FC Bongo jana ilijikuta ikipata kipigo kitakatifu cha mabao 8-1 toka kwa timu machachari ya Kilimanjaro ya Sweden. Hii ni mara ya pili kwa FC Bongo kunywea mbele ya Kilimanjaro.
Fc Bongo ambayo ilikuwa inawania kutwaa kombe la Tanzania Cup toka kwa Kilimajaro, ilijikuta ikipokea kipigo kisicho na huruma toka kwa Kilimanjaro ambao walicheza mchezo huo huku wakiwa na uchovu wa safari ya usiku mzima baharini.
Jumamosi ijayo FC Bongo watakuwa na wakati mwingine mgumu, pale watakapo cheza na timu ngumu ya Waafrika waishio katika jiji la Tampere.