Tamko la BAVICHA: Yalalamikia BVR, mikopo na wanafunzi

Tamko la BAVICHA: Yalalamikia BVR, mikopo na wanafunzi

BAVICHA Taifa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
117
Reaction score
662
BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA)


TAMKO LA BAVICHA KUHUSU MAMBO MUHIMU YA KITAIFA YANAYOENDELEA

​
Ndugu waandishi wa habari, tumewaita hapa kuwajulisha mambo kadhaa ambayo sisi kama vijana wa CHADEMA haturidhiki nayo jinsi yanavyoendeshwa.

1.MBIO ZA MWENGE ZA TUME YA UCHAGUZI KATIKA UANDIKISHAJI.

Ndugu waandishi wa habari, tangu kuanza kwa zoezi hili la uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR, Tumeshuhudia mbio za mwenge katika zoezi hili, jambo linalopelekea wananchi wengi kukosa haki hii, au kuipata katika wakati mgumu sana. Tumeshuhudia Njombe, Songea, Mtwara Iringa na maeneo mengine watanzania wakiamka Alfajiri na hata kukesha kwenye vituo vya kujiandikisha, haya ni mateso makubwa kwa wananchi, tume lazima ikubali kuwa muda wa kuandikisha wa siku saba ni mfupi na hautoshi, na ni lazima NEC wakubali kuongeza muda na kuongeza idadi ya vifaa kwa ajili ya kulifanya zoezi hili kwa ufanisi.

Viongozi wetu wakuu wa Chama Mwenyekiti na Katibu Mkuu, wamefanya Ziara katika maeneo kadhaa, na wamejionea ulaghai wa hali ya juu unaofanywa na NEC, yaani NEC Wanatangaza kuwa watakuwa mkoa Fulani, lakini cha kushangaza wanakuwepo katika kata tatu mpaka tano, jambo linalowachanganya wananchi na kuwafanya wakeshe vituoni.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam, NEC inafanya vichekesho, kwamba imetenga siku 12 tu za kuandikisha watu wa mkoa wa Dar es Salaam. Kama mkoa wa Njombe NEC ilitumia mwezi mmoja na zaidi, na wapiga kura wa Njombe wako Laki tano na ushee, iweje Dar es Salaam yenye wapiga kura takribani milioni nne uwatengee siku 12? Hapa BAVICHA tumesema HAPANA, na kwa kweli, tutachukua hatua kuilazimisha NEC kuongeza muda kwa Dar es Salaam, NARUDIA TENA TUTAWALAZMISHA NEC


MIKOPO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU:


Ndugu waandishi wa habari, ni aibu kubwa kuona kuwa serikali ya nchi haijui matatizo ya wanafunzi katika nchi hii. Mtakumbuka kuwa, jana wakati Mwenyekiti wa CCM akifungua mkutano wa wanafunzi wa ccm wa Vyuo Vikuu, aliwaambia waandike pendekezo la kuijulisha serikali namna sahihi ya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Yaani, serikali hii ya Kikwete, haijui kuwa mikopo ya elimu ya juu ni tatizo? Haijui kuwa wanafunzi wananyanyasika katika kupata mikopo? Haijui namna sahihi ya utoaji wa mikopo bila unyasasaji?

Serikali hii, ni wazi imechoka, na ndio maana inatumia nguvu kubwa ya polisi kuwaumiza wanafunzi, wako walikamatwa na kufunguliwa mashitaka kama wale wa Vhuo Kikuu cha Iringa, tunaitaka Serikali kuwafutia mashitaka haya mara moja, na kuwaacha waendelee na masomo yao bila bugudha kwa sababu walikuwa na haki ya kudai mikopo yao ambayo ni haki yao na wajibu wa Serikali kuwapa kwa wakati.


VIJANA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA NA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Ndugu waandishi wa habari, mwaka jana wakati wa Uchaguzi wa ndani ya chama, Menyekiti wa CHAMA mhe. Freeman Mbowe aliutangaza mwaka 2015 kama mwaka wa Vijana na WAnawake, nasi BAVICHA tuanawaasa vijana wa kike na kiume kujiandikisha kwa wingi ili kuwa haki ya kuamua hatma ya nchi hii.

Tunawataka pia vijana kugombea UBUNGE na UDIWANI kwa wingi ili vijana tuweze kuwa sehemu ya maamuzi katika nchi hii.

Ndugu waandishi wa habari,Kamati kuu ya Chama katika kikao chake cha Kawaida cha kikatiba kilichokaa tarehe 22.01.2015 ilipokea mapendekezo mbalimbali kutoka retreat ya chama.Moja ya mapendekezo iliyopokea ni kuhakikisha Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) linakuwa na wabunge wa Viti maalum,kwaajili ya kusimamia,kutekeleza na kufanikisha shughuli mbalimbali za baraza pamoja na kufanya uenezi wa Baraza na chama kwakuwa wabunge wa Viti maalumu kikatiba wanakuwa nanafasi ya uenezi.

Ndugu waandishi wa habari,ikumbukwe kwamba ilizoeleka kuwa wabunge wa Viti maalumu hutokana na BAWACHA peke yake,na ndiomaana tunataka kuweka utaratibu mzuri kuwajulisha wanachama wetu wenye umri usiozidi miaka 30 kwasasa wachukue fomu wajaze,kuomba nafasi hizo.

Ndugu waandishi wa habari,Mnamo tarehe 6-7/02/2015 kikao cha kamati ya utendaji ya Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Taifa kilikutana mjini Dodoma kwa mujibu wa muongozo wa BAWACHA kifungu cha 7.8.5(h) ambacho kinaipa mamlaka ya "kujadili na kupendekeza taratibu za kupata Ubunge Viti maalum kwa vigezo,vilivyo wekwa na kukubalika''.

Nakwakuwa vigezo vya kuwapata wabunge ndani ya chama ni vya aina moja,na kwakuwa wabunge wote ni wa CHADEMA,Sekretareti ya BAVICHA Taifa ilikubaliana na vigezo hivyo na kuamua kuvitumia kama vigezo ndani ya Baraza la vijana ,lakini kwa nyongeza ya umri wa mgombea.Ndugu waandishi wa habari Mgombea wa viti maalumu wa BAVICHA hatotakiwa kuwa na umri unaozidi miaka 30 kwa sasa.

CHADEMA - VEMA! VIJANA - NGUVU YA MABADILIKO
Imetolewa na idara ya habari na unezi BAVICHA Taifa.
EDWARD SIMBEYE

​
 
Wasomi wa BAVICHA
BAVICHA ina wasomi
 
Tumechoshwa na siasa rahisi rahisi zinazofanywa na BAVICHA za kutafuta kick kwa kukurupuka na kutoa matamko.
 
Nimependa Sana hiyo ya Bavicha kuwa na uwakilishi bungeni. Good move!
 
wako sahh kwa ni viini macho tupu ktk zoezi hili muhimu la kitaifa hasa vijjn yaan n upumbavu unafanyika
 
Good move.BAVICHA ndio sauti ya vijana wazalendo kwa taifa hili
 
Back
Top Bottom