Ndugu wana JF, hayo si maneno yangu bali ni maneno ya Diwani mmoja jijini mwanza mwenye mgogoro na CHADEMA Bwn. HENRY MATATA.
Nianze kwa kusema kuwa leo asubuhi hii imekuwa ni mpya ya kufungia mwaka huu kwangu, baada ya jana kituo kimoja cha redio cha kidini (KWA NEEMA FM RADIO) hapa Mwanza kumuita diwani mmoja wa CHADEMA aliyefukuzwa uanachama (Kapera) na Matata ambaye ni meya mwenye mgogoro, wa manispaa ya Ilemela leo ilikuwa zamu ya Henry Matata kwenye kufanyiwa mahojiano kwenye kituo hicho.
Kusema ukweli kabisa sikuwahi kumsikia Henry Matata kwenye mahojiano, leo nimemsikiliza na kwa saikolojia ndogo tu si amini kama ni mzima timamu kutokana na jinsi alivyokuwa anaongea hoja zake.
Pia nipende kusema kwamba huyu ni mmoja kati ya watu ambao walitumia vizuri upepo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kugombea udiwani na kufanikisha kupitia CHADEMA, hafai hata chembe wala haihitaji muda kumsoma, kuongea kwake tu kuna kudhibitishia, na pia kwa kuwa kuna madai ya kuwa anatumiwa na CCM na hata mwenye alisema hivi majuzi kwenye kikao cha Mwigulu na hapa Nape, hapa mwanza kuwa yeye ni meya wa ccm, hivyo basi hata CCM wanazidi kujipambanua kuwa hawana nia ya dhati ya kuwa mfano wa uongozi bora na hawana nia njema na wananchi wa Ilemela, Kiufupi Matata hafai kuwa meya wala diwani, nitanukku machache ya aliyoyasema leo:-
Msikilizaji mmoja amepiga simu aksema "Naomba kumuuliza huyo bwana matata swali" kabla hajaendelea kuongea mtangazaji akasema "usimwite bwana matata mwite mstahik meya Matata" msikilizaji akasema "nyie ndo mnamwita hivyo mimi namwita bwana matata", ndipo matata akasema kama hawezi kuniita meya kata simu yake, akasema siwezi kumsikiliza, basi huyo msikilizaji kweli akakata simu kweli.
Msikilizaji mwingine akauliza, mbona Dr. Slaa juzi kwenye TV, alisema kuwa uliulizwa kama kweli ulipokea pesa kutoka CCM zaidi ya mara 4 na ulikubali, na hapa hata katika maelezo yake matata mwanzoni mwa kipindi alikubali, kwa hoja kwamba alizichukua kama ambavyo CHADEMA wanapewa na Sabodo, jibu la Mtata likawa, Slaa ni mwongo number 1 duniani we endelea kumwamini Slaa, hata wakati wa uchaguzi 2010 alisema atashusha bei ya cement hadi sh. 5000, kwanza hata slaa mwenyewe hakujui we unamtetea tu wakati hata kule karatu kwao hawamtaki kwanza ameiba pesa zao kutoka kwa wafadhiri ujerumani.
Mtangazaji akamwambia naomba siku moja niwakutanishe hapa na Kapera, akasema we mlete tu hata ngumi zitapigwa humu ndani, we diwani gani eti anataka umeya wakati kaishia la tatu atafanya nini mimi nimesoma bwana, kwanza anaishi kwa wakwe zake na mke wake Sofia.
Hayo ni machache tu, kwa machache hayo mimi nimeelewa kama mtu asiye timamu sijui wewe mwenzangu kama ndo meya huyo kweli ni wa kichina kama CHADEMA wanavyomwita huku, na pia CCM watatumia hiyo nafasi vilivyo kufanikisha mipango yao.