Hekima za Suleima zahitajika

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Ktk kuhangaika na maisha, nilijenga banda la kupangisha ili liniongezee kipato. Baada ya kumaliza tu akaja Baba mmoja mwenye heshima zake kuomba nimpe lile banda na atalipia mwaka mzima. Nikasema sawa. Nikakunja madafu yangu safi. Siku moja ilibidi nipite pale kuona mafundi kama wamemaliza kujenga ukuta kama week moja tangu tupeane kodi.

Nilipigwa butwaa vibaya. Kumbe yule mzee alimuoa binti mmoja ambaye nilishindwa kuoana naye kwa sababu ya imani,yule binti alipata mtoto kabla hajaolewa na huyu baba, na mtoto yule kwa umbile anafanana na mimi vibaya. Mzazi mwenzangu huyu wa zamani alicheka kwa furaha kuu, akasema usihofu kitu.

Maswali elfu kidogo yamenizonga, hivi kweli jamaa akishindwa kodi nitamtoa? Hii siri itatunzwa mpaka lini?
 
heeeeeeeeeeeeeeeee!...hapo kweli hekima za suleiman zinahitaji mkuu....pole na hongera
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom