Helen Kijo-Bisimba; Dalili ya kutokea mauaji ya kimbari nchini Tanzania!

Mama HELLEN KIJO BISIMBA ni hatari sana kwa taifa letu teule la tanzania.
ETI dini nyinigine imeendesha propaganda kuwa mfumo wa uongozi ni mfumo kristo? hapa unataka kuwalaumu waislamu? mimi mkristo MAMA lakini nikukumbushe, WAKRISTO nao tumekuwa na propaganda chafu kuwa Uongozi mzima serikalini ni WAISLAMU , mbona hilo hajalisema? MAMA anawaasa watanzania kutumiwa na Wanasiasa, yeye binafsi hata mtoto mdogo anajua kuwa anatumiwa na CHADEMA , ameacha kutumiwa hadi atuambie maneno haya? Nakumbuka hata SLAA wakati anaongelea sakata la LWAKATARE kamsifia sana huku akihoji eti HELLEN KIJO BISIMBA naye ni CHADEMA? watu tunakuwa na mitazamo tofauti, Huyu mama ni tatizo kubwa sana

Umekosa target, walisema viongozi wa awamu ya nne top leadership ni waislamu kwa maana walikuwa wanakanusha kilichoenezwa kwamba tanzania inaongozwa kwa mfumo kristo, usipindishe mada, tatizo unaaanza na jibu badala ya swali, kuna shida hapo
 
Huu si uchochezi hajwa biased she has shown impartiality in whole observations
Ni kweli kabisa Mkuu! Tena iko waziwazi bila kuuma manene! Na serkali ingesikia sauti hiyo, hayatotukuta! Ndipo nilipo ona kwamba sikio la kufa halisikii dawa!
 
Kama wanaotetea hayo mambo ya kidini ndiyo haohao wako huko serikalini sasa tutapeleka malalamiko wapi? Kwa mungu au?
 
Ni kweli kabisa Mkuu! Tena iko waziwazi bila kuuma manene! Na serkali ingesikia sauti hiyo, hayatotukuta! Ndipo nilipo ona kwamba sikio la kufa halisikii dawa!

Mi nadhani tamko la Maaskofu na hili la taasisi iliyochini ya Bi Hellen yamekuja muda muafaka, japo yamechelewa lakini kuna faida zake pia kuchelewa kwake, faida mojawapo ni kuwa tayari kuna kundi liliokuwa likinyanyasika la wakristo japo walipaza sauti zao mmoja mmoja lakini watawala wakaziba masikio.Lakini hii sauti ya leo ni sauti ya mungu maana ni muunganiko wa waumini na watanzania.JK sasa aanze kuelewa kuwa watu wakichoka huamua kusema na wakati wanasema tayari wanakuwa na uamuzi moyoni kwamba kama NOMA NA IWE NOMA.Wanasayansi wana usemi wao kuwa a SATURATED SOLUTION has attained its peak degree no more soluble.
 
Kama wanaotetea hayo mambo ya kidini ndiyo haohao wako huko serikalini sasa tutapeleka malalamiko wapi? Kwa mungu au?
Suala hapa sio kulalamika ndugu yangu manucho bali kuchukua hatua. Suala hili ni letu sote na kila mmoja kwa nafasi yake ana wajibu wa kurekebisha mambo. Kila mtu kwa nafasi yake, tukianza mimi na wewe tunaweza kuchangia katika ujenzi wa jamii yenye mshikamano na upendo wa kweli.
 
Last edited by a moderator:
mama Bisimba ametoa darasa la bure ambalo ilibidi washiriki walipie ada.Kwa darasa hili naamini kama tutaacha akili zetu zifanye kazi sawasawa tutaepuka matatizo aliyoyabainisha.Hivi kutoa tahadhari ni uchochezi?Nafikiri mtaalamu wa kiswahili atusaidie swala neno hili.Hongera mama Bisimba endelea kutoa somo wataelewa taratibu
 
Huyu mama anachelewa sana kutimiza wajibu wake. Kwa nini angojee mpaka matukio 19 ndipo aseme, alikuwa wapi? Tatizo la wasomi wa Tanzania ni ubingwa wa kutoa uchambuzi wa kinadharia lakini hawatoi suluhu ya matatizo wanayoyajadili. Pili ni uoga. Ukisoma kwa makini maada yake anajadili kimficho mficho. Hasemi ni dini gani inatoa vipeperushi, inachoma makanisa, inaua viongozi wa dini gani. Ni kiongozi gani waliingia kwenye uchaguzi kwa kete ya udini. Aeleze wazi. Wamakuha wana methali inasema ' panapouma, ndipo panapotoka mtoto'. Serikali ya Kikwete inapalilia ukadini. Unaposema serikali haichukui hatua za maana licha ya kuwepo dalili zaudini ni kama unazunguka. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hajawa makini kuhakikisha mbegu hii chafu ya udini hapandwi, hachipui, haipaliliwi na kustawi katika kipindi cha uongozi wake. Hii ni ishara kuwa wakati wa kuingia kwenye uongozi kuna ahadi aliahidi dini fulani kuwatendelea iwe mahali pa wazi au pa kificho na ndicho anachokitekeleza sasa. Abishe asibishe siwezi kushangaa kwa kuwa ndiyo hulka za wanasiasa nchi za dunia ya tatu.
Katika kipindi cha Raisi Mkapa hili halikuwepo, lakini hata kama lilikuwepo halikuwa na nguvu kiasi hiki kama linavyoonekana sasa hivi. Namshangaa sana Raisi Mstafu Benjamini Wiliam Mkapa. Kwa nini anashindwa kulikemea hili? Kustaafu sio kufa, anapaswa kuchangia mambo yanahusu nchi yake. Ndiyo maana tunamlipa pesa zetu nyingi hata baada ya kustaafu, kama hazina yetu ili atumie uzoefu wake wa kuwa Raisi kuhakikisha nchi haiyumbi. Haitoshi kusema tu nimemaliza kipindi changu cha uongozi wangu 'LIWALO NALIWE'. Hii ni dalili ya uoga na ubinafsi. Kwa nini Maisi wote watatu: Mwinyi, Mkapa na Kikwete wasiungane kupeana mikakati ya jinsi ya kuendesha nchi? Najua kila mmoja ana mabaya yake lakini pia kila mmoja ana mazuri yake. Mbona hayati mwalimu Nyerere aliweza kuchangia kwa jambo aliloliona kuwa ni muhimu hata baada ya kustaafu
Mkuu huyu mama huwa namkubali ana Msimamo mzuri na haogopi kusema na kukemea lile analiona ni baya kwa nchi na raia wake.
 
Kama kweli waraka huu ni wa
mama bisimba ambaye namheshimu sana. naungana nae moja kwa moja lakini
mifano aliyoitoa imeelemea kutetea haki wa dini yake. naweza
kujiridhisha kuwa yeye ni mwanaharakari wa haki za binadamu wa kikristo.

na kama mimi siko sahihi basi nionyeshwe lini katetea madhila
wanayofanyiwa waislam.

Mkuu anatetea watu wote bila kujali,dini,dhehebu au hata kabila nadhani tumwunge mkono.
 
Nampongeza sana Dk. Bisimba. Tuna mijitu humu ina ma PhD imekaa tu! Wala haitoi uchambuzi wowote. Je hizo PhD sijui mnawaonesha wake zenu tu au? BIG UP MAMA HELENI KIJO-BISIMBA. Wanaojadili pumba hawajui uzoefu ulio nao katika kutetea haki za binadamu.....na hawajasoma ile report ya "NYAMUMA"....
 
