Henry Matata: Dr. Slaa mwongo no. 1 duniani

Henry Matata: Dr. Slaa mwongo no. 1 duniani

Chama changu kimeingia kirusi kibaya. Watu wanafanya kazi ya kubomoa chama badala ya kukijenga. Wengine wanathubutu kwa dhati kabisa kufanya kazi za CCM...

Wataje funguka kijana
 
[Amejithihirisha kwamba hakufaa kuendelea kuwepo CHADEMA. Iko haja CDM ikawa makini zaidi ktk kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali Watu wa namna hii wanatuchafulia chama.QUOTE=DR. MWAKABANJE;5329547]Ndugu wana JF, hayo si maneno yangu bali ni maneno ya Diwani mmoja jijini mwanza mwenye mgogoro na CHADEMA Bwn. HENRY MATATA.

Nianze kwa kusema kuwa leo asubuhi hii imekuwa ni mpya ya kufungia mwaka huu kwangu, baada ya jana kituo kimoja cha redio cha kidini (KWA NEEMA FM RADIO) hapa Mwanza kumuita diwani mmoja wa CHADEMA aliyefukuzwa uanachama (Kapera) na Matata ambaye ni meya mwenye mgogoro, wa manispaa ya Ilemela leo ilikuwa zamu ya Henry Matata kwenye kufanyiwa mahojiano kwenye kituo hicho.

Kusema ukweli kabisa sikuwahi kumsikia Henry Matata kwenye mahojiano, leo nimemsikiliza na kwa saikolojia ndogo tu si amini kama ni mzima timamu kutokana na jinsi alivyokuwa anaongea hoja zake.

Pia nipende kusema kwamba huyu ni mmoja kati ya watu ambao walitumia vizuri upepo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kugombea udiwani na kufanikisha kupitia CHADEMA, hafai hata chembe wala haihitaji muda kumsoma, kuongea kwake tu kuna kudhibitishia, na pia kwa kuwa kuna madai ya kuwa anatumiwa na CCM na hata mwenye alisema hivi majuzi kwenye kikao cha Mwigulu na hapa Nape, hapa mwanza kuwa yeye ni meya wa ccm, hivyo basi hata CCM wanazidi kujipambanua kuwa hawana nia ya dhati ya kuwa mfano wa uongozi bora na hawana nia njema na wananchi wa Ilemela, Kiufupi Matata hafai kuwa meya wala diwani, nitanukku machache ya aliyoyasema leo:-

Msikilizaji mmoja amepiga simu aksema "Naomba kumuuliza huyo bwana matata swali" kabla hajaendelea kuongea mtangazaji akasema "usimwite bwana matata mwite mstahik meya Matata" msikilizaji akasema "nyie ndo mnamwita hivyo mimi namwita bwana matata", ndipo matata akasema kama hawezi kuniita meya kata simu yake, akasema siwezi kumsikiliza, basi huyo msikilizaji kweli akakata simu kweli.

Msikilizaji mwingine akauliza, mbona Dr. Slaa juzi kwenye TV, alisema kuwa uliulizwa kama kweli ulipokea pesa kutoka CCM zaidi ya mara 4 na ulikubali, na hapa hata katika maelezo yake matata mwanzoni mwa kipindi alikubali, kwa hoja kwamba alizichukua kama ambavyo CHADEMA wanapewa na Sabodo, jibu la Mtata likawa, Slaa ni mwongo number 1 duniani we endelea kumwamini Slaa, hata wakati wa uchaguzi 2010 alisema atashusha bei ya cement hadi sh. 5000, kwanza hata slaa mwenyewe hakujui we unamtetea tu wakati hata kule karatu kwao hawamtaki kwanza ameiba pesa zao kutoka kwa wafadhiri ujerumani.

Mtangazaji akamwambia naomba siku moja niwakutanishe hapa na Kapera, akasema we mlete tu hata ngumi zitapigwa humu ndani, we diwani gani eti anataka umeya wakati kaishia la tatu atafanya nini mimi nimesoma bwana, kwanza anaishi kwa wakwe zake na mke wake Sofia.

