Heshima kwa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema

Majasho

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
413
220
Uchaguzi wa 1995 nilikuwa mdogo Primary School nakumbuka Mrema alishinda 1995, aliongoza mikoa 7 yenye nguvu Dar, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza, Tanga, Kagera na Tume ya uchaguzi ikafuta matokeo kwenye hiyo mikoa wakaamuru uchaguzi urudiwe tena November kwenye mikoa aliyoongoza Mrema na watu wakasusa Mkapa akapewa ushindi mezani. Mkapa alivyoapishwa kipaumbele chake ilikuwa kudili na Mrema, mikoa iliyompa kura na wafadhili wake.

Jukumu hili walipewa TRA, TISS, IGP Mahita na baadhi ya viongozi wa chama chake NCCR-Mageuzi hapa kuna Advocate Mabere Marando (Mjaluo wa Rorya), Advocate Lamwai, Advocate Hashim Rungwe, Mbatia aliyeachiwa jimbo na Mrema, Ali Sumaye, Chiku Abwao, Ndimara Tegambwage, Makongoro Nyerere, Dr Mvungi, Mwaiseje Polisya, Joseph Selasini, Anthony Komu n.k

Kundi la Mrema walikuwa Advocate Tundu Lissu, Godbless Lema, Thomas Ngowi Ngawaiya, Profesa Baregu, Rev Peter Msigwa, Michael Japhary, Jomba Koyi, Suzanne Lyimo, Advocate Moses Maira, Advocate Israel Magesa, Advocate Nyange, Prince Bagenda, Dr Peter Mlaki, Peter Mziray, Harold Jaffu, Abbas Mtemvu, Jese Makundi, Aloyce Kimaro, Kasim Mtopea, Michael Kisima, Cosmas Chenyenge, kasim Maguto, Makidara Mosi n.k.

Kundi la kina Marando walidai Mrema hajasoma hivyo hawezi kuwaongoza vurugu zikaanzia hapo na serikali kupitia msajili wa vyama vya siasa wakati huo Jaji George Liundi wakawawanabeba kina Marando ili kumpoteza Mrema mwishowe Mrema na kundi lake wakapigwa marufuku ofisi za NCCR pale Manzese Jengo la Ngawaiya na baadae Mrema na wenzie kina Lissu wakaamua kuhamia TLP kwa marehemu Dr Leo Lwekamwa so Ofisi zote za NCCR nchi nzima zikabadilishwa kuwa za TLP huko moshi Mbatia alipigwa marufuku kukanyaga hususani Marangu kwa kosa LA kumsaliti Baba wa Vunjo+Moshi vijijini mzee Mrema.

TLP nako hakukuwa salama TISS kupitia Bagenda na msajili mpya Bill John Tendwa walianzisha vurugu tena ,vurugu zikawa kubwa Bagenda na Lwekamwa wakatangaza kumtimua Mrema na wenzie ndio hapo kina Lissu, Lema, Msigwa, Baregu, Susan Lyimo, Michael Japhary wakavutwa na Mbowe na wakatimkia CHADEMA.

Wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wanamfadhili Mrema wakafilisiwa na wengine kupewa scandals mbalimhali kina Alex Massawe.

Wafanyabiashara wengine kama Tajiri wa kimarangu Mzee Koola (Mmiliki wa makampuni ya Zadock A1outdoor Africa) huyu alimpa support kubwa Mrema kuanzia 1995 mpaka 2005 unakumbuka vitenge na kanga za NCCR nchi nzima?

Kwa sasa huyu Zadock Koola alijiunga CCM na ni kada mkubwa wa CCM na Mmoja kati ya watoto wake amegombea huko Vunjo na ameongoza kura ya maoni kwa kumuangusha Dr. Kimei.

Hivyo kumuangusha Mrema zimetumika njia nyingi mno, kumuangusha na kumpoteza hivihivi haikuwa kazi rahisi. Kwa ujumla wanaomdharau Mrema siasa hawazijui.

Mrema atabaki kuheshimiwa kwa kutingisha siasa za Tanzania!
 
Lkn mbali na kumpamba Mrema, lkn naye Mrema alikuwa sehemu ya kuhujumu upinzani wa nchi hii na kauli zake zimekuwa zikionyesha atokako na aendako.
 
Asante sana Majasho kwa uchambuzi mzuri, umenikumbusha mbali. Upinzani mkubwa nchi hii umeanzia K'Njaro nadhani ndio sababu ya watu wa huko "kuogopwa" na hata "kuchukiwa". Mrema alikuwa mpinzani wa tatu katika historia ya upinzani mkali kutoka K'Njaro. Mpinzani wa kwanza kabisa alikuwa Mangi Mkuu kabla ya uhuru.

