Hi, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hi,

Discussion in 'JF Doctor' started by Elias fides, Jan 4, 2012.

 1. E

  Elias fides New Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoto wangu alizaliwa akachelewa kulia, hadi sasa shingo haijakaza na bado hajaweza kukaa vizr! Ana miez 9. Hv kuna uwezekano wa kukua vzr kama watoto wengine? Naomba msaada
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,251
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu,lakini wakati unangoja majibu ni vema pia useme km ushawahi kumpeleka hosp na wataalam wanasemaje.Ili madokta wa jf nao wapate pa kuanzia,lakini uwe na imani atatengemaa mkuu.
   
 3. D

  Discoverer Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana, ni kweli hiyo siyo kawaida na ukuaji wake utakuwa sio wa kawaida pia na inaonesha amepata 'cerebral palsy', kama uko Dar, nakushauri umpeleke muhimbili ili aanze physiotherapy mapema.
  Na ninyi wazazi mnahitaji pia psychological counselling ya jinsi ya kumlea na kumtunza.
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Pole sana kaka Elias....hiyo condition inaitwa 'Cerebral Palsy'. Moja ya sababu zake ni kama uliposema wewe kuwa mtoto alizaliwa akachelewa kulia. Mtoto anapozaliwa anapaswa alie immediately, hii inamsaidia kupanua mapafu na kuweza kupumua, hivyo basi damu yenye oksijeni ya kutosha kuufikia ubongo wake mchanga mapema na kuweza kuanza kazi mapema.

  Mtoto hasipolia (mara nyingi inasababishwa na kuchoka kutokana na labor kuchukua muda mrefu kupita kawaida), anachelewa kupanua mapafu na kupata oksijeni ya kutosha kwenda kwenye ubongo sehemu ya Cerebrum, na hii husababisha permanent damage kwenye ubongo wake mchanga. Na hili husababisha matatizo katika ukuaji wake kiakili (mental) na kimwili (motor). Na ni bahati mbaya sana kuwa 'hakuna tiba tatizo hilo'.

  Ni dhahiri kuwa mwanao hataweza kukua kama watoto wengine wa umri wake, atakuwa analag behind maisha yake yote, na pengine kwenye severe cases (nadhani hii ya mwanao ni mojawapo) mtoto anaweza pata ulemavu wa viungo kukakamaa (Spastic quadriplegia kama itahusisha miguu na mikono yote, au Spastic hemiplegia kama itahusisha mikono tuu au miguu tuu au mguu na mkono).

  Hata hivyo, kuna mambo kadhaa unaweza fanya kumsaidia mtoto katika ukuaji wake. Kuna clinic maalum kwa ajili ya watoto wenye Cerebral Palsy Muhimbili idara ya watoto, hapo utapewa elimu ya jinsi ya kumtunza mtoto mwenye tatizo hilo, na utakuwa unampeleka mara kwa mara kutokana na ratiba utakayopewa kwa ajili ya ufuatiliaji. Pia hapo baadae kuna shule maalum kwa ajili ya watoto wenye tatizo hilo ambapo kuna walimu specialized wa kuwafundisha. Naifahamu moja iko Ifakara inaitwa 'Bethlehem Centre'.
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,143
  Likes Received: 870
  Trophy Points: 280
  Dah pole sana mkuu!
  Kama unaamini unaweza pia kumpeka kwenye maombi!
   
Loading...