Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,176
- 48,460
Jana Asubuhi na mapema nilipanda gari la Isamilo linalotokea Iringa kwenda Mwanza. Mvua ilikuwa inanyesha kubwa sana.
Tulipofika mlima Nyang'oro Dereva wa Gari alikuwa anakata zile kona za Nyang'oro kama vile ni wakati wa kiangazi na kama anapanda mlima wakati alikuwa anashuka. Kufika kona ya mwisho gari likamshinda likapaa juu na kuanguka.
Bahati nzuri hakuna aliyeumia sana isipokuwa mama na kijana mmoja ambapo yule mama alipelekwa Hospitali ya Dodoma kwa Gari la TANAPA na kijana anajitafutia matibabu mwenyewe.
Mungu yu mwema leo nipo hai kuandika habari hii.