Hayo ni machache tu, kwa machache hayo mimi nimeelewa kama mtu asiye timamu sijui wewe mwenzangu kama ndo meya huyo kweli ni wa kichina kama CHADEMA wanavyomwita huku, na pia CCM watatumia hiyo nafasi vilivyo kufanikisha mipango yao.[/QUOTE]
 
yule mzee ni chizi we nenda hata kwenye lile behewa lake pale kirumba uone jinsi anavyoishi kama popo haijulikani wapi anajenga wapi anabomoa sasa anawezaje kuwa na akili ya kupigania mabadiliko na sasa eti hawa ndio watu ccm inawaandaa kugombea
 
Ben wewe ni nyoka mwenye vichwa viwili na mmoja wa watengeneza migogoro ndani ya chama.Iko siku yako utaaibika mbele ya wanachadema
Sasa mlitegemee aseme nini tofauti na hayo?Weekend njema
 
Last edited by a moderator:
Dr. Slaa ni mti wenye matunda acheni utupiwe mawe.
 
Nimemsikia Matata Kwa Neema FM ingawa ni dakika za mwishoni. Ni kituko kabisa.Nikiri kuwa sijawahi kumsikia kabla akiongea ila kwangu mie hata kama angkuwa hajafukuzwa Chadema hafai sio tuu kuwa Meya bali hata diwani.Huo udiwani wa Chadema najua aliupata kutokana na upepo wa Mageuzi wa 2010 na kutokana na uchanga wa chama wakati ule na woga wa watu ilibidi CDM iweke wagombea wakati mwingine bila kuchuja. Wakifanyacho CCM kutoa fedha za kurubuni sasa hivi ni msaada mkubwa kwa Chadema maana inachuja makapi kwa gharama inayolipiwa na CCM.
Uchaguzi uliopita kuna sehemu CDM ilikosa hata jiwe la kusimamisha,sasa chezea M4C! Uchaguzi ujao utakuwa moto maana hakuna anayeogopa kujitokeza kugombea upinzani tena. Matata na the like hata huko CCM hawakubaliki.maana toka lini ukaitumia toilet paper kujiswafi kisha ukaiweka mfukoni?
 
mwisho wake umekaribia na ole wao wana ilemela wakiendelea kufunga upuuzi wake kwa maana watalaaniwa.
 
Hizi akili ni aina ya zile za wakina Kisandu na Masalia wa PM7 na kiongozi wao Prezoo au Dogo
 
Dr. Slaa endelea kusimamia katiba na kanuni za chadema. Watu wa hovyo kama matata na wenzake waendelee kudhibitiwa
 
So interesting. Kwa matendo na maneno yake, tena mengine yanayotokana na kukirinkwake mbele ya vikao kuwa amechukua rushwa kutoka CCM, Matata hana uhalali wowote wa kumzungumzia hata Katibu wa Tawi wa CHADEMA anayesimamia misingi, imani, falsafa na itikadi za chama hasa kwa kutanguliza mbele Katiba, kanuni, maadili, miongozo, taratibu na itifaki za chama.

He will be nobody soon. Kumzungumzia Dkt. Slaa kwenye hoja yoyote ambayo ameianzisha mwanaCCM au mwanaCHADEMA anayefanya kazi za CCM kama tunavyowashuhudia wengi humu, tena hoja yenyewe ya kutunga kwa sababu tu wanamuona Dkt. Slaa kuwa tishio no. 1 pale magogoni, ni kumpatia credit za bure msemaji.

...mkuu tunaomba utujilishe kuhusu hii kesi ya umea wa Ilemela inaendeleaje...kukosekana kwa taarifa rasmi za chama kumesabisha kuwepo kwa upotoshaji wa makusudi kunako lenga kukidhoofisha chama..."naomba ufafanuzi wako tafadhali"...
 
Huuuu umbea ungekuwa umeelekezwa kwenye kilimo..mchele ungeuzwa sh 500 kilo
 
Back
Top Bottom