Hebu sema, ulishapiga/kupigwa na mpenzi wako?

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Wananzengo habari zenu hapa

Leo nimewaza jambo hili baada ya kuona kuna uzi fulani wachangiaji wake wengi wao wanaonyesha wana maisha ya vita na wake au waume au wapenzi wao yaani full vipigo,
Binafsi nimeowa na nina miaka kama 11 kwenye ndoa na tumejaliwa baadhi ya watoto lakini naomba nikiri sijawahi kumpiga wife hata mara moja,
labda kufoka na kuongea inatokea ,
ukweli kuwa kuna wakati hawa wanawake kama wametumwa kufanya zogo,yaani unahisi kabisa yaani huyu hapa anataka kofi ili atulie,
hebu niambie wewe umeshampiga mpenzi wako?
na siku ukimpiga unalala nae kitanda kimoja?
na je usiku utataka yale mambo wakati mchana umetoka kumshushia kichapo?
 
Siwezi kumpiga mwanamke yoyote yule achilia mbali mke.
Marehem babu yangu aliwahi kuniambia wakati nasoma primary maana nilikuwa nakesi nyingi za kupigana na watoto wakike,
Mwanaume wa kweli hapigi mke wake, basi kauli hiyo huwa naikumbuka sana, hata mke akinikorofisha namuadhibu kwa hisia tu
 
Duh sijawahi kumuona mshua hata siku moja akimpiga singi bi mkubwa naamini hii imenijenga sana mpaka umri huu sijawahi kumpiga mwenza wangu pamoja na udahifu wetu ila nitasaka njia nyingine sio kipigo.
 
Back
Top Bottom