Serikali ya K'Njaro ilishafanya mazungumzo na kupatiwa uhuru wa mpito (semi autonomy) mwaka 1958 na Malkia wa Uingereza. Ilibidi Nyerere aruke pakubwa kutuliza mambo na hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ya Nyerere kutangaza marufuku ya uchifu mwaka 1961.

Mpinzani wa pili ni Edwini Mtei (Governor wa Benki Kuu) aliyepinga sana sera za kijamaa za Nyerere. Pamoja naye walikuwepo wengi tu kama akina Sosthenes Maliti waliokuwa wana-diplomasia mahiri Umoja wa Mataifa. Waliandika sana juu ya umaskini wakiuhusisha na ujamaa na waliishia kuondoka serikalini.

Mpinzani mkubwa wa tatu ni wakati wa Mkapa ambaye ndio Mrema kama ilivyoandikwa hapo juu. Kwa kweli alishinda urais lakini bao la mkono lilikuwepo tangu zamani na likafungwa mchana peupe.

Mpinzani wa nne ni Mbatia wakati NCCR Mageuzi ikiwa chama kikuu cha upinzani.

Mpinzani wa tano ni Mbowe hadi sasa akiwa kiongozi mkuu wa CHADEMA.

Wamekuwepo viongozi wengi tu wa vyama kutoka K'Njaro wakiwa waanzilishi. Serikali imefikia mahali pa kuwaaminisha watu kwamba upinzani ni mambo ya watu wa K'Njaro wasijihusishe nao. Magufuli anachukulia CHADEMA kama uchagga na hii huongeza hasira yake kwa upinzani hadi kufikia bila aibu kuweka lengo la kuangamiza upinzani ufikapo 2020. Atafanikiwa?
 
1599644934336.png
 
Asante sana Majasho kwa uchambuzi mzuri, umenikumbusha mbali. Upinzani mkubwa nchi hii umeanzia K'Njaro nadhani ndio sababu ya watu wa huko "kuogopwa" na hata "kuchukiwa". Mrema alikuwa mpinzani wa tatu katika historia ya upinzani mkali kutoka K'Njaro. Mpinzani wa kwanza kabisa alikuwa Mangi Mkuu kabla ya uhuru. Serikali ya K'Njaro ilishafanya mazungumzo na kupatiwa uhuru wa mpito (semi autonomy) mwaka 1958 na Malkia wa Uingereza. Ilibidi Nyerere aruke pakubwa kutuliza mambo na hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ya Nyerere kutangaza marufuku ya uchifu mwaka 1961.

Anaweza kudhoofisha sana Chadema, lakini hana na hato weza kuangamiza upinzani.
Mimi niko Hai hapa Uswaa, Chadema kama chama kimenyong'onyea sana lakini sio upinzani.

Mabomu yanayo pigwa na jeshi la kisiasa la kukodiwa lililopa hapa HAI kama Mbowe atapona safari hii basi na nchi atachukua.

Silaha zote za Kimachame na hata waliokuwa mawaziri miaka ya nyuma wameletwa hapa. Na lugha ya Kiswahili imepotea ni Kimachame tuu kwa kwenda mbele mpaka tuna shangaa matajiri wa kimachame wamepewa nini na Magufuli ?.

Inaendeshwa kampeni kali sana na kuna idadi kubwa ya wanHai tayari wameelekea Kibla.
Jana wame hakikishiwa na Mh. Majaliwa barabara zinazo sumbua zitajengwa upya.
 
Wachaga mko bias sana, unamfahamu kasanga tumbo? Unamfahamu Bilal waikela, unamfahamu fundi kila?unamfahamu musa Kwikima? Au mnajitekenya wenyewe mnacheka
 
Ila kiukweli Mrema angekuwa rais Ikulu ingeamia Kilimanjaro. ivi vyama vya ukanda inatakiwa vipigwe chini.
Mpumbavu wewe kama unafikiri CDM ni chama cha kikanda, tena kwa taarifa yako ukali wa CDM upo zaidi Kanda ya ziwa, kanda ya Kusini, Kanda ya Mashariki kuliko kanda ya Kaskazini.
 
Du kumbe ilikuwa ivi miaka hiyo ikawaje chadema imepata nguvu na mvuto kiasi hiki
Mrema alikuwa hatari mkuu mimi nilikuwa mdogo ila nakumbuka tulikuwa tunatoka sehemu tukakutana na msafara akiwa kwenye landrover nyomi kama lote wananchi hawataki gari liwashe wanalisukuma linapanda mlimani acha kabisa mkuu lilikuwa nyomi kubwa hatari.
 
Anaweza kudhoofisha sana Chadema, lakini hana na hato weza kuangamiza upinzani.
Mimi niko Hai hapa Uswaa, Chadema kama chama kimenyong'onyea sana lakini sio upinzani.

Mabomu yanayo pigwa na jeshi la kisiasa la kukodiwa lililopa hapa HAI kama Mbowe atapona safari hii basi na nchi atachukua.

