Nawasalimu wote...
Kwanza nina declare interest kuwa Nampenda sana huyu kijana mwenyekiti wa Bavicha, namfahamu sana tangu namfundisha kidato cha kwanza hadi cha nne hapo Nyegezi Seminary. Lakini pia akiwa anafanya practical training zake pale mahakama ya mkoa Shinyanga alikuwa anapenda sana kunitembelea nyumbani kwangu na tulijadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo na mitazamo ya kimaisha. He is a brilliant, humble and determined boy.
Lakini BAVICHA ninayoifahamu ile ya Heche sio hii ninayoiona chini ya uongozi wake Patrobas. Tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu na kijana wangu kupewa heshima hiyo kubwa kabisa sijawahi kumsikia kwenye vyombo vya habari, mikutano ya kuamsha na kutia hamasa kwa vijana. Wanachama wengi wa Chadema ni vijana, na wakati huu ndipo tunaelekea kwenye kazi pevu na sioni dalili za kusikia falsafa za mwenyekiti wa BAVICHA mpaka sasa tangu apewe dhamana hii.
Tunataka kuona moto mkali kutoka huko juu, huku kwenye serikali za mitaa nadhani pameanza kueleweka na adui yetu ameshasoma alama za nyakati na anajiandaa kujihami kwa kutumia mbinu zake za kishetani. Kama mwenyekiti wa Bavicha utapita hapa au kusikia jambo hili juu ya ukimya wako, ni vema ukasema sababu za ukimya wake kpama una faida kwa vijana watanzania walio nyuma yake. Jitokeze tafadhari, tueleze kama bado unapikwa bado...