Sometimes You Have to Give a ROGUE a Rope Long Enough, It will Hang Itself

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
…Haya ni Maneno ya Mzee…
.
“Juma Swalehe”
.
NA…
.
…Hii ilikuwa ni Tarehe 15/06 Siku ya Alhamisi Mida ya…
.
Saa 2 na DKK 5 Usiku!
.
Maeneo ya Barakuda, Mzimbu…
.
(Morogoro)!
.
…nilikuwa Nimeenda kula Mahindi ya Kuchoma kwa Jamaa angu Mmoja huwa napenda Kumwita…
.
“Mzee wa Standard Solution”
.
Huwa ana ki Eneo chake kidogo cha Kuchoma Mahindi Opposite na Tumaini Hostel pale…
.
Yaani… ukiwa unashuka Mazimbu Chuo upande wa Kulia wa Barabara huwa ana Goli lake pale…
.
Na Mimi…
.
Mara nyingi huwa Napenda kwenda Kumuungisha kama Kijana mwenzangu Aliyethubuti Kujiajiri…
.
Kwasababu pia… Jamaa alikuwa ni Mwanafunzi aliyemaliza Chuo hapa hapa SUA
.
Kwahiyo… huwa Napenda pia kwenda Kupiga nae Stori huku akinipa Uhalisia wa Mtaa jinsi Ulivyo…
.
(By the way… A man he is Paying bills and making a Living)!
.
Basi Bhana…
.
Hiyo siku nikiwa Nimekaa zangu kwenye Benchi huku nikila zangu Kipande cha Muhindi cha 300/= huku Tukiendelea kutia Chumvi kwenye Moja na Mbili…
.
Mara Gafla…
.
Akatokea mzee Mmoja akawa anaongea Kingereza na Jamaa angu…
.
Mzee… Alikuwa anauliza Kama kutakuwa na Muhindi mzuri wa Moto ulioko tayari kwa Kula Sasahivi…
.
Jamaa akampa… Kisha Mzee akaendelea kutia Stori pale huku akitafuna zake taratibu!
.
For Sure… Huwa nikiona Mtu anaongea Kingereza huwa natamani Sana na Mimi niwe Sehemu ya Mazungumzo hayo…
.
Kwasababu… najua kama Ukiweza ku Master lugha ya Kingereza basi the World can Hear you…
.
Ndio maana hata nikiwa na Rafiki zangu huwa napenda Tuongee Kingereza muda wote…
.
(Just to Practice and Improve Myself)!
.
Kwahiyo…
.
Nikawa natafuta gia ya Kuanzisha Stori nae…
.
So ikabidi Nitumie MBINU Moja niliyojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Dale Carnegie Kinaitwa…
.
“How to Win Friends and Influence People”
.
Unajua Nilianzaje?..
.
Nilianza kwa Kumpa… “Compliment”
.
Kwanini?..
.
Kwasababu… Kiasili Binadamu wote tunapenda Kusifiwa na Kujiongelea Sisi pekee yetu…
.
Yaani kwa Ufupi… Binadamu wote ni wa Binafsi!
.
Ndio maana hata Ukipiga picha na Rafiki zako watano… Ukipewa kuiangalia hiyo Picha mtu wa Kwanza kumuangalia kwenye picha Itakuwa ni wewe…
.
(Utaiangalia Picha yako)!
.
Hata kama mtu hata kwambia kama Anapenda kusifiwa…
.
ILA…
.
Jua kwamba ndani kabisa ya Moyo wake ana hako ka Feeling… Hahahaaa
.
Kwahiyo…
.
Nikaanza kwa Kumwambia…
.
“You look like among the smartest elders around here…”
.
Akajibu…“Yeah!”
.
Kisha akarudisha tena Swali kwangu…
.
“Why you said that young boy?”
.
Tayari nikawa nishapata Attention yake kwa Kumpa kitu Kinaitwa…
.
“Compliment”
.
…baada ya Kuniuliza swali tena Hapo ndo Ikabidi nimmalize Kabisa…
.
Unajua Nilisemaje?..
.
Angalia Hapa Chini…
.
…wanasema Ukitaka mtu yoyote Akupende na Avutiwe na wewe basi…
.
Pale anapofanya Kitu flani Vizuri au Anapokuwa na Kitu flani Kizuri…
.
Basi mpe “SIFA” za dhati toka Moyoni na Muonyeshe kwamba una “THAMINI” kile alichofanya…
.
Kwanini?...
.
Kwasababu… Watu wengi Hawasifiwi, watu wengi ni wa Binafsi hawako tayari Kumsifia mtu hata kama kweli ana Uwezo
.
Kwahiyo… Ukitokea mahali na wewe Ukawa mtu pekee Unaye msifia basi Atakupenda na Kuvutiwa na Wewe…
.
NA… Hii ndio huwa Silaha yangu ya SIRI ninapokuwa Kitaani na Washikaji…
.
ILA…
.
Hakikisha kwamba Kitu unachomsifia nacho Mtu kiwe cha Kweli…
.
