereva hakika angeshambuliwa na abiria wengine.
Wakati yule mama alipata msaada wa kupelekwa Hospitali kwa gari la TANAPA, Kijana alipanda gari la Lwangilo na kushushwa Mkonze akajitafutie mwenyewe matibabu.na kijana anajitafutia matibabu mwenyewe.
...ila hebu fafanua hapo kwenye red.
Poleni sana!MUNGU yu mwema kwa kweli!!
Umewahi kuwaza ni kwa nini unajiita "Msomi uchwara"?unatudanganya broo
Duh, kwa hiyo hata akipoteza maisha haitajulikana amepatia wapi tatizo.Wakati yule mama alipata msaada wa kupelekwa Hospitali kwa gari la TANAPA, Kijana alipanda gari la Lwangilo na kushushwa Mkonze akajitafutie mwenyewe matibabu.
Kumzaba vibao kwa kupuuzia maonyo yenu na kuhatarisha maisha yenuTulimuonya. Hatua gani zaidi ya hiyo ndugu yangu.
Wengi wanatabia ya kuzira. Kumbe hawajui pia mwendo mdogo sehemu amabayo unatakiwa at least uende na 80kph ni kosa kama sikosei kosa namba 23 ya makosa ya barabarani.Zile kona za Nyang'oro ni hatari sana,ajali ni chache kwa kuwa hakuna magari mengi yanayopita njia ile lakini yangekuwa mengi naamini ajali zingekuwa nyingi sana,niliwahi kupanda Mbereselo kutoka Iringa kwenda Dodoma,dreva alikuwa analala na basi kwenye zile kona kama hana akili nzuri na abiria wote walikuwa kimyaaaaaa!!!nilinyanyuka na kumfuata na kumtwanga mkwala mzito,konda akajifanya kumtetea nikamkuda kabisa na kutaka kumtwanga akaomba msamaha,kuanzia hapo walitii sheria bila shuruti na dreva eti akazila na kutukomoa akawa anaendesha spidi ndogooo mpaka tunafika Dodoma
Sent using Jamii Forums mobile app
Soma mstari kwa mstari.kuna majeruhi wawili.Poleni sana mkuu. Hakuna habari nzuri na ya kufurahisha ajali inapotokea na hakuna majeruhi.
Mungu awape na awajalie afya na maisha marefu.
Jana Asubuhi na mapema nilipanda gari la Isamilo linalotokea Iringa kwenda Mwanza. Mvua ilikuwa inanyesha kubwa sana.
Tulipofika mlima Nyang'oro Dereva wa Gari alikuwa anakata zile kona za Nyang'oro kama vile ni wakati wa kiangazi na kama anapanda mlima wakati alikuwa anashuka. Kufika kona ya mwisho gari likamshinda likapaa juu na kuanguka.
Bahati nzuri hakuna aliyeumia sana isipokuwa mama na kijana mmoja ambapo yule mama alipelekwa Hospitali ya Dodoma kwa Gari la TANAPA na kijana anajitafutia matibabu mwenyewe.
Mungu yu mwema leo nipo hai kuandika habari hii.
View attachment 1344937
Muda mfupi baada ya Gari hilo kuanguka.
Kama kawaida yetu wabongo kutochukua hatua mpk tupatwe na janga.Mkuu ulishindwa nn kumpa onyo dereva mpk anaenda kuwabwaga?kuna siku natoka morogoro nimepanda new force nikawa nasikia mtu anaongea na cm kwa sauti huku anacheka nikamuuliza abiria mwenzangu nani huyu anapiga kelele hivi akasema dereva huyo aisee nilisimama kama upepo nikamfata pale nikamwambia naomba wakati umetupakia sisi abiria usithubutu tena kuongea na hiyo simu yako.Mbona alitii mpk tunafika dar hakuongea na cm tena.
Sent using Jamii Forums mobile app