HESLB yaanza kuwadai TZS 10.6 bilioni waliokopeshwa ‘Law School’

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,976
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Wanasheria 5,065 waliokopeshwa zaidi ya TZS 10.6 bilioni kama mikopo wakiwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Tanzania (Law School of Tanzania - LST) sasa watapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Wanasheria hawa ni wale walionufaika na mikopo ya elimu wakiwa wanafunzi wa LST kati ya mwaka 2008 na 2015 wakisoma Stashahada ya Juu ya Uanasheria kwa Vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) wakati Sheria ya HESLB ilipokua hairuhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa. Sheria ya HESLB ilirekebishwa mwaka 2014 na kuruhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa na HESLB.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa jijini Dar es salaam leo (Jumanne, Juni 21, 2022) na Watendaji Wakuu wa taasisi hizo, wanasheria hao ni wale waliosoma kupitia kundi (cohort) la kwanza hadi 19 na kukopeshwa na Serikali kupitia LST.

“Tunashukuru kuwa mikataba waliyosaini walipokua wanafunzi-wanasheria ipo wazi kuwa LST inaweza kuipa kazi ya kukusanya madeni haya taasisi yoyote ya umma au binafsi … na hivyo baada ya mazungumzo tangu 2019, leo tumefikia hatua hii,” amesema Jaji Dkt. Benhajj Masoud, Mkuu wa LST katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema HESLB ina uzoefu na utayari wa kutekeleza jukumu hilo na kuwakumbusha wanufaika hao kujitokeza na kurejesha.

“Tumejipanga kuanza kuwahudumia kuanzia Julai 1, 2022 … hivyo tunatoa wito kwa wateja wetu hawa kurejesha fedha hizi pamoja na zile walizokopeshwa wakiwa wanafunzi wa shahada za kwanza ili ziwanufaishe vijana wengine wa kitanzania wanaohitaji,” amesema Badru.

HESLB ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na majukumu makuu mawili, kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa elimu ya juu na pia kukusanya fedha za mikopo zilizoiva ambazo zimezotolewa na Serikali kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994/1995.

Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
Juni 21, 2022
IMG_20220621_191355_454.jpg

Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhajj Masoud na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Bardu wakiweka saini hati ya makubaliano yatakayoiwezesha HESLB kudai zaidi ya TZS 10.6 bilioni kutoka kwa wanufaika 5,065 waliokua wanafunzi wa taasisi hiyo kati yam waka 2008 na 2015. Hafla hiyo ilifanyika leo (Jumanne, Juni 21, 2022) Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Wanasheria wa Taasisi hizo, Abdallah Mtibora (kushoto) na Belinda Mollel.
IMG_20220621_191349_866.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzi ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhajj Masoud wakibadilishana hati ya makubaliano yatakayoiwezesha HESLB kudai zaidi ya TZS 10.6 bilioni kutoka kwa wanufaika 5,065 waliokua wanafunzi wa taasisi hiyo kati ya mwaka 2008 na 2015. Hafla hiyo ilifanyika leo (Jumanne, Juni 21, 2022) Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Wanasheria wa Taasisi hizo, Abdallah Mtibora (kushoto) na Belinda Mollel.
IMG_20220621_191346_492.jpg

Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhajj Masoud (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Bardu (kushoto) wakionesha hati ya makubaliano yatakayoiwezesha HESLB kudai zaidi ya TZS 10.6 bilioni kutoka kwa wanufaika 5,065 waliokua wanafunzi wa taasisi hiyo kati ya mwaka 2008 na 2015. Hafla hiyo ilifanyika leo (Jumanne Juni 21, 2022) Jijini Dar es Salaam.
IMG_20220621_191353_422.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzi ya Uanasheria kwa vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhaj Masooud (waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji waandamizi wa taasisi hizo mara baada ya kuwekeana saini ya hati ya kuhamishia HESLB mikopo ya wanafunzi 5,065 yenye thamani ya kiasi cha TZS 10.6 Bilioni ili kuanza kurejeshwa kutoka kwa wanufaika wa taasisi hiyo. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumanne Juni 21, 2022 Jijini Dar es Salaam.

