Ushauri: Rais avunje wizara za TAMISEMI na Utumishi ili kupunguza matumizi

Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
417
625
Wadau Salam kwenu

Moja kwa moja kwenye mada

Katika uchunguzi wangu nimebaini kuwa kuna wizara kadhaa ambazo lait kama leo hii Mh. Rais Samia angeniomba kumshauri kuzifuta kwa lengo la kupunguza ukubwa wa serikali ili kubana matumizi ya serikali yasiyokuwa na ulazima basi ningemshauri kuzifuta haraka wizara ya TAMISEMI na ile ya Utumishi wa umma.

Si kwamba wizara hizi hazina umuhimu au mawaziri wake wamechemka hapana, bali hizi wizara zote mbili majukumu yake yanaweza kabisa kubebwa na wizara nyingine na serikali ikaokoa gharama nyingi inazotumia kuendesha wizara hizo kama nitakavyojadili hapa chini.

Wizara ya TAMISEMI

Kwa ufupi hii ndio wizara inayosimamia mikoa na halmashauri zake zote.

Katika mikoa na halmashauri hizi kuna idara na vitengo mbalimbali vya kisekta kama vili Idara ya elimu, Idara ya kilimo, Idara ya Afya, Idara ya TEHAMA, Idara fedha, Idara ya Utumishi, Idara ya maedeleo ya Jamii, Idara ya mifugo, Idara ya ardhi na nyinginezo.

Kwa msingi huo wizara ya TAMISEMI ndio inayosimamia ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mikoa na halmashauri hizi ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, Kilimo, mifugo, ardhi n.k.

Hata hivyo miradi hii yote ingeweza kabisa kusimamiwa na wizara za kisekta.

Mfano miradi yote ya Afya au Elimu inaweza kabisa kusimiwa na wizara zenye dhamana tukaokoa kabisa gharama za kuhudumia wizara mbili kufanya shughuli inayoweza kutekelezwa na wizara moja.

Zaidi ya yote uwepo wa wizara ya TAMISEMI umekuwa ukitumika na watendaji wa wizara nyingine kama kichaka cha kukwepa uwajibikaji au kurefusha mchakato wa jambo kusiko na ulazima wowote.

Mfano kuna jamaa yangu alikuwa mtumishi katika moja ya halmashauri huko mkoani japo mwaka huu kahamia badarini, Sasa huyu jamaa alikuwa amekaa zaidi ya miaka 6 hajapanda daraja la mshahara hivyo kaamua kwenda Utumishi kuskilizia issue yake.

Alipofika Utumishi akaambiwa subiri tutawaandikia TAMISEMI wakitujibu ndipo tutashughulikia suala lako. Jamaa akarudi kituoni akapiga mzigo miezi 3 akarudi tena Utumishi, kufika huko akaambiwa bado TAMISEMI hawajatujibu na kwamba mhusika yuko likizo.

Jamaa akaondoka , akarudi tena utumishi, safari hii akaambiwa mtu aliyekabidhiwa kushughulikia suala lako yuko safari hivyo tutakujuza akirudi! Mpaka hapo ishapita miezi 9 !

Ukiisoma hii scenario utagundua dosari kadhaa za uwepo wa TAMISEMI;

KWANZA: Kile kitendo cha wizara ya utumishi ambayo ndiyo wizara yenye dhamana na watumishi kusema mpaka wawandikie TAMISEMI, wakiwajibu ndipo na wao washughulikie suala la mtumishi husika, Hii maana yake ni kwamba TAMISEMI na Utumishi kote kuna watendaji wanaoshughulika na masuala ya watumishi badala ya kuacha majukumu haya yashughulikiwe yote na kumalizwa palepale Utumishi, Kwa msingi huu maana yake serikali inalipa wizara mbili kutekeleza shughuli ambayo ingefanywa na wizara moja.

PILI: Uwepo wa TAMISEMI unachangia kurefusha michakato ya mambo, wizara nyingine za kisekta kuna mambo haziwezi kuanza mpaka wawandikie na kusubiri majibu kutoka TAMISEMI, kitendo hiki kinajenga mazingira ya rushwa na urasimu hata katika utekelezaji wa miradi muhimu.

TATU: Uwepo wa TAMISEMI umetoa mwanya kwa baadhi ya watendaji wavivu wa wizara mbalimbali kukwepa uwajibkaji kwa kujaribu kujenga gape lisilokuwepo!

Mfano mtendaji wa utumishi anaposema….” mpaka tuwaandikie TAMISEMI wakitujibu ndipo tushghulikie suala lako…..” Sote tunajua Wizara hizi zote mbili zipo Dodoma, lakini utofauti wake umefanya watu wa wizara hizo kujenga mazingira kanakwamba wizara moja ipo Tanzania na nyingine ipo Marekani.

