Anne Mugisha,
Nimesoma makala yako ya Jumatano, 22 April 2009, kwenye THE OBSERVER, kuhusu wizi wa kura na ufisadi mwingine wa demokrasia wa watawala wa Uganda. Kazi njema sana.
Ningependa kujua, unawajibu vipi wapinzani wako, kama wapo, wanaokwambia kwamba wewe ni mwanaharaki asiye tofauti na jemedari wa kwenye kiti kirefu, aliyekimbia uwanja wa mapambano kwenda kuishi raha mustarehe maili 5000 kutoka nyumbani?
Sijui hali halisi ya Uganda kiusalama kwa "wakorofi" kama wewe, lakini kosoa kama hizo ulizotoa dhidi ya serikali, kama wizi wa kura, vitu kama hivyo huwezi kuvifanya ukiwa Uganda? Ahsante.
I read your article on THE OBSERVER voicing grim realities of vote rigging and other election iregularities underwritten by the incumbent power, also urging your collegues in the oposition to focus on voter empowerment. I think you're raising extremely important issues.
My question, however, is how you respond to detractors, as I'm sure you must have many, who would dismiss your activism as that of an arm chair general who fled her country only to lead a struggle from a comfort place 5000 miles away from home. I do not know the security realities for hell raisers like youself in Uganda, but couldn't you orchestrate such kind of critical activism while in Uganda? Couldn't you safely lambast the ruler's voter fraud while in Uganda?