Highest Paying Jobs in Tanzania

Highest Paying Jobs in Tanzania

Kuwa na mtaji wa milion 20 uje songea nunua shamba hekari 100, lima(vibarua) mahindi kwa kisasa, utavuna kila hekari gunia 25 mara hekari 100 una gunia 2500, gunia moja ni 50,000 ukiuza zote unapata milion 150, ukitoa mtaji unapat million 130, gawanya kwa 12 unapata million 11, je ni wangapi wanapata million 11 kwa mwezi kat ya hao uliowataja, kilimo kinalipa ila mh too risk investiment mvua zikikata imekula kwako.

Mkuu nakupa like kwa mawazo yako ila siku nyngine usifikirie kuegemea kweny upande wa faida tuu umeweka changamoto chache mno tena ya hali ya hewa umesahau hasara nyng sana zitokanazo na kilimo
 
kwa utafiti wangu nimegundua kuwa kazi zifuatazo zinalipa 1.C.E.O(Directors),2.doctors 3.lawyers(jaudges&advocates) 4.soldiers 5.engineers 6.politicians 7.managers 8.accountants .

mishahara imejaa makato
biashara ndo zimejaa mapato
 
Life is how you make it, hizi zingine zote ni porojo tu!
 
kwa utafiti wangu nimegundua kuwa kazi zifuatazo zinalipa 1.C.E.O(Directors),2.doctors 3.lawyers(jaudges&advocates) 4.soldiers 5.engineers 6.politicians 7.managers 8.accountants .

Kwa hiyo kazi zilizobaki zote watu wanajitolea?
 
Hakuna kazi isiyolipa, ni wewe tu unaifanyaje. Ndio maana kuna walimu baada ya shughuli zao wanapiga tuition 40,000/hr. We accountant umekaa unahesabu hela za wenzio na 1mil/month
 
Kuosha Maiti Mochwari Pale Muhimbili Inalipa Sana,mtu Mmoja Ni Elfu 50 Ukiosha Kumi Kwa Siku Mara Wiki Mara Mwezi Plus Mshahara.,,,,pigeni Hesabu Wakuu
 
Tofautisheni kazi yenye mwanya wa kuiba (kula rushwa) na kazi inayolipa kihalali:

Mfano, Mwanasiasa akiingia mikataba akala rushwa ya mikataba mibovu, Mhasibu akiandika mahesabu (fraud) ya uongo akapata rushwa, Mchungaji akifanya kinyume na kuombea watu kwa malipo akatajirika na hata PMU (Procurement) wakifanya manunuzi ya ki magumashi wakala cha juu.

Upande mwingine basi: Daktari, kumuona tu unalipa tsh 30,000 kihalali kabla hajaanza kukutibu. Daktari anaweza pia kufanya kazi muda wa ziada na akaendelea kuingiza pesa nyingi bila kujishirikisha na kula rushwa. Tangu nilipoanza kulipa 30,000 kumuona daktari sijawahi kulalamika nadhani pia mnafanya hivyo na mwakani watalipwa 50,000.

Engineers pia wanaweza kutwengeneza pesa za kihalali kama hizo bila kula rushwa na hata Lawyers isipokuwa wanapoamua kuingia katika rushwa kwa maana ya kujilimbikizia mapesa. Kwa ufupi madaktari wanaongoza, wanafuatiwa na Engineers na kwambali Lawyers. Wengine hao tunawaita support staff ambaye akiwapo au asiwepo kazi za msingi zinaendelea na ndiyo wanaongoza kwa kula rushwa na utajiri wa kupindukia. Mchungaji hata nature ya kazi yake kuwa na mali ni kinyume na wito wake.

Mwanasiasa naye ni mtetea haki za wananchi hana kipato cha kumtajirisha, Mhasibu na afisa manunuzi hawa wanahakikisha hesabu na manunuzi yanakwenda kama inavyotaka sheria lakini ukiona wanatajirika huo ni wizi na rushwa ambayo sikatai hata madaktari na Engineers wanaweza kufanya....na wakifanya hayo matokeo yake ni majanga (tuwaombee wasiingie katika rushwa madaktari na engineers lakini tuongeze kuwalipa kupunguza tamaa zao kifedha).
 
ufinyu wa mawazo ndio inaowasumbua vijana wengi hasa hasa walio vyuoni!!! .kwanza mtoa maada kachanganya taaluma na vyeo!! hii inaonuesha wazi kwamba hajui afanyalo.

kazi inayolipa ni ya kujiajiri mwenyewe.


.... Hasa ukipata SMG, au ukaingia Katavi au Moyovosi ukatoka na bidhaa za kupeleka China .......... hata hii bangi ukijiajiri VIZURI wakakujua INALIPA .... sorry nilisahau sembe via NIA na KIA. Ndio ajira bora za walalahoi wetu!
 
kwa utafiti wangu nimegundua kuwa kazi zifuatazo zinalipa

1.C.E.O(Directors),
2.doctors
3.lawyers(jaudges&advocates)
4.soldiers
5.engineers
6.politicians
7.managers
8.accountants .

9.Sales And Marketing!!
 
Umesahau, walimu, waandishi wa habari, wajasiliamali mbalimbali, na wale dada zetu za "ile kazi", zinalipa sana tuu!.

Pasco
 
Umesahau, walimu, waandishi wa habari, wajasiliamali mbalimbali, na wale dada zetu za "ile kazi", zinalipa sana tuu!.

Pasco
mkuu Pasco waandishi wahabari hamna kitu nyie labda zile bahashaa ndio zinawapa matumaini ya kuiona kesho,
walimu ni tabaka la wanyonge wazalendo hawana sauti japo kazi yao ni kubwa sana,
ujasiliamali na udalali unalipa kiaina japo haupo kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi hapa tanzania
 
Last edited by a moderator:
umesahau ubunge na uwaziri!!! mafweza nje nje... hizi kazi zingekuwa zinatangazwa tuombe na sisi, sio kama sasa mpaka ujuane na wakubwa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom