Heshima ya kipekee sana iwafikie Wanaume

Heshima ya kipekee sana iwafikie Wanaume

Hi guys..!
Naomba hizi baraka za dhati ziwafikie WANAUME, Hasa wale wanaume wanaosimamia na kutekeleza majukumu yao ipasavyo..!

Nakumbuka muda mfupi uliopita I passed through a very rough road to hell..! Kuna zile nyakati kwenye maisha unatamani kabisa kama ujikane nafsi, yote yanayokusibu yawe tu ni kama ndoto mbaya, unatamani uamke asubuhi uone like everything is real okaaaay, but that's next to never sababu hard times ndiyo zinaleta maana khalisi ya maisha.!!

Nakumbuka nililia na kulia mpaka machozi yakakauka, lakini chozi langu, halikubadili hata chembe ya ugumu wa mlima ule, na wakati nalia lile 'tatizo' liko palepale tena 'limekunja nne na kuchezesha mguu mmoja, linakuambia kabisa Carleen wewe lia tu, ukimaliza just come and face the reality'..!!

Nilikuwa kwenye nafasi nzuri kabisa ya kukubali kuwa nimeshindwa, jamii ingenielewa sababu ningejificha kwenye mwamvuli wa 'uanamke', wangesema tu 'she's just a lady, amepambana lakini imeshindikana', lakini sikutaka kuruhusu wala kukubali that comfort zone, I said to myself sintokubali kuwa defeated, the word 'FAILURE ain't on my dictionary'..!

Mwisho wa siku Mungu alinionekania, alinisimamia kiume, and I passed through that challenge, Akanifanikishia kibabe sana..!!

Wakati napitia that hard situation, nikawaza nafasi waliyonayo 'Wanaume', ambao hakuna namna jamii ama familia yake ingemuelewa kwamba kashindwa, yaani kashindwa? Kashindwaje? Tumejengewa kuamini they're like 'Undefeated Robots'..! Hakuna namna wataeleweka wasipotatua changamoto iliyopo mbele yao, na zaidi sana mwanaume utaishia kudharaulika na kuonekana mzembe, Man..! you're passing through hell of shi**s..!!

Na mbaya zaidi tunawabebesha mizigo mikubwa mikubwa ya matatizo bila kusahau 'misalaba mizito ya majukumu waibebe hadi Golgotha', na hatutegemei excuse yoyote kutoka kwao, kila tatizo walitatue haijalishi situation wako nayo ama ugumu uliopo, tunachojali tu ni solution imepatikana na maisha yanaenda.!! Huwa hatutaki kujua imekuwaje na wamewezaje, na mbaya zaidi tunaweza hata kuwaongezea tatizo lingine tena kwa juu walitatue, tunajua tu si 'Mwanaume bwana, atapambana tu'..!

MEN, May God Bless you abundantly, you're real true heroes..! Hizi baraka kutoka ndani ya moyo wangu, ziwafikie wababa bora wote wanaopigana na (watakaopigana) kwa ajili ya familia zao, you're doing a very remarkable great job.!!

Blesses..!!
Kwa risala lote hili lazima kuna bwege kaliwa tu mahali.

By the way blessings received with all hands[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada wa watu we danganywa tsunami ni janga!
Na kufikia mahali kuitwa hivyo jua hapana historia nzuri.. malaika wa bwana nimekutembelea kukuepusha na dhahma ya tsunami..
Njoo kwangu nikuonyeshe enzi ya mapenzi yako..
Nikupe kile ambacho kitakuwa furaha ya moyo wako then nikufunulie siri ya ulimwengu ambayo kwayo hukupata kuijui kabla..[emoji6]
Aisee unapeperusha njiwa wangu mkuu angalia hii mambo aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom