Usikurupuke bila kuwa na uhakika

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
MAONI YANGU JUU YA WARAKA KWA BAVICHA ULIOANDIKWA NA RAFIKI YANGU CHARLES FRANCIS.

Rafiki yangu Charles Francis ameandika waraka maalum wenye hoja tano kwa uwazi kwa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA).

Binafsi Daniel Ezekiel Daniel nimeusoma waraka huo kwa umakini, weledi na utashi uliojitosheleza. Nimeona nami nitoe maoni yangu juu ya waraka ule kama miongoni mwa Vijana wa BAVICHA na mwanachama wa CHADEMA.

Katika utangulizi wa waraka huo, Waraka umeeleza kwamba BAVICHA imejikita katika matukio na inacheza ngoma za CCM.

Binafsi nadeclere interest kwamba ni mwanasiasa kwa taaluma na ni mwanasiasa kwa kazi yaani political scientist and political actor. Hivyo kwa vipimo vyote vya sayansi ya siasa, Hoja hii ni mufilisi na dhaifu sana. Naomba kutoa maelezo kidogo.

Katika siasa kuna matukio, kuna mambo (issues) na mirengo. Kwa kuwa siasa ni maisha matukio katika siasa haikwepeki. Matukio katika siasa ni pamoja na shughuli za mikutano, maadhimisho ya siku mathalani uhuru, muungano, maandamano na mauaji ya kisiasa, uchaguzi nk. Mambo katika siasa au issues ni pamoja na Hoja za kisiasa kama ajenda ya ufisadi, katiba mpya, Sera, ilani za uchaguzi nk wakati mirengo ni pamoja na itikadi, madhumuni ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, falsafa nk.

Ngoma ipi ambao CCM inapiga na BAVICHA inacheza??????? Je katika Siasa hakuna matukio???

Mwanasayansi wa siasa Halold Laswell anasema siasa ni "unapata nini, muda gani au wakati gani, nani anapata, kwa maslahi ya nani na anapata nini??". Tafsiri ya maana ya Laswell ni kuhusisa siasa na matukio yanayoambatana na siasa. Mfano, Julius Nyerere alipata umaarufu wa kisiasa (political popularity) kutokana na matukio ya harakati za kudai uhuru na kupatikana uhuru. Nyerere hakupata umaarufu wa jina la baba wa taifa kwa sababu ya kuoa mwanamke mzuri au kwa kuwa ni mzanaki wa Mara. Hapana. Matukio katika harakati ndio yalimfanya Nyerere kuwa maarufu.

David Easton Mwanasayansi wa siasa alisema kwamba "siasa ni mkinzano wa mawazo au mitazamo, maono na ushawishi wa kuweza kuyafanya maoni yaliyokinzana au fikra zilizokinzana kuwa katika mirengo na muelekeo mmoja ili kupata maamuzi ya pamoja"

Ukiisoma dhana ya siasa kwa muktadha wa Easton utagundua kwamba siasa haiwezi kujitenga na ushawishi, fikra kinzani na maamuzi ya pamoja. Unaweza kuunganisha maana hiyo na mwanafalsafa mahiri Aristotle aliyesema kwamba "every human being is a political animal" kwamba kila binadamu ni mnyama wa kisiasa. Katika Tafsiri hiyo ni dhahiri shahiri kwamba binadamu anaendan na matukio. Ni mvivu wa kufikiri pekee anayeweza kudhani kwamba kuna siasa bila fikra, matukio na mirengo. Maarim Seif alikataa mkono wa Mohamed Shein katika msiba lakini kukataa mkono wa salamu wa Shein ni tukio ambalo lilikua na political impact kwa siasa za Zanzibar kama ishara ya kuonesha "GRIEVANCES"

Je Francis Charles Rafiki yangu, BAVICHA watajitenga vipi na matukio?? Je kuanzisha safari ya kuzuia mkutano mkuu maalum wa CCM halikua tukio?? Hakuna ujumbe CCM waliupata na Dunia nzima haikujifunza chochote kuhusu suala hilo?? Ukweli ni kwamba, CCM walijikuta nao ni chama cha siasa, maamuzi ya kukomoa Upinzani yalikigharimu pia chama chao cha CCM. Walipata funzo kubwa na Dunia iliona na kushuhudia.

Naomba sasa nijikite kutoa maoni yangu kuhusu Hoja tano za Francis

1/NAFASI YA MWENYEKITI IMEPWAYA

Charles Francis ameeleza kwamba mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi amepwaya sana na nafasi yake ni kubwa kuliko uwezo wake.

Mtoa Hoja ameendelea kwa kufananisha unyekiti wa Patrobas na makamu wa BAVICHA (Bara) Patrick Ole Sosopi pamoja na zama za BAVICHA chini ya uenyekiti wa John Heche na uenyekiti wa Patrobas Katambi.

Kwanza niwe muwazi kwamba utendaji wa BAVICHA chini ya Heche ulikua imara na thabiti kwa kuwa ulikua na Vijana wachapa kazi, mahiri na wenye uelewa mkubwa licha ya kwamba pia walikuwepo dhaifu. Mtoa Hoja ameshindwa kabisa kufikiri na kujua vipawa vya watu na tofauti za kimaumbile na kibinadamu.

Binadamu wote hatupo sawa, tumetofautiana sana kifikra, mitazamo, uelewa, maumbile nk. Kuna warefu na wafupi, wembamba na wanene, wakali na wapole, wachafu na wasafi. Hivyo Hivyo katika karama tumetofautiana.

John Heche ana karama kubwa sana ya uongozi, ujasiri, usikivu na mchapakazi na muongeaji sana . Patrobas hana karama ya uongeaji, hana karama ya kujichanganya sana na Vijana lakini Patrobas ana karama kubwa ya uelewa wa mambo pengine kuliko hata Heche.

Godbless Lema ni mbunge wa Arusha, ni mtu mwenye karama ya kutoa kauli zenye kila vinasaba vya ujasiri, kujaza ujasiri na kuondoa woga kwa watu. Lakini Lema Sio mtaalamu wa mambo ya Sera. Pengine leo unaweza kumuuliza swali Lema kwamba hivi Sera ya maendeleo ya afya ya CHADEMA ya mwaka 2014 inasemaje kuhusu tiba mbadala, ambulance na hospitali za kisasa?? Inawezekana kabisa Lema akashindwa kabisa kukujibu maana yeye karama yake kubwa ni ujasiri na hotuba za ujasiri. Swali hilo hilo ukimuuliza John Mnyika mbunge wa Kibamba atakujibu kwa weledi, utashi wa hali ya juu na ufafanuzi wa kujitosheleza. Mnyika ni mtu wa kufanya tafiti na takwimu, nyaraka na taarifa za kitafiti lakini si mtu wa hotuba za kujaza watu ujasiri

John Heche alikua mwenyekiti mwenye uwezo mkubwa sana lakini alikua na katibu ambaye alikua sio mwenye mvuto wa kisiasa kabisa bwana Deogratius Munishi. Heche alimbeba Katibu mkuu wa BAVICHA katika BAVICHA ndio maana katika BAVICHA ile aliyefahamika sana alikua ni John Heche na Daniel Naftal Ngogo ambaye alikua mtunza hazina wa BAVICHA. Leo Mwenyekiti wa BAVICHA Patrobas hana karama ya usemaji sana lakini ana uwezo mkubwa sana wa fikra na wakati huo huo anasaidiwa na katibu mkuu mchapakazi Julius Mwita na katibu mwenezi Edward Simbeye pamoja na makamu mwenyekiti Bara Patrick Ole Sosopi.

Utofauti wa kibinadamu (Human differences) ndio huo huo uko kati ya Patrick Sosopi na Patrobas Katambi. Katambi sio msemaji na mtu wa kujichanganya lakini Patrobas ni jasiri, mtu wa kujichanganya lakini pengine anaweza kuwa na busara sawa na alivyo Patrobas. Patrobas ana kipawa chake cha ujenzi wa Hoja sana katika vikao lakini hana kipawa cha ujasiri.

Halma James Mdee Mwenyekiti wa Bawacha Taifa ni jasiri na mwenye uwezo mkubwa sana kuliko pengine katibu mkuu wake Grace Tendega lakini Inawezekana Tendega akawa na kipawa cha uwezo fulani zaidi ya Halma Mdee.

Ni vema tofauti za kibinadamu zikaeleweka na kutambuliwa vizuri. Kupuuza tofauti za kibinadamu na kutoa hukumu ni kuziba fikra zetu na kuweka ukungu katika bongo zetu. Mtu mfupi asihukumiwe kwa kushindwa kuchuma embe katika mti, anaweza kuwa mzuri kuokota Fedha ardhini kuliko mrefu.

Kwa mujibu wa Katiba ya BAVICHA ibara ya 5.4.2 kuna kazi kuu tatu za mwenyekiti. Kazi ya Kwanza ni kuongoza vikao vyote, kuwa msemaji wa Baraza la Vijana wa CHADEMA, ni kiongozi mkuu wa Baraza.

Mtoa Hoja hajaeleza chochote kuhusu kushindwa kwa mwenyekiti au kupwaya kwa mwenyekiti katika majukumu yake. Je katika kazi za Patrobas Katambi kama mwenyekiti wa Baraza la Vijana ni kazi gani hasa aliyoshindwa kuitekeleza ukiacha udhaifu wa kibinadamu wa kutokua msemaji sana sana kama alivyo John Heche na Patrick Sosopi????

2/BAVICHA IMEKOSA HOJA MBADALA KUSAIDIA CHAMA.

Mtoa Hoja ameeleza kwamba, BAVICHA haina mkakati wowote wa Baraza na Hivyo ni Baraza linalosubiri tu maamuzi ya Chama.

Mtoa Hoja amekwenda mbali zaidi kushambulia wale wote ambao hawakubaliani na Hoja yake kwamba watakaopinga au wafia chama ni watu wasiofikiri. Kwanza hii ni ishara kwamba Mtoa Hoja sio muumini wa demokrasia anayoitaka. Huwezi kufunga milango ya hoja kinzani kwa kutaka kuaminisha kwamba Mtoa hoja umehodhi ukweli kwamba ulichozungumza ni cha kwanza na cha mwisho na ndio ukweli usiopingika. Huko ni kuhodhi ukweli wakati ukweli haumilikiwi na mwanademokrasia mzuri ni yule ambaye hafungi milango ya kuita wapinzani wake katika hoja ni wasiofikiri. Mtoa hoja hana tofauti na wale wasiopenda hoja kinzani kwa kuwapachika majina ya msaliti, mamluki, umenunuliwa, unatumika na majina mengine kama hayo.

Hivyo mimi niko tayari kuitwa jina la nisiyefikiri na Mtoa hoja kwa kuvunja mlango wa hoja yake.

Daniel Ezekiel Daniel alitoa hoja kwa Viongozi waandamizi wa BAVICHA Taifa hasa kwa Edward Simbeye ambaye aliwasilisha maoni ya mkakati kwa mwenyekiti na hatimaye kuutekeleza kwa sehemu na baadhi ya mambo kuwasilishwa Kamati kuu. Mfano,BAVICHA iliweza kuwasilisha mpango mkakati wa kusaidia CHASO kuwa na uwakilishi katika chama. Mwishoni mwa Februari 2016 na mwanzoni mwa Machi 2016 BAVICHA iliitisha mkutano wa waratibu wote wa CHASO na kumuita Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA ambaye ni Naibu katibu mkuu Zanzibar Salumu Mwalimu kujadiliana kwa pamoja kuona ni namna gani CHASO inaweza kuhakikisha kwamba inashiriki katika vikao mbali mbali vya juu vya CHADEMA na kupatia ufumbuzi matatizo ya CHASO. Mkutano wa Baraza kuu la CHADEMA TAIFA lililofanyika jiji la Mwanza tarehe 12 na 13/3/2016 CHASO ilipata wawakilishi katika mkutano huo. Huo ni mkakati wa BAVICHA

BAVICHA imetoa maoni ya mkakati ya kurekebisha Sera mbali mbali za CHADEMA hasa Sera ya Vijana ya CHADEMA ya mwaka 2014, BAVICHA imefanya ziara za Baraza nchi nzima kuanzia Morogoro mpaka Kigoma kama mkakati wake wa ujenzi wa Chama.

BAVICHA imesaidia kupatikana kwa wabunge Vijana viti maalum kama njia ya motisha kwa Vijana Mfano Aida Khenani, Upendo Peneza, Jesca Kishoa na Vijana wengine kwa kuwatetea Kamati kuu na kuonesha wanaweza.

Bavicha imetoa ushauri mbali mbali kwa Kambi ya ya Bungeni.

Ipo pia mikakati mingine muhimu ambayo haitatajwa hapa ambayo ni zao la BAVICHA. BAVICHA Ipo kuanzia katika matawi mpaka Taifa. Sio lazima kila jambo liamuliwe na kufanywa na BAVICHA Taifa.

Mtoa hoja ni kijana wa BAVICHA, ameshauri nini kwa BAVICHA kama kijana kutoa hizo hoja mbadala????? Hoja mbadala kwa chama ni zipi badala ya kulaumu na kujimilikisha ukweli kwamba kupinga hoja hiyo ni kutofikiri?????

Wajibu wa mwanachama wa BAVICHA umeelezwa vema katika ibara ya 4.3(a-i) katika katiba ya BAVICHA. Je Mtoa hoja amekekeleza Wajibu gani ili kupata hoja mbadala kwa chama????

Ibara ya 4.3(g) inamtaka kila mwanachama wa BAVICHA "Kushirikiana na Viongozi na wanachama katika kutekeleza Sera na mipango mbali mbali ya chama"

Je Mtoa hoja ameeleza chochote kuhusu utekelezaji wa wajibu huo ili baraza lisiwe tegemezi kwa mikakati ya CHADEMA????

3/MIGOGORO YA BAVICHA NA CHASO.

Ni kweli kabisa kwamba Uhusiano wa BAVICHA na CHASO kabla ya Februari 2016 ulikua hafifu na dhaifu sana.

Lakini kuanzia Machi 2016, BAVICHA imejitahidi sana kuhakikisha CHASO zinaimarika na kuboresha Uhusiano wake na BAVICHA. CHASO kwa sasa ina uwakilishi wake katika vikao vikubwa vya chama katika maamuzi. CHASO ina uwakilishi katika vikao vya juu kabisa vya chama yaani Baraza Kuu na Mkutano mkuu Taifa.

Viongozi wa Bavicha ngazi ya mikoa na wilaya wameendelea kuimarisha CHASO vyuo vikuu na kutatua changamaoto mbali mbali ambazo ziko katika uwezo wao. Mfano, Mwishoni mwa Disemba 2016, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro Dicksoni Kibona, mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya Hai Ruston Msangi na Viongozi wengine wameshiriki ziara za kutembelea vyuo vikuu mbali mbali Mkoa wa Kilimanjaro na kufanya nao vikao. Mwenyekiti Bavicha Mkoa wa Mbeya George Tito , katibu wa Bavicha Mkoa wa Mbeya Gwamaka Mbughi na katibu mkuu wa Bavicha Taifa Julius Mwita na katibu mwenezi Taifa Edward Simbeye wametembelea na kufanya ziara vyuo vikuu kuzungumza na CHASO Mkoa wa Mbeya mwezi Novemba 2016

Viongozi wa kitaifa wa BAVICHA wamefanya ziara za kichama katika vyuo vikuu vya Mkoa wa Dodoma na kufanya mwezi Novemba 2016. Ziara hiyo pia imefanyika katika Mkoa wa Iringa, Morogoro.

CHASO Mkoa wa Dar Es Salaam na BAVICHA Mkoa wa Dar Es Salaam na Taifa wamefanya makongamano mbali mbali Dar Es Salaam Mwishoni mwa mwaka 2016 wakiwaalika Viongozi mbali mbali wa CHADEMA Taifa kama vile Tundu Antipas Lissu, Prof Mwesigwa Baregu, Wabunge mbali mbali nk.

Disemba 18,2016 Daniel Ezekiel Daniel, Patrobas Katambi, Joseph Kasambala, Zeud, na Viongozi wengine tulifanya ziara ya kuonana na Viongozi na wanachama wa CHASO Mkoa wa Dar Es Salaam katika ukumbi mmoja jirani na Mlimani city.

Ni Uhusiano upi huo mtoa hoja anasema umejaa migogoro ???? Migogoro inaweza kuwepo halafu makongamano na ziara za Viongozi wa Bavicha zikafanikiwa?????

Upotoshaji mwingine ni kwamba ziara za Bavicha hufanyika wakati wa mahafali pekee. Huo nao ni Upotoshaji mkubwa. Kuna mahafali gani ya CHASO yanafanyika mwezi Agosti, septemba, oktoba, Novemba, Disemba, Januari, Februari na Machi??????

Hii inaonesha kuwa, mtoa hoja hakufanya uchunguzi au utafiti kabla ya kuandika. Aliendeshwa pengine na hisia na Hivyo kujipotosha na kupotosha.

Uhusiano wa Bavicha na CHASO kwa sasa umeimarika na unaendelea kuimarika na kuboreshwa zaidi. Kama ni asilimia basi Uhusiano wa CHASO na BAVICHA ningetoa 92%.

4/BAVICHA YA KULALAMIKA NA KUTOA MATAMKO

Mtoa hoja ameeleza kwamba Bavicha haina siasa za utekelezaji bali matamko tu na kulalamika na akatolea Mfano Bavicha kutoa tamko la wanafunzi vyuo vikuu kukosa mikopo.

Kwanza naomba nishangae kidogo, mtoa hoja aliwahi kulalamika kati ya tarehe 8-9/12/2016 kwamba ni kwa nini CHADEMA na BAVICHA haitoi tamko kupotea kwa Ben Saa Nane??? Alilamika sana siku ile. Je alitaka Bavicha watoe tamko la utekelezaji upi????

Leo anasema kwamba Bavicha imejaa matamko yasiyo ya utekelezaji. Je tamko la Bavicha kuitaka Serikali kutoa mikopo kwa wanafunzi vyuo vikuu utekelezaji wake ni upi????.

Je Bavicha ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi vyuo vikuu?? Kama ndio, Bavicha inakusanya kodi???? Je mtoa hoja alitaka Bavicha ikachukue Fedha hazina na kuwagawia wanafunzi??

Bavicha ni taasisi ndani ya CHADEMA na kazi yake kubwa ni kuonesha kwamba Serikali ya CCM iwajibike kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi kwa kuwa inakusanya kodi. Bavicha inaitaka Serikali na Serikali kama ni ya wananchi kweli ingesikiliza Bavicha na kutoa mikopo. Kama Serikali haitaki kuwajibika basi wananchi wote wanaweza kuiwajibisha kwa kuwapa kazi wabunge kumkataa waziri mkuu au kupitisha azimio la bunge kutokua na imani na Rais na kumuondoa madarakani (impechment of president).

Bavicha has nothing to do with university students loans zaidi ya kuitaka Serikali kutekeleza matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 8(1)(a)-(d), kupitia mahakama na njia nyingine za uwajibishaji wa Serikali.

Bavicha ni sawa na Kambi ya Upinzani Bungeni. Kambi ya Upinzani hutoa mawazo mbadala na muda mwingine huitaka Serikali kufanya mambo kadhaa. Ni jukumu la Serikali kufanya au kutokufanya jambo hilo. Mfano, Kambi ya Upinzani inataka muswada wa huduma za habari urekebishwe lakini Serikali inapuuza. Unataka Kambi ya Upinzani ifanyeje???

Au unataka Bavicha iongoze maandamano ambayo Charles Francis ameeleza mara kadhaa kwamba ni njia za kizamani kwamba zije njia mbadala ambazo hazielezi ni mbinu gani????

Bavicha ni watch dog (mbwa mwangalizi) hana mamlaka ya kuuma mgeni au mwizi anaweza kumuonesha Mwenye nyumba kwamba kuna mgeni au mwizi nje na Mwenye nyumba kuchukua hatua. Bavicha inafanya kazi nzuri ya kuwa watchdog. Kazi hiyo pia inafanywa na madhehebu ya dini, taasisi zisizo za kiserikali, Kambi ya Upinzani nk.

5/BAVICHA IMEKOSA VIONGOZI WA JUU KUKOSOA CHAMA.

Mtoa hoja amejaribu kutoa hisia zake wala sio hoja. Hajatoa uthibitisho wowote ni kivipi hakuna Viongozi wa juu wa Bavicha ambao hawakosoi chama zaidi zaidi ameishia kusema hawahoji kuhusu ruzuku na hawako jasiri kama Malema wa Afrika Kusini.

Francis Charles anapaswa kusoma katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 toleo la 2014 kanuni za uendeshaji wa chama maadili ya Viongozi kanuni namba 10.1(xi) na hata 10.1(xii) inayomtaka kiongozi yeyote wa CHADEMA KUKOSOA chama ndani ya vikao vya chama.

