msindikizaji
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,763
- 2,891
haya kweli majanga............
Wakati mwingine naona wanawake wako kama watumwa vile... dume lifanyiwe kila kitu, kila kitu...
umpikie, umfulie, umpasie nguo, umuandalie ipi avae, soksi na boksa ziwe safi, utandike kitanda na bado kila iitwapo usiku ulale bila pichu...
mwisho wa mwezi mnagawana majukumu 50/50...
Its not fair kwa wanawake, lol.
Tehtehteh.... haya mleta mada jibu hili hapa
Mie naenda kwenye siasa huko kuna msiba wa mbunge
hao ndo mabinti wa dotcom nadhani hata wazazi wake wamemfundisha hivyohivyo
Anawaiga kina Beyoncee atashaaaaa
Nimependa sana, natamani siku moja wangu naye awe kama hivyo.Pole sana. Ni lini wanaume tutaacha kuwafanya wake zetu watumwa?? Ni furaha iliyoje kumwona mke wako anachoka sana tena wakati mwingine akiwa mjamzito? Wewe unafurahije kukaa juu ya sofa unaangalia Tv na kusoma magazeti ili hali mkeo anateseka na kazi. Halafu usiku au mchana huo huo unamataka kitandani akutimizie ndoa!!! Je na kuchoka huko unategemea ufanisi? Usipopata ufanisi unatafuta nyumba ndogo au kuja kurusha matatizo yako ya ndani JF!!! Wewe ndiyo chanzo. Kuna wakati miaka hiyo rafiki yangu alikuwa anamwachia mke wake kila kazi ili hali watoto walikuwa ni wadogo na waliofuatana sana. Mke alikuwa anachoka sana na ugomvi kila usiku maana mgongo unauma. Siku moja nikawakaribisha nyumbani makusudi kabisa. Nami nilikuwa na watoto almost same age kama yeye. Niliwaalika kuanzia lunch hadi dinner, it was our day. Nakumbuka walifika kama saa nne hivi maana walikuwa wanatokea mbali na usafiri walikuwa hawana (ngumu kupata magari enzi zile japo JABA ilikuwa kusaidia kidogo -tumetoka mbali sana). Alipofika tukawalaki na nikaanza kuwaandalia chai huku mwenzangu akiwa busy na kulisha watoto (tulikuwa tumetoka ibada). Walipomaliza kupata kifungua kinywa basi nikaondoa vyombo na kuweka meza vizuri (binti wa kazi alikuwa amekwenda ibada na tulikuwa tunasubiri dada yangu afike kutusaidia kupika kwa ajili ya ugeni ule). Rafiki yangu yule aninikodolea macho sana. Baadaye watoto wakawa wanacheza na wale wa kwake nikawaaga kuwa ngoja nimpe mama support kidogo. Nikaingia jikoni tukaanza kukata nyama na kuanza mapishi na dada yangu akawasili tukaendelea kusaidia kazi za mapishi. Tulikula na tulipomaliza nikajiunga nao wakati dada na binti wa kazi anaendelea na kazi za usafi baada ya kula.
Baadaye jioni wakati tunawasindikiza akaniambia kuwa atanipigia kesho yake kuna issue (hakukuwa na mobile alitumia ttcl ofisini). Ainipigia kunishangaa ila nikamwambia mke ni msaidizi na mwanaume maana yake ndiye mtendaji mkuu. Kuanzia siku ile alibadilika na mkewe alipata ahueni na mapenzi makubwa katika familia. Mke ni msaidizi wako na si mtumwa au mtwana. Hakuna cha limbwata bali ni upendo na wadogo zangu wote wa kiume niliwaonyesha njia and are happily married.
Nimependa sana, natamani siku moja wangu naye awe kama hivyo.
Sioni like. Ngoja nikupe samsing else.
According to African's culture,washng and ironing clothes of your husbnd,kitchen activities,cleaning of the house are the duties of a complete wife,other wise he decide himself to do dat., so please mama! If you real love him, Do dat for your benef,otherwise ua going to loose your hubby. Take care