Hazina wanachelewa kutoa fedha za miradi kimkakati ili watendaji watumbuliwe?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Miradi mingi ya wizara na idara za serikali imesimama au kusuasua kwa kukosekana fedha ambazo zimepitishwa na bunge au kuahidiwa na Mhe. Rais.

Viongozi wa kisiasa wanapotembelea miradi hii nakuambia hazina awajatoa fedha utosikia wakiwakoromea hazina badala yake watamgombeza mkuu wa Idara na mkandarasi.

Ni rahisi sana mkandarasi kunyimwa kazi nakuelekezwa achunguzwe huku ukweli ukibaki kuwa fedha hazijatolewa na hazina. Wakuu wa Idara na wizara wameng'olewa kwa sababu tu hazina awatoi pesa.

Ukienda kwenye riport ya CAG na kamati za Bunge hazina wanalalamikiwa kutokutoa fedha kwa wakati au wakati mwingine kutoa mwisho wa mwaka kisha kufunga mwaka nakurejeshewa fedha hizo.

Je, hazina Kuna watendaji wenye ngozi na mioyo tofauti na watumishi wengine?

Kwanini tusianze kushughulikia hazina kabla yakuondoa watendaji wasio na hatia?
 
Fedha hakuna, siyo kwamba hazina wanachelewesha. Fedha zote zinaelekezwa eneo la kimkakati "Chato" ili iwe kama "URAYAAA".
 
Ni lazima watendaji na wakandarasi wawe ni mikakati ya namna ya kufinance miradi ya kimkakati kwa kupitia PPP,municipal bonds,Loans,etc kwa kuzingatia Ushindani wa kibiashara.hazina lazima wakusanye kodi ili waweze kutoa PESA so kama hakuna makusanyo ni tatizo.
 
20 Dec 2020
Lushoto, Tanga

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA) CHALIA "UKATA" MKALI​



Bajeti yapigwa panga toka Shillingi bilioni 1.6 hadi fedha kiduchu shilingi million 300 tu yaani chuo kimepunguziwa bilioni 1.3 katika bajeti yake. Fedha hizo nyingi pamoja na kukatwaa lakini hicho kiasi kidogo pia huchelewa sana kufika pamoja ya kuwa shughuli na majukumu yameongezeka.

Chuo cha uongozi wa mahakama (IJA) kilichopo wilayani Lushoto mkoani Tanga kinakabiliwa na ufinyu wa bajeti ambayo inapelekwa chuoni hapo kwa ajili ya uendeshwaji wake jambo lililotajea kuchelewesha utekelezwaji wa shughuli mbalimbali. Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo hicho Dkt. Paul Kihwelo wakati wa mahafali ya 20 ya chuo hicho.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo hapo chuoni, mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahimu Juma amekitaka chuo kutumia zaidi TEHAMA ili kukabiliana na kufanya kazi vyema ktk zama hizi mpya.
 
Pesa anatoa Ndugu Jiwe,
Hazina hawana meno,ni Kama picha.
 
Ni lazima watendaji na wakandarasi wawe ni mikakati ya namna ya kufinance miradi ya kimkakati kwa kupitia PPP,municipal bonds,Loans,etc kwa kuzingatia Ushindani wa kibiashara.hazina lazima wakusanye kodi ili waweze kutoa PESA so kama hakuna makusanyo ni tatizo.
Mtawalaumu tu hazina, kila leo meko anakuja na miradi yake toka kichwani ambayo haikuwekwa kwenye bajeti, na anataka ianze hapo hapo, unadhania jiyo pesa ya kutekeleza miradi hiyo inatoka kwenye bajeti gani??kama sio kutolewa kwenye mafungu ambayo yalikuwa ya metengewa fedha hizo?kuendesha nchi bila kuheshimu utaratibu wa bajeti ni mgumu sana kwa watendaji, vyanzo vya kodi vimepungua ndio maana umeanza ubambikiaji tu,
 
Jamaa yule anaweza kuamuru kuchapisha manoti bugulu yakazagaa mtaani bila ya kuwa na thamani yeyote. Naanza kuiona Zimbabwe ya Mugabe ndani ya Tanzania siku si nyingi.
 
Back
Top Bottom