Je mtoa hoja anaweza kututhibitishia kwamba Viongozi wa Juu wa Bavicha hawakosoi chama katika vikao????

Mtoa hoja ni mjumbe wa kikao gani cha chama ambacho ameona Viongozi wa juu wa Bavicha hawahoji Chochote??? Ni mjumbe wa Kamati kuu, Baraza kuu, Sekretariet ya Kamati kuu, mjumbe wa Kamati tendaji Bavicha taifa, mjumbe wa Sekretariet ya Bavicha?? Ni kwa vipi anaweza kuthibitisha bila shaka kwamba Viongozi hao wa juu wa Bavicha ni mabubu katika vikao vya chama????

Au mtoa hoja alitaka kwamba, Patrobas Katambi, Julius Mwita, Patrick Ole Sosopi, Zeudi, Edward Simbeye aitoshe vyombo vya habari na kuanza KUKOSOA chama hadharani ndio ajue huwa wanakosoa?? Au alitaka Julius Mwita aandike katika ukurasa wake wa facebook na jamii forum KUKOSOA chama chake ndio ajue huwa wanakosoa????? Naomba mtoa hoja anisaidie majibu hapo. Kwamba ni criteria ipi ametumia kuonesha kwamba Viongozi wa juu huwa ni mabubu vikaoni kwamba hawakosoi???

Ruzuku aliyoitolea mfano kwamba hakuna kiongozi anayehoji matumizi yake nayo ni kihoja kingine. Kuanzia Mwezi Agost 2016 CHADEMA imepeleka Ruzuku katika ofisi za Kanda zote 10 Za CHADEMA na ofisi za Kanda kutoa Ruzuku hizo katika majimbo yote ndani ya Kanda husika. Labda changamoto ni kwamba ni kiasi kidogo sana. Mpaka kufikia Disemba 2016 karibu majimbo yote 36 Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) yanapata Fedha za Ruzuku. Changamoto inayobakia sasa ni kwamba ni Fedha kiasi kidogo sana zinazotolewa.

Mtoa hoja anamalizia kwamba kuna makundi ya mitandaoni kwamba Kuna kundi la Friends of Bavicha, CHADEMA Asilia na Bavicha Asilia.

Kwanza makundi hayo mawili ya Bavicha Asilia na CHADEMA Asilia yalikuwepo wakati aliyekua katibu mkuu wa CHADEMA Dk Slaa kujiuzulu. Walikuwepo waliokua wanajiita wafuasi wake na wakadai kuwa CHADEMA ilipompokea Edward Lowassa ilipoteza uhalisia wake hivyo wakataka CHADEMA Asilia kwa hoja kwamba CHADEMA imeacha kuhoji ufisadi. Kundi hilo liliisha nguvu na kwa sasa hakuna kundi kama hilo ndani ya CHADEMA bali wapo wanaoamini uwezo wa Dk Slaa lakini sio wafuasi wake bali wafuasi na wanachama wa CHADEMA.

Kundi la Friends of Bavicha ni kundi salama kabisa ambalo mimi Daniel Ezekiel Daniel ndiye muanzilishi wake nikishirikiana na maadimin wenzangu Hilda Newton na Ruston Msangi. Kundi hilo la whatsaap lina wanachama wa CHADEMA na Viongozi mbalimbali akiwepo mheshimiwa Freeman Mbowe, Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Wajumbe mbalimbali wa Kamati kuu, Viongozi mbalimbali wa Kanda, mikoa, wakurugenzi wa chama taifa, wakuu wa idara CHADEMA TAIFA, Wabunge zaidi ya 30 nk. Hivyo usifanyike upotoshaji kwamba kundi la Friends of Bavicha ni kuonesha mpasuko lahasha, ni kundi la watu makini na wanachama wa CHADEMA na Viongozi wakuu wa Chama na BAVICHA.

NB.
Haya ni maoni yangu binafsi Daniel Ezekiel Daniel kama mwanachama wa CHADEMA na kijana wa Bavicha..