Silaha zote za Kimachame na hata waliokuwa mawaziri miaka ya nyuma wameletwa hapa. Na lugha ya Kiswahili imepotea ni Kimachame tuu kwa kwenda mbele mpaka tuna shangaa matajiri wa kimachame wamepewa nini na Magufuli ?.

Inaendeshwa kampeni kali sana na kuna idadi kubwa ya wanHai tayari wameelekea Kibla.
Jana wame hakikishiwa na Mh. Majaliwa barabara zinazo sumbua zitajengwa upya.
Ni kitu gani hasa kimewabadili hao wanachame huko? Maisha yamekuwa mazuri au ni vitisho?
 
Asante sana Majasho kwa uchambuzi mzuri, umenikumbusha mbali. Upinzani mkubwa nchi hii umeanzia K'Njaro nadhani ndio sababu ya watu wa huko "kuogopwa" na hata "kuchukiwa". Mrema alikuwa mpinzani wa tatu katika historia ya upinzani mkali kutoka K'Njaro. Mpinzani wa kwanza kabisa alikuwa Mangi Mkuu kabla ya uhuru. Serikali ya K'Njaro ilishafanya mazungumzo na kupatiwa uhuru wa mpito (semi autonomy) mwaka 1958 na Malkia wa Uingereza. Ilibidi Nyerere aruke pakubwa kutuliza mambo na hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ya Nyerere kutangaza marufuku ya uchifu mwaka 1961.

Mpinzani wa pili ni Edwini Mtei (Governor wa Benki Kuu) aliyepinga sana sera za kijamaa za Nyerere. Pamoja naye walikuwepo wengi tu kama akina Sosthenes Maliti waliokuwa wana-diplomasia mahiri Umoja wa Mataifa. Waliandika sana juu ya umaskini wakiuhusisha na ujamaa na waliishia kuondoka serikalini.

Mpinzani mkubwa wa tatu ni wakati wa Mkapa ambaye ndio Mrema kama ilivyoandikwa hapo juu. Kwa kweli alishinda urais lakini bao la mkono lilikuwepo tangu zamani na likafungwa mchana peupe.

Mpinzani wa nne ni Mbatia wakati NCCR Mageuzi ikiwa chama kikuu cha upinzani.

Mpinzani wa tano ni Mbowe hadi sasa akiwa kiongozi mkuu wa CHADEMA.

Wamekuwepo viongozi wengi tu wa vyama kutoka K'Njaro wakiwa waanzilishi. Serikali imefikia mahali pa kuwaaminisha watu kwamba upinzani ni mambo ya watu wa K'Njaro wasijihusishe nao. Magufuli anachukulia CHADEMA kama uchagga na hii huongeza hasira yake kwa upinzani hadi kufikia bila aibu kuweka lengo la kuangamiza upinzani ufikapo 2020. Atafanikiwa?
Asante kwa uchambuzi makini. Mkuu we unavyoona amefanikiwa kuangamiza huo upinzania?
 
Nimesikia Advocate Hashim rungwe nimebaki kucheka tu hawa wazee mwishoni walipeleka akili wapi? Au ndio system iliamua kuwafanya vituko ivi
 
Uchaguzi mkuu wa 1995 ulitawaliwa na mbwembwe za kila aina kuliko ule wa 2015.

Mgombea urais wa NCCR Mageuzi Augustino Lyatonga Mrema alikuwa anabebwa juu juu na vijana kama mkungu wa ndizi na wengi waliamini angeibuka kidedea.

Kila alikopita Lyatonga Pwani hadi Bara shughuli zote zilisimama watu wakaenda kumsikiliza mzee wa " Siku 7".

Lakini siku ya uchaguzi aligaragazwa mapema kabisa na ndivyo itakavyokuwa kwa Tundu Antipas Lissu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Uchaguzi mkuu wa 1995 ulitawaliwa na mbwembwe za kila aina kuliko ule wa 2015.

Mgombea urais wa Nccr mageuzi Augustino Lyatonga Mrema alikuwa anabebwa juu juu na vijana kama mkungu wa ndizi na wengi waliamini angeibuka kidedea.

Kila alikopita Lyatonga Pwani hadi Bara shughuli zote zilisimama watu wakaenda kumsikiliza mzee wa " Siku 7"

Lakini siku ya uchaguzi aligaragazwa mapema kabisa na ndivyo itakavyokuwa kwa Tundu Antipas Lisu.

Maendeleo hayana vyama!
Tuache kuishi kwa hizo history za kichwara hapo sisi tupige kampeni ili ccm ipate ushindi mkubwa sio uropokaji wa akina Mrema maana dhama znabadilika mkuu tujtahd kuwanadi wagombea wetu ili tuchukue majimbo mengi pia
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom