Heko wana uzi wote mnaojitolea mafunzo ya kilimo yamenipa tija

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
772
Wadau mwezi huu mwishoni Mungu akipenda navuna nyanya shambani kwangu Nimejaaliwa kulima heka 3 na zimebeba vizuri. Shamba lipo morogoro eneo la Dakawa. Ninachojivunai zaidi nimejifunzia humu humu Jamii forum kilimo hiki. Heko kwa wote ambao mmekuwa mskijitolea kutoa mafunzo mbali mbali.

1691745408001.png

Baada ya majaribio 2 ambayo hayakunipa faida nzuri sababu zsikuzingatia sana kanuni za kilimo hatimae mwaka huu nimesema lazima nifuate kanuni haijalishi ni gharama kiasi gani na Mungu amejibu. Nilianza na hekla moja na sasa nalima heka 3 nitabaki hapo mpk nibobeee kwanza.Msimu ujao nataka kulima ya miti nitaanza na heka moja mbili ntalima kawaida kama hii. Asanteni wote mnaoshare nasi tips bila kinyongo wala kuhitaji malipo. Mungu akawaongezee kila mlipopunguza.
 
Hongera na safi sana.Kilimo kina shubiri na maudhi ukivumilia kinaweza kukupa pesa nyingi ya pamoja na hakijawahi mpa hasara mtu mara 2 mfululizo.
 
Hizo heka tatu mpaka hivi sasa unaenda kuvuna unaweza ukatwambia umetumia gharama kiasi gani mkuu? Na vipi kuhusu matarajio baada ya kuvuna?
 
Kilimo kinataka uvumilivu na utimamu...nyie wadada mwanaume anaepata kipato chake kwenye kilimo huyo ni husband material.
Anajua;
  • kupanda mbegu
  • kulea
  • kuvumilia
-
-
mengine wadau wataongezea hapa
 
Wadau mwezi huu mwishoni Mungu akipenda navuna nyanya shambani kwangu Nimejaaliwa kulima heka 3 na zimebeba vizuri. Shamba lipo morogoro eneo la Dakawa. Ninachojivunai zaidi nimejifunzia humu humu Jamii forum kilimo hiki. Heko kwa wote ambao mmekuwa mskijitolea kutoa mafunzo mbali mbali.

View attachment 2714355
Baada ya majaribio 2 ambayo hayakunipa faida nzuri sababu zsikuzingatia sana kanuni za kilimo hatimae mwaka huu nimesema lazima nifuate kanuni haijalishi ni gharama kiasi gani na Mungu amejibu. Nilianza na hekla moja na sasa nalima heka 3 nitabaki hapo mpk nibobeee kwanza.Msimu ujao nataka kulima ya miti nitaanza na heka moja mbili ntalima kawaida kama hii. Asanteni wote mnaoshare nasi tips bila kinyongo wala kuhitaji malipo. Mungu akawaongezee kila mlipopunguza.
👏👏👏🙏
 
Back
Top Bottom