sheikh yasin
Member
- Aug 6, 2015
- 61
- 45
Wadau nawasalimu,
Kuna mtoto nilizaa na binti mmoja wakati makazi yangu yakiwa Dar, kwa sasa ana miaka 7 na darasa la pili.Nilipoondoka Dar na kuamia mwanza kwa shughuli zangu binafsi niliamua kumpangishia huyu binti chumba na sebule waweze kuishi na mwanangu hapo, na natuma hela za mahitaji yote, ikiwemo kodi, kula, afya na ada ya mtoto, huyu mzazi mwenzangu hana shughuli yeyote kwenye maisha, namhudumia mimi kila kitu.
Sasa hivi karibuni ameleta jitu moja hapo nilipompangisha na linaishi nae humo humo na mtoto wangu, binti na hili jitu wanasubiri hizi hizi hela za matunzo ninazotuma ndio waishi, Je hii ni haki?
Ina maana huyu mwanaume anatembea na mama wa mtoto wangu humo humo huku mtoto akiwa amelala humo maana ni chumba na sebule tu, Je hii ni haki?
Hizi taarifa nilizisikia muda mrefu kupitia kwa mwenye nyumba ambae tuna mawasiliano ya karibu,sasa kuanzia January nikaacha kutuma pesa za matunzo, tukawa na mzozo, akanipeleka ustawi wa jamii, wakanipigia simu niende Dar, hivi juzi ndio nimekuja, ustawi wa jamii wakanieleza mambo ya ajabu sana na sifuati hata moja.
Masharti yangu ni haya, huyo mwanaume aondoke hapo, kama anaendelea kukaa hapo alipe hiyo kodi mwenyewe, au wanipe mtoto niondoke nae pia hawataki.
Nimeenda ustawi wa jamii kwenye hiyo kesi nashangaa kumkuta na yule jamaa pale kaja na mzazi mwenzangu, ikabidi niwaulize wale maafisa huyu anahusikaje hapa.
Nilitaka nimpe kipigo kizito huyo jamaa, bahati yake nikakuta ana li mwili la kuinua vyuma, halafu ni kama anavuta bang,e hivi kikao kiliisha bila muafaka.
Nimempa mwanamke masharti akiyafuata ndipo narudisha huduma
Au wadau nimekosea?