Mke wa Lissu amepewa kazi ubelgiji, watoto wake wanasomeshwa Marekani. Mke wa Lema amepewa kazi Canada na watoto wake wanasoma Canada. Haya ni mafao ya ukimbizi kwamba nchini kwao sio salama.
Ili mafao haya "manono" yaendelee kuwepo angalau watoto wamalize masomo, Tanzania lazima kusiwe shwari angalau hata kwao tu. Hii maana yake Lissu, Lema na wenzao wanaopata mafao ya ukimbizi hawezi kufurahia malidhiano hata kidogo. Faida yao hii ya ukimbizi inapatikana kwa "kukinukisha vibaya sana" kunakoweza kuzalisha majeruhi na kamatakamata ambayo itatokea mbele ya camera za watu wao ili kuhalalisha status yao ya ukimbizi.
Heche na Mnyika mafao kama haya hawajapati, wanaotumiwa tu. Familia zao tunazo hapahapa kama sisi. Wanacheza music wasiyojua.
Tafadhali sana watu Hawa Heche na Mnyika msiwapige kirungu Wala kuwakamata, wametingwa tu na mkumbo.