Safi sana huo ndio uchambuzi unaotakiwa kufanywa na Utawala ulio makini. Lakini kwa vile hawako TZ au waliopo ni waratibu wa mauaji ya kimbari basi tumekwisha. Kijo endelea kudocument na toa mawasilisho hayo hague ili wapuuzi wapelekwe mapema kabla ya kutumaliza. Mlipo wapelekea Hague yale ya mwanzo na Fatou Bensouda kutinga TZ wametengeneza video za kubumba kupayusha upepo! Tutakupa ushirikiano zaidi.

hivi ninyi mnaowindwa na udini toka mioyoni mwenu, mnashindwa hata kuona udini wa wazi ndani ya huu UTAFITI UCHWARA?????
Labda kama hamuishi TANZANIA na kama mnaishi TZ ni wazi mtakuwa mnafahamu kuwa WAISLAM ndio watu waliokuwa MOST DISORGANIZED CIVIL GROUP.. hivi mnavyoviona ni vikundi vya waganga njaa ambavyo havina mashiko kabisa miongoni mwa waTZ... KIJAMII,, HII NCHI BADO NI MOJA NA TUNASHIRIKI KAIKA KILA KITU PAMOJA NA HAKUNA TOFAUTI YOYOTE YA KIMSINGI BAINA YETU(wakristo na waislamu). hizi propaganda za mauaji ya halaiki yenye mrengo wa kidini ni eendelezo za zile hadithi za udini miongoni mwa waTZ hadithi ambazo ZIKO WELL ORGANISED AND WITH HIDDEN AGENDERS.
ANGUKO LA TAIFA HILI LIKO MIKONONI MWA WANASIASA NA VIONGOZI WA DINI huku anguko hilo likiratibiwa kwa ukaribu kabisa na wanahabari(wahariri,waandishi na wamiliki) na wanaharakati( kama alivyo mama kijo bisimba(mungu ampe laana)
 
Ukweli upo palepale, CCM inatumia karata za dini na ukabila kutugawanya watanzania. Hatari tunaichuma kwa mikono yetu
 
hivi ninyi mnaowindwa na udini toka mioyoni mwenu, mnashindwa hata kuona udini wa wazi ndani ya huu UTAFITI UCHWARA?????
Labda kama hamuishi TANZANIA na kama mnaishi TZ ni wazi mtakuwa mnafahamu kuwa WAISLAM ndio watu waliokuwa MOST DISORGANIZED CIVIL GROUP.. hivi mnavyoviona ni vikundi vya waganga njaa ambavyo havina mashiko kabisa miongoni mwa waTZ... KIJAMII,, HII NCHI BADO NI MOJA NA TUNASHIRIKI KAIKA KILA KITU PAMOJA NA HAKUNA TOFAUTI YOYOTE YA KIMSINGI BAINA YETU(wakristo na waislamu). hizi propaganda za mauaji ya halaiki yenye mrengo wa kidini ni eendelezo za zile hadithi za udini miongoni mwa waTZ hadithi ambazo ZIKO WELL ORGANISED AND WITH HIDDEN AGENDERS.
ANGUKO LA TAIFA HILI LIKO MIKONONI MWA WANASIASA NA VIONGOZI WA DINI huku anguko hilo likiratibiwa kwa ukaribu kabisa na wanahabari(wahariri,waandishi na wamiliki) na wanaharakati( kama alivyo mama kijo bisimba(mungu ampe laana)
Kuna shida gani? amegusa wapi? wewe ni mmoja wa waliondaliwa kuua siyo? UDINI wa hii habari uko wapi? Toa mbadala siyo unabwata kama batamaji!. Ametoa tu mifano katika hatua alizoonyesha!! Kwa vile umejiandaa kwa shughuli uliyotumwa ya mauaji hutaki kusikia! uko kwenye DENIAL stage aliyoitaja!!
 
