Hewa yachafuka CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hewa yachafuka CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Sep 16, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Aliyempinga mtuhumiwa mauaji ya albino atupwa

  [​IMG]Asema si shabiki wa siasa za makundi, Mungu atamlinda

  KATIBU wa CCM Mkoa wa Kigoma aliyedaiwa kupigania chama hicho kutomteua mgombea ubunge anayehusishwa na kashfa za mauaji ya albino na ujambazi, Moudline Castico, amehamishiwa makao makuu ya CCM, mjini Dodoma, Raia Mwema limebaini.

  Taarifa za uhakika zinasema kuwa Castico alipewa barua ya uhamisho saa sita usiku, siku ambayo mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete alifika Kigoma kwa ajili ya kampeni.

  Katika moja ya matoleo ya gazeti hili, hasa baada ya kuhitimishwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, Dodoma uliopitisha wagombea ubunge na udiwani, liliripoti kupitishwa mgombea ubunge mwenye kashfa ya mauaji ya albino na ujambazi katika moja ya majimbo mkoani Kigoma.

  Katika habari hiyo, gazeti hili liliripoti habari za ndani kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma ndiye aliyeongoza hoja za kumpinga mgombea huyo, akirejea mazingira halisi ya jimbo anakogombea mgombea huyo (jina limehifadhiwa).

  Kwa mujibu wa habari hiyo ya ndani ya NEC-CCM, Katibu huyo alilazimika kutoa maelezo kwa nini mgombea husika asipitishwe.

  Anadaiwa kutoa maelezo hayo wakati wa mkutano wa NEC kwa kurejea kilichojiri kwenye mkutano wa Kamati ya Siasa ya Wilaya husika na Mkoa.

  Katika mkutano wa mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, anadaiwa kuwasilisha ripoti iliyochambua madhambi ya mgombea husika.

  Hata hivyo, katika mkutano huo wa NEC, Mjumbe mmoja kutoka Kigoma anatajwa kumtetea mgombea huyo ambaye pia anatajwa kuungwa mkono na wafanyabiashara wakubwa mkoani Kigoma ambao maadili yao yana utata. Pia mgombea huyo anaungwa mkono na mfanyabiashara na mwanasiasa mashuhuri kutoka mkoani Tabora ambaye ni mjumbe wa NEC.

  Ikiwa imepita miezi takriban miwili sasa, taarifa za hivi karibuni kutoka Kigoma zinabainisha kuwa kile kinachoelezwa kuwa ni ‘fitina’ za kundi la wafanyabiashara; hasa wenye utata wa kimaadili, limepambana kutumia ushawishi wa mtandao kumng’oa katibu huyo Kigoma.

  Baada ya kupewa barua ya uhamisho, katibu huyo anadaiwa kutengenezewa zengwe jingine kwamba alijaribu kubadilisha majina ya wagombea saba wa udiwani, Jimbo la Kigoma Mjini, akikwaruzana na mgombea ubunge, Peter Serukamba.

  Habari kutoka ndani ya CCM Kigoma zinadai kuwa katibu huyo aling’olewa kutokana na kujaribu kusaidia kuleta vurugu kwa kushawishi kamati za maadili na kamati za siasa kuwaengua na kuwapa alama za chini wagombea walioongoza kwenye kura za maoni.

  Anadaiwa kudhamiria kuwaengua wagombea saba wa udiwani Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuwaweka washindi wa pili na tatu katika kata za watu hao waliokusudiwa kuenguliwa.

  Hata hivyo, gazeti hili liliwasiliana na Katibu huyo ambaye alithibitisha kuhamishwa kutoka Kigoma hadi Dodoma lakini akipinga madai mengine dhidi yake.

  “Sio ajabu kuhamishwa, ni masuala ya kazi. Kuhusu kujaribu kupangua madiwani hilo ni suala la vikao sio la kwangu…sio suala la mtu binafsi. Wanaosema hivyo hawajui chama kinaongozwa vipi.

  “Wananisema kwa sababu wanajua mimi ni mwanasiasa na kiongozi bora, ninayesimamia kazi kikamilifu. Simwogopi mtu yeyote wala sifanyi siasa za makundi. Namwogopa Mungu tu.

  “Nimeonyesha uwezo wangu wa kazi Kigoma na kwingine na ndiyo maana nabadilishiwa kazi kutokana na utendaji mzuri. Na kwa sababu wananihusisha kwenye mambo yao kwa nia wanazozijua hiyo inazidi kunijenga kiuongozi maana yake kuna mambo ya msingi nayasimamia bila kujali siasa za makundi.

  “Ukiona wanakuandama au kukujadili kila wanapokutana ujue una thamani fulani ya kiuongozi ambayo labda wao hawana,” alijibu Katibu huyo wa zamani wa Kigoma katika mazungumzo yake na mwandishi wa gazeti hili.

  Lakini wakati majibu ya kigogo huyo yakiwa hayo, taarifa zaidi kutoka Kigoma zinaeleza kuwa kiongozi huyo alikuwa akimpigania mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo ambalo CCM imemteua anayetuhumiwa kwa mauaji ya maalbino na matukio ya ujambazi.

