Hebu tukumbushane machungu ya timu zetu siku tulipojutia kwenda uwanjani au Vibanda Umiza

1. Manchester United 3 Bayern 2
Mechi ya mkondo wa kwanza Wayne Rooney alichomwa sindano ya ganzi ili acheze, tukafa 2 kwa 1.

Mechi ya marudiano Arjen Robben anafunga bao la kikatili sana, hakika niliumia sana.

2. SIMBA SC vs UD SONGO (kwa mkapa)
Daah! Luis Miquesson alikua mwiba sana, nilihisi kutoa machozi
Mechi ya kwanza nafikiri ndio Rooney aliumia ya marudiano akalazimika kuchomwa sindano ili acheze na kwa mchango wake tuliongoza 3 bila hadi apo anaanza kuchechemea ikabidi atolewe bayern wakaamka sasa
 
Kwamba simba ilikua haifungiki au mpinzani anunue mechi? Sikubaliani na hili.
Mimi nilikuwaga mtoto bwana,sijui ilikuwaje,lakini ilikuwa mechi yenye presha,iliyosubiriwa kwa hamu,iliongelewa sana tanzania nzima,ilionekana kama simba atashinda tu,ikizingatiwa ilikuwa ueanja wa nyumbani,ndio maana baada ya kufungwa,watanzania wengi waliumia.
 
Kama wewe ulimwaga chozi baada ya cristiano ronaldo kumwaga chozi alipoumia kwenye fainali ya EURO dhidi ya france ,hebu tujuane,najua mpo humu
 
2006 mwaka ulikuwa si sehemu yangu ya kushangilia vikombe..

Arsenal tunakufa fainali ya uefa vs barca
Kisha
France anakufa fainali ya world cup vs italy
hiyo nakumbuka kibanda umiza nipo na blo angu machozi yakimtoka jinsi Arsenal anavyo tafuta mpira kwa tochi ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kushabikia washika mitutu, kaka mkubwa mpaka kaenda kaburini hakuwahi shabikia timu yeyote ile 😭 litimu la arsenal lilimpa maumivu kaka yangu shwaini 😠
 
hiyo nakumbuka kibanda umiza nipo na blo angu machozi yakimtoka jinsi Arsenal anavyo tafuta mpira kwa tochi ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kushabikia washika mitutu, kaka mkubwa mpaka kaenda kaburini hakuwahi shabikia timu yeyote ile 😭 litimu la arsenal lilimpa maumivu kaka yangu shwaini 😠
Pole ndugu ndio maana hujui hata unashabikia timu gani?
 
hiyo nakumbuka kibanda umiza nipo na blo angu machozi yakimtoka jinsi Arsenal anavyo tafuta mpira kwa tochi ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kushabikia washika mitutu, kaka mkubwa mpaka kaenda kaburini hakuwahi shabikia timu yeyote ile litimu la arsenal lilimpa maumivu kaka yangu shwaini
Dah! Apumzike kwa amani huko alipo chief..

Lakini ulitegemea nini kwa timu iliyolula umeme dakika ya 18 sijui.. Ilikuwa ni suala gumu kidogo na th14 alituua, alikosa goli kadhaa za wazi usiku ule.
 
Kumbe we mkongwe, Simba alipigwa2-0. Zile Kia zikaota mbawa. Hata hivyo inasemekana hiyo mechi mdhamini mkuu wa Mnyero fc kipindi hicho Azim Dewji aliuza hiyo mechi.
Simba hawatakuwa na kikosi kikali kama kile. Walikuwa wanagawa dozi si nyumbani si ugenini. Hichi cha sasa ni maneno tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom