Hebu fikiria! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu fikiria!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by pascaldaudi, Oct 3, 2010.

 1. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kisha nikasikia sauti ikisema"Wafanyakazi wangu wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini hawasikii tene wana elimu lakini hawana maarifa."Je hukuona mafisadi wakikamatwa bila kushtakiwa?Hukusikia JK akitamka hahitaji kura za wafanyakazi?Je elimu yako inakusaidiaje kutambua kuwa rasilimali za nchi zinachakachuliw a na wachache?mfano madini,samaki na wanyama pori?TANZANIA BILA JK INAWEZEKANA?
   
 2. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JE HAUKUSIKIA KUWA WOTE WALIOIBA FEDHA BOT WAZIRUDISHE HAWATASHTAKIWA NA MAJINA YAO HAYATATAJWA? NA KUWA MPAKA LEO HATUJAAMBIWA KUWA FEDHA ZOTE ZIMERUDI NA ZIMEFANYA NINI? JE HATUPASWI KUCHUKUA HATUA DHIDI YA HAO?:hand:
   
 3. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We quality vipi bana? Hela si zimesharudishwa na zimepelekwa kule kwenye kilimo kwanza, na nyingine kuanzisha benki ya kilimo?? cha ziada nini unataka?? wakati mtoto wa mkulima Mizengo alikwambia mafisadi wana nguvu na wakikamatwa nchi itatikisika au wewe hutaki amani na utulivu uliopo? Hata mwema mwenyewe alisema jeshi la polisi halina uwezo wa kuwakamata kwa sababu kwanza muungwana alisema anawajua wahujumu uchumi na amewapa nafasi wajirekebishe... alipohutubia bunge SIX akamwambia aache kuchekacheka nao kilichompata wote tunakijua.

  Nafikiri Tanzania ni nchi pekee duniani ambapo mwizi wa mabilioni anaambiwa arudishe atasamehewa wakati yule hakimu aliyekula buku tano ataenda jela kwa sababu kama ni kuiba alitakiwa aibe nyingi sio kidogo!!!!!

  Hii ndio Tanzania ambayo jeshi limegeuka kuwa la Walanchi na sio la Wananchi kama ilivyokuwa enzi hizo!! Tumebaki na risasi moja tu ya kujaribu kujiokoa kwa kuhakiksaha unamlenga adui kichwani nayo ni Kadi yako ya kupigia kura>>> ukiona wanafaa warudishe waendelee na kazi yao, ukiona wamechoka wapumzishe mchague mwingine!!!!
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  je hukusikia kuwa mafisadi wa nchi hii ni watu safi,chapakazi na hodari?tafakari chukua hatua
   
 5. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nchi imekwisha. Kweli kiongozi anadiriki kusema
  1. Mafisadi wana nguvu, huwezi kuwashika!!?? Hii ni kauli ya nchi????
  2. Warudishe hatutawataja!
  Inatia hasira, CCM bye bye
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Inawezekana ukafikiria na kutaka kuchukua hatua,tatizo bado ni fikra duni wengi wanazo hasa maeneo ya vijijini ambako shule za kata zinafanya kazi yake.
  Kilichobaki si kufikiria bali ni kufanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi ambao ni huu kwa kuchagua mgombea ambaye ataleta maendeleo ya kweli.
   
Loading...