Hersi Said amepotosha kuhusu mkataba wa Yanga na kampuni ya BlackBird AI

Hersi Said amepotosha kuhusu mkataba wa Yanga na kampuni ya BlackBird AI

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Nimetoka kuangalia clip ya Rais wa Yanga Hersi Said akisema wameingia mkataba na kampuni ya Artificial Intelligence inayoitwa Blackbird AI.

Kwa maelezo yake anasema mkataba huu ni kwa ajili ya kuiwezesha Yanga kupata analysis za wachezaji wakiwa mazoezini na katika mechi. Huu ni upotoshaji.

Kwanza, kwa misimu walau miwili na zaidi, Simba na Yanga zimekuwa na teknolojia hii ya kukusanya na kuchakata taarifa za wachezaji kwa njia ya kuvaa zile vesti ndani ya jezi. Kwa hiyo kusema hii ni teknolojia mpya kwa ukanda huu, siyo kweli.

Pili hii kampuni ya Blackbird AI imejikita katika kitu wanachoita "narrative intelligence" ama kwa tafsiri ya haraka ni "uchunguzi wa taarifa zinazosambaa katika jamii". Ukienda mbali zaidi, ni teknolojia yenye nia ya kuchunguza kinachosemwa mitandaoni ila wakati huo huo kusambaza upotoshaji na propaganda kwa manufaa ya wateja wao.

Ni kampuni ambayo inaingia mikataba na taasisi, makampuni na watu binafsi kwa ajili ya kucontrol taswira ya hao wanaoingia nao mikataba. Ni njia ya kutumia AI kucontrol jinsi taasisi au mtu binafsi anavyoongelewa mitandaoni.

Hii kampuni imejikita kwenye mambo yanayosambaa kama tetesi, conspiracy theories na taarifa mbaya zinazohusu watu au taasisi zenye uwezekano wa kuchafua brand yao, kufanya watu wasiziamini na kuharibu taswira chanya na soko la brand hiyo.

Kwa mtazamo wangu, hii kampuni imeletwa mahsusi kwa shughuli zingine kabisa. Haimake sense kwa Yanga kuingia mkataba na kampuni ya namna hii. Yanga inatumika kama kuipa taswira nzuri au kama chambo tu.

Sitashangaa kukuta hii kampuni haikuja Tanzania kwa ajili ya Yanga ila Yanga wamepewa hii fursa baada ya hiyo kampuni kuingia dili na taasisi zingine.

Inachekesha na kushangaza kwa Yanga kuingia mkataba wa kupambana dhidi ya "narrative attacks" wakati wasemaji wake ndiyo wamekuwa vinara wa kushambulia timu zingine na kujaribu kuharibu biashara zao, mfano wa hivi karibuni ni kwenye suala la jezi za Simba.
 
Back
Top Bottom