Hebu soma tafakarini kisa hiki!

amanindoyella

Senior Member
Oct 13, 2009
104
9
Kuna jamaa mmoja nimwite kwa jina la YUDA alikuwa ameoa na wamejaliwa na Mungu watoto watatu. Alikuwa anafanya biashara ya kuuza miwa hapa kijijini kwetu, maisha yalivyokuwa yanaendelea alianza mahusiano ya mapenzi na dada mmoja naomba nimuite Bi Kiroboto huyu alikuwa mke wa mtu na alikuwa na watoto wawili wakati huo. Wakati Yuda yupo ktk mausiano na Kiroboto aliachika na mumewe wa kwanza.
Wakati mahusiano kati ya Yuda na kiroboto yanapamba moto, Yuda akaanza kumaliza mtaji wake wa miwa. Akalazimika akope kwa rafiki yake kiasi cha Tshs 10,000/= Baada ya mahusiano kunoga Yuda alihama nyumbani kwake na kuhamia kwa hawara na kuiacha familia yake pasipo na msaada wowote.
Baada ya muda kupita bila kulipa deni rafiki yake akaanza kumdai na jamaa akaamua atorokee kijiji jirani kwa kushidwa deni la 10,000. Masika ikamkuta huko huko akatafuta shamba na kulima baada ya mavuno akarudi kijijini na kuchukua familia yake.
Aliporudi alikuta Bi. Kiroboto ameolewa na mtu mwingine na kutimkia Tabora kwa shughuli za kilimo cha tumbaku.
Yuda aliishi kijiji cha jirani kwa muda wa mwaka mmoja na miezi kadhaa, nako huko mambo yakawa hayaendi vizuri. Wakati wapo huko akafiwa na mwanae wa kiume, akaamua kurudu tena kijijini kuanza maisha mapya.
Wakati wapo kijijini Bi. Kiroboto alirudi na mumewe wa pili na inasemekana maisha yao yalikuwa si swali kwani mume alikuwa anampiga sana mke. Maisha yao yalikuwa ya kulima vibarua kwenye mashamba ya tumbaku na walijikusanyia laki sita(600,000) na kurudi nazo kijijini. Walipofika wakagawana kila mmoja laki tatu(300,000)
Bi. Kiroboto alivyopata mgao wake akaamua amrudishie mumewe laki moja(100,000) ili kila mtu achukue taimu zake. Jamaa aliridhia baada ya kurudishiwa mahali yake! Makubwa haya!
Bi. Kiroboto akarudi kwa wazazi wake na alikuwa mwenye afya nzuru sana yaani alikuwa anapendeza na kuvutia sana.
Yuda akaanza tena mahusiano na Bi. Kiroboto, Yuda akaanza manyanyaso kwa mkewe na baadaye akamwacha kabisa mkewe wakagawana mali. Yuda kuhamia kwa Bi. Kiroboto(hawara) wakawa wanakula maraha kama zamani.Maisha yakaendelea hatimaye mke wa Yuda akaolewa na mtu mwingine hapohapo kijijini.
Mwezi wa tisa 2011 Bi. Kiroboto amefariki kwa kujaribu kutoa mimba! Kumbuka Yuda alikuwa anaishi kwa wakwe na aliyekuwa anamfanya aishi hapo ameshafariki
Je ingekuwa ni wewe ungefanyaje? Pili jamaa alikuwa anadaiwa elfu 10,000/= tu lakini anashindwa kulipa hadi anakimbia kijiji? Tatu nini mwanamke/mwanamume kuwa na mahusiano mengi?
 

amanindoyella

Senior Member
Oct 13, 2009
104
9
[QUOTE=Mwanaweja;ulimbukweni huo wla hakuna jipya na wajinga ndio waliwao

Mkuu kwanini unasema hivyo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom