Heche ameondoka na BAVICHA?

Heche ameondoka na BAVICHA?

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
579
Reaction score
887
Wanajamvi sijui ni mimi pekee au na wenzangu mnaona. Nilitarajia moto mkubwa zaidi na harakati kali zaidi kutoka BAVICHA mpya zaidi ya zile za Heche hasa katika masuala nyeti ya kitaifa kama Escrow nk, ila cha kushangaza sisikii kashikashi zozote kutoka Bavicha wala sijaona harakati za kiujanaujana zinazotingisha nchi toka wamechaguliwa vipi kulikoni wanajamvi?

Nimefurahi kumuona Heche juzi akiendelea kupambana kwa kuwahamasisha vijana kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ila sijasikia Bavicha wakihamasisha mambo hayo wala masuala nyeti ya Kitaifa zaidi ya ile ziara ya Mbowe aliyofanya nao na perfomance yao haikuwa nzuri ya kuwafanya waonekane wapo sasa sijajua BAVICHA kulikoni wako wapi?

Bawacha, Mdee yuko Bungeni nyie mko wapi?
 
mkuu sasa hivi mambo ni kimya kimya
 
Mwenyekiti wa Bavicha ni kijana wa Diallo.
 
Hakuna heche alivuruga sana bavicha walikula pesa zote wakafungua maduka kariakoo kwahiyo sasa bavicha hakuna hela watafanya mikutano na nini kwani hata kutoa matamko lazima pesa ili kulipa wandishi wanaokuja.
 
Huyu jamaa ni bora afanye kazi, bavicha used to be very active, we anticipate the same pace and more to happen. Please Mwenyekiti Mpya, KAZI IFANYIKE SASA hadi 2019.
 
Hata mimi nimeliona tatizo hilo, kwa mazingira ya nchi watu waliokuwa wamelala na kuzoea siasa za propaganda bila kupitisha amshaamsha ya nchi nzima ni ngumu.

Bila kupiga debe la nguvu watu bado wanaamini CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi kumbe hizo nembo zimebaki kwenye bendera, sasa hivi ni chama cha wafanya biashara tena nyingi ni zisizo halali kama mikataba isiyo na tija kwa nchi, wanyama kuuzwa kinyemela na mauaji ya tembo, unga ndio imekuwa dili kubwa kwenye chama hicho.

Uwezo wa kushawishi kama wa Nyerere watu wajitolee kujenga nchi haupo na kujenga hoja umewaishia bali wamebaki kutumia jeshi kulazimisha mambo.

Ama Bavicha Iimekabidhiwa kwa Checkbob anayejivunia elimu ya vitabuni bila kuleta mtaji wa watu. Tunataka watu sio kushinda ofisini kupitia mafaili wakati watu hawajui.

Hivi bavicha wameshindwa hata kukusanya dhuluma zilizofanyika nchi nzima kwenye uchaguzi wa s/m na kuueleza umma na dunia kwa ujumla. Au mnangoja mpaka mauji yatokee huko mbeleni ndio mjifanye kulialia.

Watu wanatishiwa, kuumizwa na hata kuuwawa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba nyinyi mnakaa kwenye viyoyozi mnaangalia tv, kuchat kwenye facebook na miwhatsapp!!! Au mnangoja wazee wa kina Slaa waitishe maandamano ndio mvae magwandwa?

Nendeni mahakamani kama vijana ili tuone mahakama ikiepuka wajibu wake hapo umma utakuwa tayari kuchukua hatua. Au mimi ndio sijui wajibu wa bavicha? Muda wa kujipaka manukato na kutembea na kalamu na milaptop sio huu. Vijana ndio dira ya nchi na sio akina Slaa. Hao akina Slaa wabaki washauri tu. Au mmelewa ile propaganda ya vijana ni taifa la kesho!!?
 
Ccm tumeshaiweka BAVICHA mfukoni, bado BAWACHA
 
Bwana Paschal Patrobass pamoja na tetesi nyingi kipindi cha uchaguzi wa mabaraza ya Chadema, tuliamini ilikuwa ni sehemu tu ya mambo ya uchaguzi ambao hauwezi kuisha bila vijembe, vitina na kuzushiana.

Ilisemwa sana na baadhi ya watu wa ndani na nje ya chama kwamba una ''link'' na mafisadi ambayo ingeweza kuwa kikwazo cha utendaji wako katika chama. Watu huru ikiwemo mimi sikuamini hayo na bado sitaki kuamini.

Lakini ukimya wako unaanza kunitisha sasa, pengine bado unashangilia ushindi au size ya kiatu cha J.Heche ni kubwa kiasi cha kusubiri kwanza mguu ukue ndo ukivae.

Pamoja na mambo mengine, John Heche na timu yake ni kati ya mabaraza ya chama yaliyotia hamasa sana kwa vijana kuipenda CHADEMA. Au huamini kuwa wewe ni mtu ''mzito'' nchi hii. Mwenye kutoa kauli na kukemea. Mwenye nafasi ya kupaza sauti ya vijana, mwenye nafasi ya kuwasemea hata UVCCM kwa mambo ambayo wamepigwa kufuli kuyasemea.

Nani amemsikia huyu bwana uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ESCROW jeeh.

Please endana na kasi ya siasa za Tanzania na fuata nyayo za John Heche ambaye alikuwa ndani ya jamii mda wote akisema hili na lile.
 
Binafsi nilitaka mtu kama Ephata awe mwenyekiti.
Hawa wazee wa busara hawatusaidii sana
 
Muongo mkubwa hana undugu na dialo hata chembe.

Mkuu usibishe Sana hata kama Hawana undugu alikuwa mwajiriwa pale, ndiye alikuwa HR na mimi alinifanyia interview......kiukweli jamaa ni mpole Sana,amepoa katika suala LA kufanya maamuzi, nenda star TV pale mwanza uulize.
 
Waliokuwa na uongozi wa kuipeleka BAVICHA mbele walipigwa chini kwa visingizio mbalimbali vikiwemo umri,Sasa wamewekwa watu wa Mheshimiwa flani na matunda yake ndo hayo yanaonekana.Pole sana Ben Saanane!
 
Patrobass Ni Kiongozi Mzuri wa aina yake nakiri si caliber ya Heche. bado anajisimika unajua media zatu zinataka connections. kazi anapiga kila Leo mfano Alikua Kahama juzi akitokea shy. Jana alikua Arusha kwenye kumbukizi. za trh 5. Jamaa anamtihani wa kujenga Presence yake. Kama Salum Mwalim
 
Waliokuwa na uongozi wa kuipeleka BAVICHA mbele walipigwa chini kwa visingizio mbalimbali vikiwemo umri,Sasa wamewekwa watu wa Mheshimiwa flani na matunda yake ndo hayo yanaonekana.Pole sana Ben Saanane!

Jamaa anahitaji media connection Tu mziki anauweza. Engine chuki Tu kubali matokeo songa mbele. Hii tabia ya chuki kwa washindi Mwisho wake Ndo Yale ya akina Mwampamba dhidi ya Heche.
 
Waliokuwa na uongozi wa kuipeleka BAVICHA mbele walipigwa chini kwa visingizio mbalimbali vikiwemo umri,Sasa wamewekwa watu wa Mheshimiwa flani na matunda yake ndo hayo yanaonekana.Pole sana Ben Saanane!

namjuwa patrobas na mimi binafsi si mwanachadema ni ccm damu nimesoma nae SAUT akiwa law four mimi nilikuwa law two alitupa taabu sana ktk kuimarisha tawi la ccm na asingekuwa mwenyekiti wetu kipindi hicho moud sijuwi ingekuwa vipi maana hata yaledy alizidiwa sana kete na akina patrobas. napenda sana nchi yangu isonge mbele bila kujali itikadi za vyama. tunahitaji vijana watakao fanya nchi yetu isonge mbele bila kujali itikadi zetu. tanzania ni yetu sote we have not to think only of ourselves we have also to think about our next generation. dogo patrobas anatoka kahama nijuavyo mimi jitahidini basi kuondoa dhana ya ukanda. you have to think big
 
Mkuu hapo mwisho umeleta upuuz weni!! kwani Heche anatokea Kibosho?...
 
Hata mimi nimeliona tatizo hilo, kwa mazingira ya nchi watu waliokuwa wamelala na kuzoea siasa za propaganda bila kupitisha amshaamsha ya nchi nzima ni ngumu. Bila kupiga debe la nguvu watu bado wanaamini ccm ni chama cha wakulima na wafanyakazi kumbe hizo nembo zimebaki kwenye bendera, sasa hivi ni chama cha wafanya biashara tena nyingi ni zisizo halali kama mikataba isiyo na tija kwa nchi, wanyama kuuzwa kinyemela na mauaji ya tembo, unga ndio imekuwa dili kubwa kwenye chama hicho. Uwezo wa kushawishi kama wa Nyerere watu wajitolee kujenga nchi haupo na kujenga hoja umewaishia bali wamebaki kutumia jeshi kulazimisha mambo. Ama Bavicha Iimekabidhiwa kwa Checkbob anayejivunia elimu ya vitabuni bila kuleta mtaji wa watu. Tunataka watu sio kushinda ofisini kupitia mafaili wakati watu hawajui. Hivi bavicha wameshindwa hata kukusanya dhuluma zilizofanyika nchi nzima kwenye uchaguzi wa s/m na kuueleza umma na dunia kwa ujumla. Au mnangoja mpaka mauji yatokee huko mbeleni ndio mjifanye kulialia. Watu wanatishiwa, kuumizwa na hata kuuwawa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba nyinyi mnakaa kwenye viyoyozi mnaangalia tv, kuchat kwenye facebook na miwhatsapp!!! Au mnangoja wazee wa kina Slaa waitishe maandamano ndio mvae magwandwa?

Nendeni mahakamani kama vijana ili tuone mahakama ikiepuka wajibu wake hapo umma utakuwa tayari kuchukua hatua. Au mimi ndio sijui wajibu wa bavicha? Muda wa kujipaka manukato na kutembea na kalamu na milaptop sio huu. Vijana ndio dira ya nchi na sio akina Slaa. Hao akina Slaa wabaki washauri tu. Au mmelewa ile propaganda ya vijana ni taifa la kesho!!?

Ndugu yangu tindo

Hayo ndiyo majembe ya BAVICHA!.

Hata mwaka haujaisha mmeshaanza kuwarushia ngumi?.

Wenzenu ni vijana wa kidijitali!.

Wanaendesha mambo kisayansi ya dijitali!.

Sasa mnataka wakafanye nini kwenye wakati mnasema CCM imeshindwa kwenye uchaguzi na pia kwa sasa CCM inajifia!

Au ndiyo zile lugha za propaganda. Mkitoka nje mnasema CCM imekufa lakini mkirudi ofisini mnaanza kutingisha vichwa!.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom