Henry Matata: Dr. Slaa mwongo no. 1 duniani

Henry Matata: Dr. Slaa mwongo no. 1 duniani

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,150
Ndugu wana JF, hayo si maneno yangu bali ni maneno ya Diwani mmoja jijini mwanza mwenye mgogoro na CHADEMA Bwn. HENRY MATATA.

Nianze kwa kusema kuwa leo asubuhi hii imekuwa ni mpya ya kufungia mwaka huu kwangu, baada ya jana kituo kimoja cha redio cha kidini (KWA NEEMA FM RADIO) hapa Mwanza kumuita diwani mmoja wa CHADEMA aliyefukuzwa uanachama (Kapera) na Matata ambaye ni meya mwenye mgogoro, wa manispaa ya Ilemela leo ilikuwa zamu ya Henry Matata kwenye kufanyiwa mahojiano kwenye kituo hicho.

Kusema ukweli kabisa sikuwahi kumsikia Henry Matata kwenye mahojiano, leo nimemsikiliza na kwa saikolojia ndogo tu si amini kama ni mzima timamu kutokana na jinsi alivyokuwa anaongea hoja zake.

Pia nipende kusema kwamba huyu ni mmoja kati ya watu ambao walitumia vizuri upepo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kugombea udiwani na kufanikisha kupitia CHADEMA, hafai hata chembe wala haihitaji muda kumsoma, kuongea kwake tu kuna kudhibitishia, na pia kwa kuwa kuna madai ya kuwa anatumiwa na CCM na hata mwenye alisema hivi majuzi kwenye kikao cha Mwigulu na hapa Nape, hapa mwanza kuwa yeye ni meya wa ccm, hivyo basi hata CCM wanazidi kujipambanua kuwa hawana nia ya dhati ya kuwa mfano wa uongozi bora na hawana nia njema na wananchi wa Ilemela, Kiufupi Matata hafai kuwa meya wala diwani, nitanukku machache ya aliyoyasema leo:-

Msikilizaji mmoja amepiga simu aksema "Naomba kumuuliza huyo bwana matata swali" kabla hajaendelea kuongea mtangazaji akasema "usimwite bwana matata mwite mstahik meya Matata" msikilizaji akasema "nyie ndo mnamwita hivyo mimi namwita bwana matata", ndipo matata akasema kama hawezi kuniita meya kata simu yake, akasema siwezi kumsikiliza, basi huyo msikilizaji kweli akakata simu kweli.

Msikilizaji mwingine akauliza, mbona Dr. Slaa juzi kwenye TV, alisema kuwa uliulizwa kama kweli ulipokea pesa kutoka CCM zaidi ya mara 4 na ulikubali, na hapa hata katika maelezo yake matata mwanzoni mwa kipindi alikubali, kwa hoja kwamba alizichukua kama ambavyo CHADEMA wanapewa na Sabodo, jibu la Mtata likawa, Slaa ni mwongo number 1 duniani we endelea kumwamini Slaa, hata wakati wa uchaguzi 2010 alisema atashusha bei ya cement hadi sh. 5000, kwanza hata slaa mwenyewe hakujui we unamtetea tu wakati hata kule karatu kwao hawamtaki kwanza ameiba pesa zao kutoka kwa wafadhiri ujerumani.

Mtangazaji akamwambia naomba siku moja niwakutanishe hapa na Kapera, akasema we mlete tu hata ngumi zitapigwa humu ndani, we diwani gani eti anataka umeya wakati kaishia la tatu atafanya nini mimi nimesoma bwana, kwanza anaishi kwa wakwe zake na mke wake Sofia.

Hayo ni machache tu, kwa machache hayo mimi nimeelewa kama mtu asiye timamu sijui wewe mwenzangu kama ndo meya huyo kweli ni wa kichina kama CHADEMA wanavyomwita huku, na pia CCM watatumia hiyo nafasi vilivyo kufanikisha mipango yao.
 
Huyu diwani si yule aliyepokea mil 20 kutoka kwa CCM na kukiri mbele ya kamati kuu ya CHADEMA?

Hafai,huwa anamshambulia sana Dr kwenye media.
 
Mwongo namba 1 duniani? loh

Yaani kwa maneno mepesi ni kuwa ukichukua waongo wote duniani mchumba wa josephine anaongoza kwa uongo.

hili neno kubwa sana! mtake radhi slaa.
 
Si nasikia ni mgombea binafsi? . Mwambieni tumemsikia . Atakula vichache kama chungu kibovu.
 
So interesting. Kwa matendo na maneno yake, tena mengine yanayotokana na kukirinkwake mbele ya vikao kuwa amechukua rushwa kutoka CCM, Matata hana uhalali wowote wa kumzungumzia hata Katibu wa Tawi wa CHADEMA anayesimamia misingi, imani, falsafa na itikadi za chama hasa kwa kutanguliza mbele Katiba, kanuni, maadili, miongozo, taratibu na itifaki za chama.

He will be nobody soon. Kumzungumzia Dkt. Slaa kwenye hoja yoyote ambayo ameianzisha mwanaCCM au mwanaCHADEMA anayefanya kazi za CCM kama tunavyowashuhudia wengi humu, tena hoja yenyewe ya kutunga kwa sababu tu wanamuona Dkt. Slaa kuwa tishio no. 1 pale magogoni, ni kumpatia credit za bure msemaji.
 
He will be nobody soon. Kumzungumzia Dkt. Slaa kwenye hoja yoyote ambayo ameianzisha mwanaCCM au mwanaCHADEMA anayefanya kazi za CCM kama tunavyowashuhudia wengi humu, tena hoja yenyewe ya kutunga kwa sababu tu wanamuona Dkt. Slaa kuwa tishio no. 1 pale magogoni, ni kumpatia credit za bure msemaji.

Mkuu tishio no. 1 wengine kwenye chama wanamuona muongo namba 1 tumuamini nani?
 
Chama changu kimeingia kirusi kibaya. Watu wanafanya kazi ya kubomoa chama badala ya kukijenga. Wengine wanathubutu kwa dhati kabisa kufanya kazi za CCM...
 
Mwongo namba 1 duniani? loh

Yaani kwa maneno mepesi ni kuwa ukichukua waongo wote duniani mchumba wa josephine anaongoza kwa uongo.

hili neno kubwa sana! mtake radhi slaa.

kazi hii ndo'mliojaaliwa "wabongo". Na huwa mnaifanya kwa ustadi wa hali ya juu... Mnatamani hata kungekua kuna shule na vyuo vinavyotoa elimu ya kazi hii.
 
kazdisha na yey. wanasiasa mara nying kama si zote wanakuwaga waongo lakin kumuita dr slaa muongo na 1 duniani ni uongo na 1 duniani.
 
Kwa wanao muunga mkono ndgu MATATA ,rejea Zaburi 15 : 2 " ULIMI WA MWENYE HEKIMA HUTAMKA MAARIFA VIZURI ,BALI VINYWA VYA WAPUMBAVU HUMWAGA UPUMBAVU ." Hapa ndo CCM imetufikisha. Sijui kama kauli mbiu yao mpya ya NGUVU YA MUNGU ina maana hapa kama si nguvu ya shetani. MUNGU hawezi kusimama nyuma ya ufedhuri huu.
 
Kweli Dr slaa mwiba sana anawachoma yaani uchafu wote anapewa yeye je yalikuwa wapi siku zote haya mpaka 2010 uchaguzi mkuu baada ya watu kukimbizwa hadi usalama wa taifa kuingilia ngoma kati.

Hivi mnajua kikwete alianguka chini matokeo ya vituo vya mwanzo yalipokua yanatangazwa pale osterbay kwa mafisadi tu Dr slaa aliongoza sasa itabidi tutake tume huru na ya haki kabla ya uchaguzi maana hakuna katiba mpya mpaka itachelewa kufika 2015.
 
imeandikwa hatimaye watakuja manabii wauongo .ndivyo hvyo kuna mamluki walotumwa kuharibu chadema kikubwa ni kuwa makini na hawa wanaotumwa huku cdm.eti mwigulu jembe,toka lini kafisadi kakawa jembe?
 
Hawa pamoja na wote wenye uchu na vyeo na ambao wanaharibu taswira ya CDM ni konokono tu ambao kamwe hawatafika popote maana wengiwao wanategemea ushirikina tu.
 
Aliyekuwa Diwani wa CHADEMA,anavituko kweli kweli!
 
Unajua , ukiona mgonjwa wako anaanza kuchanganyikiwa , hiyo ni dalili ya kifo kumkaribia , Matata alifukuzwa na kamati kuu ya CDM lakini yeye anaamini kafukuzwa na Slaa ! Sasa sijui alienda shule kusoma au alihudhuria tu masomo ? Namsikitikia mno , si siku nyingi ataadhirika vibaya sana , njaa ni Mbaya mno !
 
kama hawezi kuniita meya kata simu yake, akasema siwezi kumsikiliza, basi huyo msikilizaji kweli akakata simu kweli.


Slaa ni mwongo number 1 duniani we endelea kumwamini Slaa, hata wakati wa uchaguzi 2010 alisema atashusha bei ya cement hadi sh. 5000, kwanza hata slaa mwenyewe hakujui we unamtetea tu wakati hata kule karatu kwao hawamtaki kwanza ameiba pesa zao kutoka kwa wafadhiri ujerumani.

we mlete tu hata ngumi zitapigwa humu ndani, we diwani gani eti anataka umeya wakati kaishia la tatu atafanya nini mimi nimesoma bwana, kwanza anaishi kwa wakwe zake na mke wake Sofia.

Duh!
:A S-confused1:

 
Back
Top Bottom