  Inadaiwa kuwa kiongozi huyo aliyehamishwa alikuwa akiungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia na Mkuu wa Wilaya Kigoma, John Mongela katika kuhakikisha mgombea ubunge mwenye kashfa za mauaji ya albino na ujambazi hagombei kwa tiketi ya CCM ili kunusuru ushindi wa chama hicho.

  Lakini wakati mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na kiongozi huyo aliyehamishwa wakitajwa wakati wa kura za maoni kuhakikisha mgombea huyo hachaguliwi, Mwenyekiti wa CCM-Kigoma, Azim Premji na Mjumbe wa NEC-CCM, Muhsin Abdallah Sheni walitajwa kumtetea kwenye vikao mbalimbali kwa wakati huo.

  Mgombea huyo anayetetewa na Premji pamoja na Muhsin Sheini huku akipingwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya, kwa kuzingatia taarifa za Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa, anadaiwa pia kuwafungulia mashitaka viongozi wa dini na kujikuta katika mgogoro mzito uliovuka mipaka kutoka kwa viongozi wa dini hadi kwa wapiga kura.

  Viongozi hao wamekuwa wakimtetea ndani ya NEC kwa hoja kuwa kama angekuwa anahusika na mauaji ya maalbino au matukio ya ujambazi, basi viongozi wa dola akiwamo Mkuu wa Mkoa, Simbakalia wangepaswa kumchukulia hatua lakini hawakufanya hivyo.

  Lakini wakati hayo yakiendelea, taarifa kutoka jimbo anakogombea mtuhumiwa huyo zinabainisha kuwa mgombea husika amewashitaki padre wa Kanisa Katoliki pamoja na mwalimu wa Shule ya Kiislamu (madrasa) kwa madai ya kumkashifu.

  Tukio hilo la kufunguliwa kwa kesi hiyo linatajwa kuibua mgogoro mkubwa kati ya mgombea huyo na viongozi wa dini, ikielezwa kuwa mgogoro huo sasa umevuka mipaka na wananchi wanaunga mkono viongozi wao wa dini.

  Katika hatua nyingine, habari zaidi za uhamisho wa Katibu wa CCM Kigoma, Castico zinabainisha kuwa alipewa barua ya uhamisho kwenda kuripoti makao makuu ya CCM Dodoma saa sita usiku, siku ya mkutano wa kampeni ya mgombea uraisi wa CCM, Jakaya Kikwete mkoani Kigoma.

  Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa kabla ya kikao cha NEC-CCM na hasa baada ya kupata taarifa ya mvutano uliokuwapo Kigoma, Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM-Taifa, aliwaita Dar es Salaam viongozi watatu waandamizi wa CCM Kigoma ambao wanaingia kwenye kikao cha NEC – Taifa ili kuzungumzia mwenendo wa zilizokuwa kura za maoni ndani ya chama chao Kigoma.

  Viongozi hao waliokutana na Kikwete kwa wakati huo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Azim Premji, Katibu wa Mkoa, Moudline Castico na Mjumbe wa NEC, Muhsini Abdallah Sheni.

  Raia Mwema iliwasiliana na Mwenyekiti wa CCM Kigoma, Azim Premji kuhusu uhamisho wa katibu huyo na masuala mengine anayohusishwa kuyafanya na hatima ya CCM katika Jimbo ambalo wanadaiwa kumteua mgombea ubunge mtuhumiwa wa mauji ya maalbino ambaye alipendekezwa katika kura za maoni zilizoendeshwa na serikali kubaini wauaji na wauzaji wa viungo vya albino.

  Katika majibu yake kuhusu uhamisho wa katibu huyo, Premji alisema huo ni uhamisho wa kawaida na kwamba yeye si mtu wa kwanza kuhamishwa kituo cha kazi.

  “Suala la kumhamisha kiongozi ni la kawaida, pengine imetokea anahitajika zaidi huko alikopelekwa lakini hakuna matatizo hapa. Kampeni zinakwenda vizuri.”

  Alipoulizwa kuhusu mgombea mtuhumiwa wa mauaji ya maalbino na ujambazi, ambaye pia ameingia katika mgogoro na viongozi wa dini kwamba mazingira haya yanaweza kukinyima ushindi CCM, alisema hilo ni suala lake binafsi (la mgombea) na si la chama.

  “Mgombea wa (anataja jimbo) kuwa na matatizo na viongozi wa dini ni lake binafsi, chama hakina mgogoro na tunaamini tutapa kura na viongozi (wa dini) kwa sababu ni watu wazima wanajua. Ni suala lake binafsi , haliwezi kuathiri kampeni,” alisema.

  Castico amewahi kutangazwa kuwa si raia alipokuwa kiongozi wa CCM Zanzibar kabla ya kurudishiwa kwa maelezo kwamba alifuata taratibu za kuhalalisha uraia wake. Uamuzi huo ulihusishwa na msimamo wake katika kutetea anachokiamini ndani na nje ya vikao vya CCM, jambo ambalo ni adimu kwa viongozi wengi wa chama hicho tawala.
  Source Raia Mwema

  [​IMG]
   
 2. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kimsingi, kama Castico amehamishiwa makao makuu ya CCM ya Dodoma akitokea Kigoma, hiyo ni PROMOTION, si DEMOTION. Itakuwa wameona umuhimu wake, wakapenda aende makao makuu ili akakitumikie chama vizuri.