rudi upya kwenye thread usome DENIAL stage inakuja wakati stage ngapi zikiwa zimeshapita!!!!
anyway,, sijafunzwa kutukana kaka. nawapa pole wazazi wako kwa kutolelewa vizuri huko kwao hadi wakashindwa kukulea wewe katika maadili ya kitanzani...
rejea vizuri utafiti wa KIJO BISIMBA... weka imani yako ya dini pembeni, jaribu kuwa muumini wa ukweli, then utuambie ndani ya matokeo ya huo utafiti wamelengwa akina nani??? naandika hapa nikiwa sio mtumwa wa imani(NA WALA MUNGU WANGU HATOKI MIDLE EAST kama mungu wenu ninyi. na labdanikuhakikishie tu kuwa naweza nikamchukia mtu kutokana na matendo yake(phisical) kijamii and i dont give a damn about ABRAHAM(IBRAHIM) LINKED RELIGION.. utumwa wa imani huwatawala watu walio na bongo ndogo mithili ya mataahira na ndio unaowatesa watz wengi. GET UPU AND WAKEUP FROM THAT DEEP AND ROTTEN COMMA
 
Wewe ndiye hukusoma vyema!! Those prejudices wo'nt let u think freely! mifano michache ambayo ni ya kweli imekufanya ukaiita ya UDINI. Mtu kama wewe hakuna wa kushawishi ujitoe kwenye hilo zimwi la UDINI lililokujaa!!
Hata vichaa huwa wanaona dunia nzima ni ya vichaa!!
Ni kichaa tu na au ambaye ameshibishwa uchafu kama ninavyokuona hapa atakayekataa mapendekezo haya:
Serikali:
i) Serikali ichukue hatua za haki na za dhati katika kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wale wote wanaohusika na harakati za kuondoa uvumilivu wa kidini katika nchi yetu
ii) Serikali ihusike katika kupiga marufuku vyombo vya habari, mikutano na matangazo yote yanayoeneza chuki, ikiwa ni pamoja na kuondoa vipeperushi, kanda na nyaraka zozote yanayochochea chuki na zinazohatarisha taifa kutumbukia katika mauaji ya kimbari
iii) Serikali isimamie sheria na katiba ya nchi kuhakikisha kuwa uhuru wa kuabudu pamoja na uhuru wa maoni hautumiwi vibaya na kuhatarisha usalama wa taifa na watu wake.
iv) Serikali ishughulikie kero za watanzania waliowengi ambao huweza kusadiki propaganda yoyote kutokana na wingi wa mahitaji yao ya kila siku kama elimu, afya, maji, chakula, ajira na malazi.

Taasisi za Dini:
i) Kila taasisi ya kidini iheshimu ibara ya 19 ya Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa kuabudu dini tunayoitaka na kuheshimu imani za wengine.
ii) Viongozi wa dini waweke mkazo na kuwahimiza waumini wao kuhusu umuhimu wa uvumilivu wa imani tofauti kama moja wapo ya nguzo kuu za amani ya taifa.
iii) Viongozi wakuu wa dini, wakaripie na kuwachukulia hatua wenzao wanaotoa kauli zinazoashiria chuki na uvunjifu wa amani

Wananchi:
i) Wananchi wa Tanzania tukatae kutumiwa na wanasiasa au viongozi wa dini wanaotuhamasisha kugombana baina yetu kwa misingi ya dini
ii) Wananchi tuendeleze amani ya taifa letu kwa kuheshimu imani ya kila mmoja ili kuliepusha taifa na mauaji ya kimbari au vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vitatuongezea zaidi shida kuliko kutatua matatizo tuliyonayo
iii) Wananchi tuchukue hatua ya kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama pale watu wanapotoa kauli na propaganda zinazochochea chuki miongoni mwa jamii

Kama kweli waraka huu ni wa mama bisimba ambaye namheshimu sana. naungana nae moja kwa moja lakini mifano aliyoitoa imeelemea kutetea haki wa dini yake. naweza kujiridhisha kuwa yeye ni mwanaharakari wa haki za binadamu wa kikristo.

na kama mimi siko sahihi basi nionyeshwe lini katetea madhila wanayofanyiwa waislam.

