Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,093
- 22,806
Naandika taarifa hii nikiwa tayari nimeshakasilishwa......
Ipo hivi......Mimi ni kijana wa kiume na fiancee wangu tunaishi maeneo ya tabata kinyerezi kwenye chumba cha kupanga(self contained). Hii wiki iliyoisha fiancee wangu alikuwa amerejea kutoka Arusha kwenye safari ya msiba wa mfanyakazi mwenzao iliyomchukua siku tatu. Nilikwenda kumpokea airport tukarejea home mida kama ya saa mbili na nusu kutoka airport...... dakika si nyingi walikuja wasichana wawili ambao walikuwa wanazunguka kukusanya maoni kuhusu huduma za kibenki chini ya kampuni yao jina limenitoka..........
Sasa hapo maskani kuna mijengo miwili tu......nyumba ya vyumba vinne kubwa na hili geto langu huku nyuma ndani ya fensi...........
Hawa wadada walipomaliza kuhoji wapangaji nyumba kubwa wakaja na mlangoni kwangu.......sasa waifu ile kuwafungulia akashangaa kuwa mojawapo ya wale wadada ni shosti yake walisoma wote primary utotoni.
Bas wale mademu wakaingia ghetto ndani........wakaketi kwenye mito kwenye jamvi maana sina makochi maana ndo kwanza naanza life na wife.....
Sasa wakati hawa manzi wametimba wife alikuwa ana andaa breakfast heavy........maana nilikuwa hata sijapiga tea.......
Basi waif akajiongeza akatoa kitu cha kutosha watu wanne......tukawa tunapiga breakfast.......sasa demu m'mojawapo alikuwa full kuwasiliana na wenzake wengine ambao walikuwa nao wanasugua gaga kwenye kazi yao hiyo hiyo akiwaambia amekutana na waifu ambaye ni shost wao so waje kumpa hi.Muda si muda wakati waif ndio anatoa vyombo na kuvipeleka nje kuosha.....wakatimba mademu wengine watatu so ikawa tupsi ya wasugua gaga watano.
Ghafla hali ya hewa ikabadilika kutoka utulivu 100% hadi utulivu 0% maana ilikuwa ni kelele mtindo m'moja hapo ndani kwa vicheko...mabishano......umbea full majanga........!
Mimi nilikuwa natazama series ya for better for worse ya tyler perry na wife......ambayo tulikuwa tunaicheki kwa utulivu na ukimya wa hali ya juu ukijumlisha na mazingira ya pale maskni eneo zima huwa ni kimya hata ikidondoshwa sindano utasikia mlio.
Sasa hawa manunga yembe wakaanza kunikinai uwepo wao maana hizo story na mabishano zilikuwa ni baina yao hadi wakamsahau waifu na mimi.......
Dakika zikawa masaa tokea saa saa nne hadi saa nane mchana hata dalili ya wao kusepa sikuona ndio kwanza wakawa wanabadili mikao na kujadili mikasa ya mabuzi na mabwana zao huko kazini kwao.......
Waif akanitext akaniambia mbona kama haupo sawa.......ngoja nitafute pozi la kuwasepesha.........nikamwambia waifu angoje kidogo watajishtukia watasepa.......
Kumbuka huo ni muda wa lunch......so waifu akamwita dogo wa boda boda akamnunulie maini.........
Waifu akazama tena jikoni akatoa kitu cha chapati na roast ya maini........tukapiga menyu tena na hawa manunga yembe ........basi tukashiba pale ila "UKAWA" mode ikawa bado ON......yaani utadhani walitumwa kutukomoa kwa kutunyima uhuru wa mimi na waifu kufanya yetu pale room .....
Basi mishale ikatembea hadi saa kumi na moja kasoro jioni. Hapo sijaoga maana ntakosa pozi la kubadili nguo........waifu anahamu na mimi anataka nimpe mambo........ila majanga ni UKAWA ya hawa manungayembe.........
Waifu ikabidi anitext akasema husband bwana me nawazingua wasepe..... basi waif akajifanya ananiomba pesa ya salooni akafumue na kuosha nywele......muda huo huo nikajifanya na mimi nimetumiwa ujumbe na mshikaji ananingojea pub tukajidili biashara......
So nikasimama nikachukua tshirt kabatini maana nilikuwa na tracksuit pants chini na vest kwa juu........sasa yule shost wake aliyekuwa wa kwanza kuja akasuggest waende na waifu saloon.....hawa wengine wawangoje wakicheki t.v then watawakuta wakirejea kutoka saloon.....
Me nkaona hapa kuna dalili kuwa hawa manunga yembe wanataka kukaba hadi penati maana siku nzima tupo nao.......mbona majanga.
Waifu akastukia mchezo akawa mnjanja.......akamwambia kuwa yeye akitoka salooni atakwenda kwa ndugu yake tabata bima na huenda akachelewa au kulala huko huko.............yule nungayembe bila hiyana akauliza na wewe shem utachelewa sana......nikamfix kuwa huyu mshikaji wangu naweza rudi hata saa nane za usiku story nyingi. Ndio ikawa ponea yetu wakafunga virago wakasepa na sisi tukitoka............tukawasogeza hadi segerea stand ili wachukue daladala tukageuza tukarudi geto tukaendelea na mahaba yetu.
Sasa swali langu.......Hivi kuna ugumu gani wa mtu kujiongeza kistaarabu unapoenda kwenye geto la mwenzako.......unashindwa hata kusoma ishara kuwa hapa nawabania wenyeji wangu uhuru wa kufanya yao.........mxeummmmmmm.........yaani mijitu ustaarabu ni zero kabisa these days kazi kuendekeza tamaa na njaa za kiboya aaaaaaaaaaghhh.