  Nyie mnaonaje? Au ni mizengwe?
   
 3. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu inategemea Dodoma na Kigoma kwa CCM vina hadhi gani. Labda wenye chama wanajua hadhi ya kila mkoa wa Tanganyika na Zanzibar
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mizemngwe hiyo Waitara alikataa kutolewa Tanga kwenda Dar kumpikia chai mbwabwajaji Makamba
   
 5. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo Serukumba anauza viungo vya albino akishirikiana na Rostama?? Mbona sijaelewa vizuri hapa??
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Hawa CCM, watu wa ajabu sana, wametaka kumvua uraia Bashe kisa ni asili yake ya Msomali, wakati inajua wazi Modeline Castico ni Mmalawi na alizaliwa Malawi baba Mmalawi na mama Mmalawi aliyehamia Tanzania Mode akiwa mdogo. Urai wake huu ni kawa uraia wa Chee.. alizaliwa kule na baba na mama wa kule, wakavuka akaanza shule huku, tayari ni raia huku kwa mujibu wa ile sheria ya uraia wakati tunapata uhuru, wote waliokuwepo Tanzania kuanzia ile saa 6 usiku wa Desemba 9, 1961, ni Wanzanzania (Watanganyika).

  Huyu mama ni mgogoro kweli, alipokuwa naibu katibu CCM Zanzibar, moto wake waliuona, sasa kama ndio wanapeleka jikoni Dodoma, ama wanakwenda kumdhibiti na kummaliza kabisa, au kumpandisha akawakoroge vizuri.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huko Makao Makuu wanaenda kummaliza, maana hana kazi yoyote. Afadhali hata angekuwa amepelekwa Lumumba angepewa majukumu, lakini huko Dodoma ni kusubiri tu vikao vya chama. Mambo yote yako Lumumba. Hata ma-file nyeti huwa yanabebwa kutoka Lumumba kwenda Dodoma wakati wa vikao, na vikao vikiisha yanarudi tena Lumumba.

  Kimsingi ni kwamba hapo wameishammaliza, asubiri kupokea mshahara tu ... hapo hakuna posho wala gari la kutanua nalo.
   
 8. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamempeleka huko ili kumfunza 'busara' ya kisiasa. Akiwa kichwa ngumu, watamfifisha kabisa asisikike tena.:confused2:
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  lol ... waangalie tu kile alichowashauri na wakakikataa kisije kikawarudi. Waombe Mungu wasipoteze Jimbo la Muhambwe, maana huyo ambaye wanayempigia debe ana kasheshe nyingi na hata kama watatumia fedha bado wanaweza wasishinde.

  Ngoja tuone, nani atacheka mwisho, Castico au wao waliomhamisha Kigoma?
   
 10. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau, mgombea anayelalamikiwa kuuza viungo vya albino ni mgombea ubunge wa jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo kwa jina la Jamal TAMIMU, huyu alipigiwa kura za maoni za kuwasaka wanaohusika na uuzaji wa viungo vya albino na inasemekana kesi yake bado iko mikononi mwa polisi ndio maana mkuu wa mkoa wa Kigoma alipinga uteuzi wake. Pia ana tuhuma lukuki za ujambazi wa kutumia silaha
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Another reason to hate CCM
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280

  This is why I love sisiemu.
  Yaani jamaa pamoja na tuhuma zote hizi (kama ni za kweli) bado anataka kuwa mtunga sheria za nchi hii? Kwamba sisiemu wameishiwa wagombea kiasi hiki?
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu hizo tuhuma tu zinatosha kum-disqualify kugombea mpaka hapo atakaposafishwa!!!
  Yale yale ya Mramba, EL na kazaliak!!!:confused2:
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  mbona silaaa kuzini na mke wa mtu na jamaa mpaka kafika mahakamani bado anaendelea
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Kama bado anafikiri ccm ni baba na mama yake acha wakamtengue kiuno. Si ajifunze kwa Mwita wa Tarime? Walikuwa wanataka kumhamishia makao makuu Lumumba na aliwaambia kuwa Makamba hana hadhi ya kwenda kupikiwa chai na yeye. Hivyo akaachana nao kwa talaka tatu. Sasa ni mgombea ubunge huko Tarime kupitia Chadema na ana uhakika wa kuwagalagaza ccm.
   
 16. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Ni Jamal Tamim wa Muhambwe.
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Namkumbuka sana mama Castico kipindi kile cha utawala wa komandoo Salmini Amour, Zanzibar, huyu mama alikuwa matata sana aliwachachafya wajinga wajinga ndani ya CCM mpaka akaundiwa zengwe la uraia...kiuongozi huyu mama nampa haki yake ni hodari na anajiamini sana.
   
Loading...