Tuinusuru Majimaji Fc na jinamizi la kufukuzwa, kuzuiliwa, au kukimbia madeni Hotelini

Maguguma

Member
Mar 13, 2023
13
6
44112800_2355620754453970_5765816255680348160_n.jpg
Machi 23, 2022 Timu ya Mpira wa Miguu ya Majimaji Fc toka Songea, ilizuiliwa Hotelini jijini Dar es salam mara baada ya kushindwa kulipa madeni yao. Timu ikashindwa kurejea nyumbani kwa wakati.

Februari 23, 2023 Wachezaji na Viongozi zaidi ya 12 wa Majimaji Fc walifukuzwa Hotelini (Dar es salam) kisa deni. ikijiandaa kucheza na Dar City, katika mwendelezo wa First League (Ligi Daraja la Pili).

Mei 2019 Klabu ya Maji Maji Fc ilijikuta ikiweka basi lake ‘bondi’ kufuatia deni la Milioni tatu na elfu tisini pesa waliyodaiwa na Hoteli ya JM iliyopo jijini Dar es salaam. Suala ambalo liliwatikisa sana Wanalizombe baada ya kuacha basi lao Hotelini.

Pia Miaka ya Nyuma Majimaji Fc iliwahi Kukimbia bila kulipa Deni la Hoteli, Ukanda wa Ziwa.

Hata katika baadhi ya nyumba za kulala wageni za Songea Mjini Majimaji Fc imerokodiwa kwenye vitabu vya wadaiwa wa muda mrefu, mara nyingi Majimaji Fc imekuwa ikisamehewa Madeni yake na wamiliki wa nyumba hizo au kulipiwa na wasamaria wema.

Matukio ya aibu ya kufukuzwa, kukimbia au kufungiwa Hotelini, Majimaji Fc imekutana nayo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 na hadi sasa timu imeshindwa kupata suluhisho la kudumu.

bb.jpg

Maji.JPG
Kuna kipindi Majimaji Fc ilimpata Mfadhili aliyedumu kwa muda mfupi (miaka ya 2010), ingawa wachezaji waliishi vizuri kwa kipindi hicho kuna kiasi fulani cha fedha kilipotelea mikononi mwa viongozi wachache wenye tamaa.

Hivi kweli Majimaji ni Timu ya Mkoa wa Ruvuma? au ni timu ya watu wachache? au ni timu ya watu fulani wa Songea Mjini tu! Kimsingi Majimaji Fc ni kioo cha Mkoa wa Ruvuma.

Ilipokuwa na Pesa chini ya DKT. Lawrence Gama Majimaji ilichukua Ubingwa wa Kombe la Muungano mara 3. Mwaka 1985, 1986 na 1998.

Kifupi Majimaji inahitaji viongozi wazuri wenye nia njema na Timu wenye akili ya kuipatia Majimaji Fc fedha kwa lengo la kuepukana na aibu ya kufukuzwa Hotelini mara kwa mara.
 
View attachment 2553769

Wanalizombe wapo hoi, pole kwao.
 
Back
Top Bottom