******************************

Daniel Ezekiel Daniel (DED)
Mwanachama wa CHADEMA
danielezekiel2222@gmail.com
ILEJE
 
Mkuu hapa unatetea TUMBO lako tu....TUAMBIE KWANZA NI MATAMKO MANGAPI BAVICHA WAMEISHA YATOA TOKEA MAGUFULI AWE RAISI WA NCHI HII...na je hayo matamko ni yapi UTEKEREZAJI WAKE?????maana kwa haraka haraka hakuna taasisi iliyoongoza NDANI YA NCHI HII kutoa matamko kwa awamu hii kama BAVICHA tena matamko ambayo yaliitaji utekerezaji iwapo tu WASIPOTIMIZIWA wanachokitaka,,,lakini hawajawai timiziwa hitaji lao na MWISHO WASIKU na wao kukunja mkia......UKWELI LAZIMA USEMWE KAMA KAULI MBIU YA CHADEMA KWENYE AWAMU HII.....SASA UKWELI NA SISI TUNAWAPA tunataka kujua hao BAVICHA ni kiasi gani wameisha kitumia kupitia haya matamko yao...MAANA INASEMEKANA wanapata posho mno kupitia haya matamko ndio maana kila uchwao na MATAMKO YASIYO KUWA NA KICHWA WALA MIGUU........MKUBALI MKATAE CHADEMA YA LEO INAPUMULIA MACHINE......hata wafuasi mlio nao nafsi zao zinasuta kabsa JUU YA CHADEMA ya sasa......Na soon moto utalipuka huko ni suala la muda tu......
 
Njia ya muongo na mnafiki ni fupi sana,

Sasa tulishaijua rangi halisi ya chadema, wanatudanganya watapambana na mafisadi kumbe wanakuja kutetea na kukumbatia mafisadi!!!!
 
IMG_20170102_140137_126.jpg
 
Mkuu hapa unatetea TUMBO lako tu....TUAMBIE KWANZA NI MATAMKO MANGAPI BAVICHA WAMEISHA YATOA TOKEA MAGUFULI AWE RAISI WA NCHI HII...na je hayo matamko ni yapi UTEKEREZAJI WAKE?????maana kwa haraka haraka hakuna taasisi iliyoongoza NDANI YA NCHI HII kutoa matamko kwa awamu hii kama BAVICHA tena matamko ambayo yaliitaji utekerezaji iwapo tu WASIPOTIMIZIWA wanachokitaka,,,lakini hawajawai timiziwa hitaji lao na MWISHO WASIKU na wao kukunja mkia......UKWELI LAZIMA USEMWE KAMA KAULI MBIU YA CHADEMA KWENYE AWAMU HII.....SASA UKWELI NA SISI TUNAWAPA tunataka kujua hao BAVICHA ni kiasi gani wameisha kitumia kupitia haya matamko yao...MAANA INASEMEKANA wanapata posho mno kupitia haya matamko ndio maana kila uchwao na MATAMKO YASIYO KUWA NA KICHWA WALA MIGUU........MKUBALI MKATAE CHADEMA YA LEO INAPUMULIA MACHINE......hata wafuasi mlio nao nafsi zao zinasuta kabsa JUU YA CHADEMA ya sasa......Na soon moto utalipuka huko ni suala la muda tu......
UTEKEREZAJI=Utekelezaji!!
Ila umeeleweka hivo hivo
 
Njia ya muongo na mnafiki ni fupi sana,

Sasa tulishaijua rangi halisi ya chadema, wanatudanganya watapambana na mafisadi kumbe wanakuja kutetea na kukumbatia mafisadi!!!!
Ma
Njia ya muongo na mnafiki ni fupi sana,

Sasa tulishaijua rangi halisi ya chadema, wanatudanganya watapambana na mafisadi kumbe wanakuja kutetea na kukumbatia mafisadi!!!!
mafisadi gani wewe wakati mwakyembe amesema mahakama imekosa mafisadi! au huelewi unazungumza nini?
 
Tatizo letu vijana tuliowengi huwa tunaweka vyeti vyetu nyumbani na kutembea na maamuzi ya watu wengine vichwani mwetu.Hoja za Francis zina mashiko sana kwa anayeifahamu vizuri CHADEMA. Ila kwa mtu ambaye ameifahamia CHADEMA mwaka 2014 kwenye mkutano mkuu wa Chama pale Mlimani City,ni ngumu kujua.
 
Mleta uzi nafikri hujui kuwa muda ni resource ghali kuliko vyote! Time is precious my dear. Makala ndefu afu haina utumbo ni upuuzi mwingine.
 
Back
Top Bottom