(NA MPIGAPICHA WETU)
 
Bodi imeninyoosha nashukuru nimemaliza nao
Aiseh jamaa wamenikunyuga 8yrs
Mpaka nilishazoea
Wanasheria wajiandae kisaikolojia
 
sa
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Wanasheria 5,065 waliokopeshwa zaidi ya TZS 10.6 bilioni kama mikopo wakiwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Tanzania (Law School of Tanzania - LST) sasa watapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Wanasheria hawa ni wale walionufaika na mikopo ya elimu wakiwa wanafunzi wa LST kati ya mwaka 2008 na 2015 wakisoma Stashahada ya Juu ya Uanasheria kwa Vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) wakati Sheria ya HESLB ilipokua hairuhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa. Sheria ya HESLB ilirekebishwa mwaka 2014 na kuruhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa na HESLB.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa jijini Dar es salaam leo (Jumanne, Juni 21, 2022) na Watendaji Wakuu wa taasisi hizo, wanasheria hao ni wale waliosoma kupitia kundi (cohort) la kwanza hadi 19 na kukopeshwa na Serikali kupitia LST.

“Tunashukuru kuwa mikataba waliyosaini walipokua wanafunzi-wanasheria ipo wazi kuwa LST inaweza kuipa kazi ya kukusanya madeni haya taasisi yoyote ya umma au binafsi … na hivyo baada ya mazungumzo tangu 2019, leo tumefikia hatua hii,” amesema Jaji Dkt. Benhajj Masoud, Mkuu wa LST katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema HESLB ina uzoefu na utayari wa kutekeleza jukumu hilo na kuwakumbusha wanufaika hao kujitokeza na kurejesha.

“Tumejipanga kuanza kuwahudumia kuanzia Julai 1, 2022 … hivyo tunatoa wito kwa wateja wetu hawa kurejesha fedha hizi pamoja na zile walizokopeshwa wakiwa wanafunzi wa shahada za kwanza ili ziwanufaishe vijana wengine wa kitanzania wanaohitaji,” amesema Badru.

HESLB ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na majukumu makuu mawili, kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa elimu ya juu na pia kukusanya fedha za mikopo zilizoiva ambazo zimezotolewa na Serikali kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu tangu mwaka 1994/1995.

Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
Juni 21, 2022
View attachment 2268005
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhajj Masoud na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Bardu wakiweka saini hati ya makubaliano yatakayoiwezesha HESLB kudai zaidi ya TZS 10.6 bilioni kutoka kwa wanufaika 5,065 waliokua wanafunzi wa taasisi hiyo kati yam waka 2008 na 2015. Hafla hiyo ilifanyika leo (Jumanne, Juni 21, 2022) Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Wanasheria wa Taasisi hizo, Abdallah Mtibora (kushoto) na Belinda Mollel.
View attachment 2268007
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzi ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhajj Masoud wakibadilishana hati ya makubaliano yatakayoiwezesha HESLB kudai zaidi ya TZS 10.6 bilioni kutoka kwa wanufaika 5,065 waliokua wanafunzi wa taasisi hiyo kati ya mwaka 2008 na 2015. Hafla hiyo ilifanyika leo (Jumanne, Juni 21, 2022) Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Wanasheria wa Taasisi hizo, Abdallah Mtibora (kushoto) na Belinda Mollel.
View attachment 2268008
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhajj Masoud (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Bardu (kushoto) wakionesha hati ya makubaliano yatakayoiwezesha HESLB kudai zaidi ya TZS 10.6 bilioni kutoka kwa wanufaika 5,065 waliokua wanafunzi wa taasisi hiyo kati ya mwaka 2008 na 2015. Hafla hiyo ilifanyika leo (Jumanne Juni 21, 2022) Jijini Dar es Salaam.
View attachment 2268006
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzi ya Uanasheria kwa vitendo Tanzania (LST) Jaji Dkt. Benhaj Masooud (waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji waandamizi wa taasisi hizo mara baada ya kuwekeana saini ya hati ya kuhamishia HESLB mikopo ya wanafunzi 5,065 yenye thamani ya kiasi cha TZS 10.6 Bilioni ili kuanza kurejeshwa kutoka kwa wanufaika wa taasisi hiyo. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumanne Juni 21, 2022 Jijini Dar es Salaam.

