HESLB: Batch One Out Now

Mkuu upo makini na una uelewa sana wa mambo mbalimbali huwa nafuatilia nyuzi na comments zako.

Huyo jamaa anapotosha makusudi eti waombaji jumla walikuwa zaidi ya 250k wakati sio kweli.

Pia anadanganya kwamba waliomaliza form six pekee mwaka huu na walioomba mkopo ni zaidi ya 200,000 wakati sio kweli.

Form six wa mwaka huu waliomaliza ni 100,000 hivi na kidogo. Matokeo ya form six yametangazwa hadharani pamoja na idadi ya watahiniwa iliwekwa wazi.
 
Accou ya dogo inasoma hivi.. karibia mwez na kitu sasa, kuna kitu kweli hapaView attachment 2798504View attachment 2798505
Kuwa na imani tu mkuu hadi hapo maombi yake yanafanyiwa kazi.

Anaweza asipate labda batch 3 lakini kabla ya mwezi wa 12 kuisha ukakuta amefanyiwa allocation maana serikali kupitia HESLB huwa wanaendelea kutafuta fedha ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mkopo kadri ya uwezo wa mfuko.
 
Watu tumeambiwa wait for final results roho ziko juu juu jmn mungu atusaidie sisi
Mkuu nina imani kuu kwamba utapata kabla ya Novemba 3 kama walivyosema.

Huwa serikali inaendelea kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mkopo ili watimize ndoto zao za masomo.

Ndo maana unaona leo utakuta mwanafunzi amepangiwa ada let say 250,000 out of 1,650,000 lakini baada ya muda akiwa masomoni anakuta ada imekuwa allocated kwa 100%.
 
Mkopo ni privilege siyo haki kuwa ni lazima kila mmoja apate wanapata wachache, unavyosema January and February watu wanapangiwa mkopo ni chuo kipi linafunguliwa hiyo miezi? TCU wenyewe mwisho wa kupokea list ya wanafunzi walio sajiliwa ni December mwanzoni.

Rai yangu ni kwamba watu wasijibweteke kusubiria mkopo, Kama mtu ana njia nyingine ya kwenda chuo atumie. Batch ya kwanza na ya pili zikipita hujapata mkopo unaasilimia 0.01 ya kupata mkopo. Tena kuappeal ndiyo usitegemee kabisa labda Kama una kigogo uko loan board.

Kuhusu kuongezewa asilimia za Tuition Fee ni kweli wengi wanao appeal wanaongezewa. Hii ni kutokana kuna pesa zinazo baki za wanafunzi walioshindwa ku report na continues walio Disco au kushindwa kuendelea na masomo.
 
Sawa ila fatilia kitu kabla haujaandika haujui jambo ni vizuri kukaa kimya

Wewe upo chuo? Au unafanya Kazi helsb ?


Chuoni watu huwa wanajiunga hadi mwezi wa kwanza unalijua Hilo?

Mwaka Jana umefatilia mkopo ulitolewa Hadi mwezi gani ?


Kuna Uzi upo unaonesha wanafunzi wa udsm ,udom wanaidai Ada zao refund je unajua kwanini wanadai Ada zao jibu ni kuwa walilipa Ada then bodi mwezi wa 1-2-3 waliwaongezea Ada na kuwapa wanafunzi wengine wapya mkopo .


Mwanafunzi anayeingia chuo kikuu anakuwa chin ya nacte na Tcu na anapofika mwaka wa mwisho na anakuwa chini ya Tcu ramsi na endapo mwanafunzi akaishia mwaka wa pili anaweza kupewa Diploma kutoka Nacte unanjua kuhusu hili?
 
Mkuu huyo jamaa Penologist anaongea vitu ambavyo havina uhakika wala source za kueleweka.

Imagine kama amekomaa kwamba idadi ya waliomaliza form six mwaka huu pekee ni zaidi ya 200,000 kitu ambacho ni uongo sasa tutamuamini kwenye lipi tena?

Kuna marafiki zangu wa Mzumbe mwaka jana walikuwa first year hawakupata batch zote lakini mwezi wa 12 aliingia kwenye akaunti yake akakuta amekuwa allocated ada 500,000 out of 1,600,000 kama sikosei na wakati huo alikuwa ameshalipa ada kwa mbinde sana.

Ndo hizo refund huwa wanadai kama ulivyosema.

Kitu asichokijua huyo jamaa ni kwamba serikali huwa inaendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili kuwapunguzia mzigo wanafunzi wa elimu ya juu.