Kama kweli Kapendeza basi Sema kweli Kapendeza…Usimpambishe!
.
Ukijaribu Kumpambisha mtu Utapoteza… CREDIBILITY!
.
Na… Hata kuona kama Rafiki ILA kama ni Snitch tu!
.
Kwahiyo…
.
Wakati Mzee Juma Kaniuliza… “Why you said that young boy?”
.
Na… hapo Ndipo nilipoanza Kumpa mzee Juma sifa zake alizokuwa ana Stahili…
.
Kwasababu…
.
Jinsi alivyokuwa anaongea ile flow yake ya Maneno na Confidence nina Uhakika hata kuna Wanachuo kibao hawawezi Kuongea vile…
.
For Sure alifurahia Sana kwasababu… Nahisi watu wengi walikuwa awa Appreciate Jinsi alivyokuwa anaongea…
.
Na alinambia yeye…
.
Hajasoma sana wala Hafanyi kazi kwenye Taasisi yoyote ya Elimu bali…
.
Yeye ni Mfanyabiashara mdogo na anamiliki Duka lake maeneo ya pale Barakuda…
.
Ila… Kajifunza lugha ya Kigeni kwa ku Practice sana…
.
Yaani… kwa kuongea Bila kujali kama Anakosea au Laah na hadi Leo hii amefikia hatua ile!
.
Kwahiyo…
.
Wakati tunamalizia Kupiga stori na Mzee ili Niondoke zangu… Alinambia haya Maneno hapa Chini
.
“Sometimes You Have to Give a ROGUE a Rope Long Enough, It will Hang Itself”
.
Sikuelewa Alikuwa ana Maana gani…
.
Nikamuuliza… Una maana gani Mzee wangu?
.
(Hapo Tumerudi kwenye Kiswahili Sasa)!
.
Akanambia kwa Sauti ya Upole na ya Chini huku Kanishika bega langu la Kushoto…
.
“Seif… Ukitaka kumuuwa Mbwa Mkali na Mjeuri basi usimpige… Bali Mfunge na Kamba ndefu kisha Atajinyonga mwenyewe”
.
Bado nilikuwa kwenye Giza nene… Sikuelewa alikuwa ana Maana gani…
.
Nikamwambia tena… bado Sijakuelewa Mzee wangu…
.
Na hapo ndipo Mzee alipoanza Kunifungukia Sasa…
.
Akasema…
.
Kwenye Maisha kuna Muda inabidi uwape watu Nafasi ya Kuongea…
.
Wape watu Uwanja wa kusema wanachotaka Juu yako ILA Kumbuka mwisho wa Siku maneno yao Ndio yatawahukumu…
.
Usihangaike kujibizana wala Kupigana Vijembe na watu Status… Wewe wape nafasi waongee wanavyotaka Ila…
.
Siku ukishatusua Maneno yao ndio yatawanyonga kwa Walichokuwa wanakisema…Kama ilivyo kwa Mbwa Jeuri na Mkali…
.
Ngoja Nikuulize Hiki Kitu Leo…
.
Ni watu wangapi Walisema… Samatta hawezi Kufika mbali?..
.
Ni watu wangapi Walisema… Diamond Platnumz hawezi Kufikisha Mziki wa Bongo mbele?..
.
Kina nani Walisema… Kocha Nabi wa yanga Sio Mzuri?..
.
Watu wangapi Walisema… Pep hawezi kubeba UCL tofauti na timu ya Barcelona?..
.
Watu wangapi Walisema kwamba… Hutofika pale Ulipo leo?...
.
Ukweli ni Kwamba…
.
Watu wengi huwa Wanapenda kusema na ni kwasababu…
.
Kusema ni Rahisi kuliko Kufanya ndio maana Inabidi uwape Nafasi ya kusema wakati wewe Unaendelea kupambana ili Kufikia malengo yako…
.
Kwahiyo…
.
Katika Maisha yako yote Usitake kushinda Vita ya maneno… Bali shinda Vita ya Vitendo!
.
Na… Hiyo ndio maana ya…
.
“Sometimes You Have to Give a ROGUE a Rope Long Enough, It will Hang Itself”
.
Aliyokuwa ana Imaanisha Mzee Juma Swalehe…
.
Na…
.
Baada ya hapo Tukaagana na Mzee na Mimi nikarudi kwangu Ili Kukuandalia na Kukuletea Ujumbe huu unao Usoma hapa!
.
By the way…
.
Kama umependa Makala hii ya Leo... Usiache ku Like na ku Share ili pia watu wengine Wapate huu Ujumbe kutoka kwa Mzee Juma.
.
Vile Vile…
.
Kama umeipenda Makala hii ya Leo niandikie Kitu chochote kwenye Comment hapo chini…
.
(Nitasoma na Kujibu Comments Mimi Mwenyewe)!
.
I Hope Umejifunza Kitu!
.
Uwe na Jumatatu Njema.
.
Gracias...
.
Seif Mselem
 
Back
Top Bottom