(NA MPIGAPICHA WETU)
sawa kabisa walipe ili na wengine wapatekopeshwa kwa sababu wahitaji ni wengi.tena naona wamepewa muda mrefu wa kulipa na kwa vile yale maadhabu yalitolewa inawapa urahisi wanufaika kuerejesha.
 
Wanufaika wapya wa Mkopo zaidi ya elfu 20 HESLB 2022/2023 | Majina ya Waliopata Mkopo
Habari njema kwa waombaji wote wa mkopo wa HESLB, Allocation ya mkopo bechi ya kwanza sasa inapatikana mtandaoni kuangalia allocation ya mkopo Tembelea Tovuti ya HESLB ya Maombi ya Mikopo na Mfumo wa Usimamizi https://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/Olas

Nifanye nini nikikosa mkopo kwenye bechi ya kwanza HESLB?
Kuwa mvumilivu na subiri kwa sababu bodi ya mkopo inatoa majina ya waombaji wa mkopo waliopata mkopo kwa Bechi. Bechi za majina ya waliopata mkopo ni nyingi wakati mwingine hufikia tano au sita

Je nikisubiri hadi bechi zote za majina zikatoka na ikiwa sioni jina langu, nifanye nini?
Bodi ya mikopo hufungua dirisha kwa waombaji kukata rufaa kwa hivyo ikiwa unajiona kuwa una hoja, unaweza kukata rufaa
Je, nifanye nini ikiwa sipati mkopo baada ya kukata rufaa?
  • Lipa ada ya masomo na chakula cha kujifadhili na gharama za malazi.
Naweza kuomba mkopo huku nikiendelea na masomo?

  • Ndio mwaka ujao bodi itafungua dirisha jipya la maombi
Maswali baadhi ambayo naweza kukupa msaada angalau wa majibu kuendena na uelewa wangu
Je, iwapo nilikatisha(disco) masomo nifanye nini ili niweze kupata mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) Soma hapa

Je, ni lazima nifuate taratibu gani ili nilipwe mkopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB)?

Ili bodi ifanye malipo, mnufaika lazima afuate taratibu hizi

1. Mfadhiliwa lazima ajiandikishe kikamilifu katika taasisi ya elimu ya Juu, vinginevyo itamfanya akose sifa ya kupokea fedha hizo.

2. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) lazima ipokee maelezo ya ziada ya wanufaika. Jukumu la kutuma taarifa hizo ni la taasisi ambayo wamekubali Wanufaika na kuwasajili kikamilifu.

Nyongeza:

iwapo mnufaika wa mkopo atajiandikisha katika taasisi ya elimu ya juu ambayo ni tofauti na ile ambayo TCU ilipeleka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), mnufaika hatapokea fedha za mkopo hadi aombe kupangiwa upya au Kuhamishiwa mkopo.

Ikiwa mnufaika atabadilisha programu yake aliyoichagua awali, kiasi cha mkopo wake hakitabadilika hadi aombe kutengewa tena.

Mwisho, bodi ya mikopo Huendelea kufuatilia maendeleo ya mnufaika katika Vyuo vya Elimu ya Juu mara kwa mara ili kufanya uamuzi wa malipo.

Recomended Posts

Back
Top Bottom