Labda unaweza kumsaidia kama una vielelezo vya dini nyingine yoyote Tanzania inayohamasisha chuki, mauaji, na hta majina ya ajabu ajabu kwa waumini na viongozi wa dini nyingine ziaidi ya waislam wasio na woga wala aibu kutangaza hadharani mauaji dhidi ya Wa-Kristo.

Yeye amesema radio kama imani, tetesi za chuo cha ukerewe na vipeperushi vingi vilivyo bayana vinavyotayarisha saikolojia ya mauaji ya Wa-Kristo. Kama wewe unaelewa taasisi, redio, ama chombo chochote kingine cha dini nyingine kinachotangaza mauaji ya waislam ama dini nyingine zaidi, unaweza kumpelekea tu. Utakuwa umetusaidia.

Wakati Wakristo wakiitwa makafiri na Ilung aakitangaza wauawe hadharani, serikali iko tu utadhani inashangilia, unaweze pia ukasema dini gani imewapa jina la fedheha waislam na nani ama dini gani imetangaza kuwaua.

Ni vizuri ukakaa kwenye neutral point iili uone u kweli na lakin pia inahitaji neema ya Mungu wa kweli ili kuukubali ukweli hata kama uko kinyume na utashi wako.
 
hapo mama amenena,wala sina la kuongeza.ila simuamini sana kwani sikumuelewa ktk sakata la madaktari kutokana na yeye kutozitambua haki za wananchi wasio na hatia (wagonjwa) kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha mgomo.

ili shwari :yaliyopita si ndwele....., safisha file. :A S 39::A S 39::A S 39:
 
Mama HELLEN KIJO BISIMBA ni hatari sana kwa taifa letu teule la tanzania.
ETI dini nyinigine imeendesha propaganda kuwa mfumo wa uongozi ni mfumo kristo? hapa unataka kuwalaumu waislamu? mimi mkristo MAMA lakini nikukumbushe, WAKRISTO nao tumekuwa na propaganda chafu kuwa Uongozi mzima serikalini ni WAISLAMU , mbona hilo hajalisema? MAMA anawaasa watanzania kutumiwa na Wanasiasa, yeye binafsi hata mtoto mdogo anajua kuwa anatumiwa na CHADEMA , ameacha kutumiwa hadi atuambie maneno haya? Nakumbuka hata SLAA wakati anaongelea sakata la LWAKATARE kamsifia sana huku akihoji eti HELLEN KIJO BISIMBA naye ni CHADEMA? watu tunakuwa na mitazamo tofauti, Huyu mama ni tatizo kubwa sana

.
Taarifa za kituo cha haki za binadamu ambapo Kijjo ni mkurugenzi zinapaswa ziwe zimeishapelekwa UN kwa maandishi kama kumbukumbu.
Maana watanzania tumeisha kuyaona yote yaliyoorodheshwa katika taarifa yao. Taifa linaandaliwa katika mauaji ya kimbare na watawala. Tulishuhudia mauaji yaliyofanywa na Mwigulu huko singida, Igunga, Arumeru nk. Na kwa kazi hiyo inayoonekana ni nzuri kwa wakubwa zake wamempandisha cheo. Achilia mbali mauaji yanayofanywa na vyombo vya usalama kama kwa Mwangosi na utekaji wa Ulimboka na wahusika wakitajwa kwa majina na wengine wakishuhudiwa na umati wakitekeleza mauaji bila kuchukuliwa hatua yeyote. Hii ndiyo fursa kwa wale wanaonufaika na utawala uliopo kuandaa mauaji kwa kuwa wameshajiridhia kwamba utawala wa sheria umewekwa kando na sasa kinachoonekana kwa dola ni abuse of the office.
.
 
It is good observation ikiwa na ujumbe kwa kila mtanzania, msishangae watakuja watu watatoa povu kuponda correct observation ya Mkurugenzi huyu makini. Subirini muone wehu wengi sana nchi hii.

Tayari wameshaanza kutoa povu na uvundo kupinga. Inasikitisha na kushangaza mtu anapopinga ukweli dhahiri.
 
Back
Top Bottom