Ndiyo maana kadri fedha inavyopatikana ndivyo wanavyoendelea kuwapangia ili mradi uli submit application zako na vigezo unavyo.
 
Mungu atusaidie maana haya mateso ugenini ni aibu
 
Hiyo apo ni Almanac ya TCU mwisho wa kuwasilisha enrollment ya wanafunzi wapya unaona ni tar ngap?.

Vyuo vikuu vyote vipo chini ya TCU hapa namaanisha full fledged Universities, na Vyuo vya kati vipo chini ya NACTE. Ikiwa na maana baadhi ya vyuo vya kati vilivyo ruhusiwa kitoa shahada ya kwanza NTA level 8 automatically vinafwata calendar ya TCU na kuwa under supervision of TCU kwenye programme za Bachelor degree na Postgraduate Diploma au Masters. The same kwa vyuo vikuu vilivyo pewa ruhusa ya kutoa Diploma na certificate yaani NTA level 6 kushuka chini, izo programme zinakuwa monitored na NACTE.

Kwaiyo basi kwa calendar ya TCU hakuna nwanafunzi wa mwaka wa kwanza atakaye sajiliwa baada ya December na kwa miaka ilikuwa hivyo pia.

Mambo ya kwamba nwanafunzi wa degree akifeli akiwa mwaka wa pili anapewa diploma hicho kitu akipo University bro ni story za kwenye vijiwe vya kahawa. Ukweli ni kwamba kwenye vyuo vya kati vilivyo ruhusiwa kutoa Bachelor degree wameigawanya kwenye category mbili NTA level 7 na NTA level 8. Hiyo NTA level 7 ndiyo ilikuwa High Diploma au Advance Diploma lakini ulikuwa unaisoma kwa miaka mitatu. Sasa kwa vyuo vya kati ipo ndani ya bachelor degree ndiyo maana wanafunzi wa hivyo vyuo wakiwa mwaka wa kwanza na wa pili wanatambulika kama High Diploma students then mwaka wa tatu wanakuwa Bachelor degree student. Ila haimaanishi waki Disco wanapewa Diploma. Kwanza Diploma ni level nyingine ya chini kidogo ya undergraduate NTA level 6 hii ina mitiani yake na mafunzo yake.

Wanafunzi wote wa shahada ya kwanza na kuendelea wanakua chini ya TCU hivyo ukidisco ata Kama ni mwaka wa tatu au wa nne kwa wanafunzi wa engineering na law au mwaka wa tano kwa wanafunzi wa MD NACTE hawawezi kuingilia kati kukupa Diploma.
 
Mzumbe University Ada 1.3 Million hakuna nwanafunzi anaye dai refund Mzumbe akiwa mwaka wa kwanza ada yake itakuwa compensated mwaka unao fwata, Otherwise kama amepata 100% atakuwa refunded akimaliza mwaka wa tatu. Hii inatokea mara nyingi kwakuwa Mzumbe wanataka nwanafunzi alipe minimum amount kabla ya registration na direct fee so kwa wanafunzi wenye asilimia 100% huwa wanakuwa na excess amount wakiingiziwa ada na loan board kwenye account za chuo.

Serikali haitafuti pesa nje ya budget iliyo panga hizo ni pesa zinazobaki baada uncertainty ya discontinued na wanafunzi wasio report vyuoni wanakuwa hawaja sign allocation zao ndiyo zinarudishwa kutengwa kwa walio appeal.
 
Hongereni kwa kazi wenzangu, ninaomba msaada namba ya simu ya Loan board ambayo hasa inapatikana Watsapp, kama haiko watsapp basi ninaomba yoyote ile
 
We jamaa unaulewa upo chini Sana hiyo ratiba usitegemee kuwa ndivyo ilivyo Mimi binafsi nilianza chuo mwezi wa 1


Yaani usichofahamu mambo ya helsb na Tcu hayapo Kama unavyokariri


Ungekuwa wewe ni Lectururer au helsb angalau ungekuwa na ulelewa yaani umekariri tu hauna u achofahamu .
 
Ja
Yes jamaa Anaonekana Hana ufahamu na mambo ya TCU Wala Helsb anababisha hajui kuwa mwaka Jana serikali iliongeza PESA kwa lengo lakuwapatia wanafunzi mikopo ya Elimu ya juu.


Watu wepata mikopo mpaka mwezi wa 1-2-3 na Mwanzo walikosa so jamaa Haelewi anaishi kwa kukariri wakati kila kunapokucha mambo hubadilika sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…