Hi everyone, am a guest here

Hi everyone, am a guest here

Shudu96

Member
Joined
Dec 1, 2011
Posts
8
Reaction score
0
Jaman hodi nmeingia huku napenda sana stori za kizushi na nimeshaweka stori 1 kwenye udaku pale, jaman nitarajie nini
 
Kinywaji changu ni stori baridi za kizushi. Hapo ntaenjoy...
 
guest?!! sasa utaondoka lini mjukuu wangu.
 
Jaman hodi nmeingia huku napenda sana stori za kizushi na nimeshaweka stori 1 kwenye udaku pale, jaman nitarajie nini
Karibu; hapa JF moderators wanaweza kuwa wanayapitia maandishi yako mara kwa mara na kuyaweka sawa ili yasomeke kwa rika zote. Mfano, ulichoandika hapo juu kinaweza kuandikwa upya na kuonekana kama hivi:
Jamani hodi nimeingia huku. Napenda sana 'stori' za kizushi na nimeshaweka stori 1 kwenye udaku pale. Nitarajie nini?
SABABU:

  • Umeandika neno 'jaman' na halipo kwenye kamusi ya kiswahili, ukalirudia na uandishi hauruhusu hivyo.
  • Ilikuwa ni sentensi moja ambayo ilitakiwa kutenganishwa.
  • Stori si neno la kiswahili, kwa kuanzia unaliweka kwenye mabano kisha baadaye unaendelea na 'flow' yako.
  • Jitahidi andika neno zimazima, wengine humu ni over 60yrs, wanahitaji kukusoma na kukuelewa.

KARIBU SANA

😛oa
 
Karibu; hapa JF moderators wanaweza kuwa wanayapitia maandishi yako mara kwa mara na kuyaweka sawa ili yasomeke kwa rika zote. Mfano, ulichoandika hapo juu kinaweza kuandikwa upya na kuonekana kama hivi:

SABABU:

  • Umeandika neno 'jaman' na halipo kwenye kamusi ya kiswahili, ukalirudia na uandishi hauruhusu hivyo.
  • Ilikuwa ni sentensi moja ambayo ilitakiwa kutenganishwa.
  • Stori si neno la kiswahili, kwa kuanzia unaliweka kwenye mabano kisha baadaye unaendelea na 'flow' yako.
  • Jitahidi andika neno zimazima, wengine humu ni over 60yrs, wanahitaji kukusoma na kukuelewa.

KARIBU SANA

😛oa

Invisible una akili kama Nyerere.
BTW: Karibu mkuu shudu, ila jina lako lanipa shaka, nadhani ni mbadala wa pumba, ama?
 
Ndiyo, watu wengi wanasema wanaongea (pumba) sasa mimi naongea (mashudu)
 
Back
Top Bottom