Pia hivi sasa Serikali ilishaboresha mawasiliano yake ya kiofisi kwa njia ya mitandao lakini watendaji wa wizara hizo wanawazungusha watumishi kamakwamba barua wanazoandikiana na TAMISEMI ni za kupeleka kwa mkono tena mesenja akitumia usafiri wa miguu! Haingii akilini, miezi 6 bado barua ya mtu mmoja iwe haijafika TAMISEMI huku wote mko Dodoma!

2. Wizara ya utumishi

Hii ndio wizara ya kisekta inayosimamia masuala yanahusu watumishi wa umma.

Hata hivyo watumishi wote katika ujumla wao wamegawanyika katika sekta mbalimbali na kila sekta ina wizara yake yenye dhamana.

Hivyo inawezekana kabisa kila watumishi wasimamiwe chini ya wizara wanayoitumikia.

Mfano watumishi wote wa mikoa na halmashauri walioko idara ya Elimu, wsimamiwe na wizara ya Elimu, kadharika watumishi wa Afya wasimamiwe na wizara ya Afya n.k.

Kila wizara iwe na kitengo au idara ya rasilimali watu. Chombo hiki ndicho kiwe na mamlaka ya kusimamia masuala yote ya watumishi katika wizara husika.

Ofisi ya waziri mkuu au katibu mkuu kiongozi iwe na jukumu la kutoa miongozo kwenye wizara hizi zote ili kuhakikisha kunakuwapo na uwiano sahihi wa ubora na huduma kwa watumishi wote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madaraja na viwango vya mishara vinakwenda kwa pamoja!

Mapendekezo ya hatua za kuchukua kukamilisha mchakato huu;-
  • Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri wasimamiwe na ofisi ya waziri mkuu chini ya kamati ya kitaifa ambayo waziri mkuu ndiye mwenyekiti wake
  • Watumishi wa wizara za TAMISEMI na utumishi wahamishiwe kwenye wizara mbalimbali za kisekta kulingana na majukumu yao.
  • Wakuu wa mikoa wazisimamie moja kwa moja halmashauri za mikoa yao

  • Faida za mchakato huu
  • Kutasaidia kupunguza ukubwa wa serikali na hivyo kuokoa fedha za serikali inazotumia kuhudumia mawaziri, makatibu wakuu, Wakurugezi na watendaji wengine waandamizi wa wizara hizi.
  • Kutapunguza urasimu na kufupisha michakato katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika kila sekta.
  • Kutatoa mamlaka kamili kwa kila wizara katika usimamizi wa miradi yake na hivyo kutasaidia pia kuwajengea uzoefu watendaji wa kila wizara katika kusimamia miradi ya tofauti na sasa ambapo wamekuwa ni wapokeaji wa miradi iliyoj ngwa na TAMISEMI.
  • Kutasaidia kuboresha na kuharakisha huduma kwa watumishi kwani kero zao zote zitashughulikiwa na wizara husika.
  • Itaimarisha usimamizi wa fedha za miradi, ambapo kila wizara sasa itahusika moja kwa moja na usimamizi wa fedha za miradi ya sekta yake.
  • Itaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi kwani miradi yote ya kisekta sasa itaweza kutekelezwa kwa pamoja.
 
Wazo zuri Sana,,kimsingi wakati wa serikali ya awamu ya nne zilianzishwa idara na Tasisi nyingivSana ambazo ukiangalia uhalisia hakukuwa na ulazima Kwa mfano Hata TBS ivunnjwe kiwe kitengo ndani ya TMDA
 
Mfano Mwalimu ana mabosi wengi,Yani wizara ya Elimu,Utumishi ,Tamisemi duuuu MTU akiwa na tatizo anazunguka na makaratasi mpaka basi Ila kuna ulazima WA kufanya mabadiriko
 
Unayo hoja, nafikiri wahusika wataipitia kwa umakini......hii pia itapunguza mikanganyiko na muingiliano wa kiutendaji na kuondoa urasimu na milolongo mirefu isiyo na maana. Kwa kimombo unaweza sema 'you streamline the government' kuondoa loopholes na redunduncy....
 
Mfano Mwalimu ana mabosi wengi,Yani wizara ya Elimu,Utumishi ,Tamisemi duuuu MTU akiwa na tatizo anazunguka na makaratasi mpaka basi Ila kuna ulazima WA kufanya mabadiriko
Yap ! Hiyo ni moja ya changamoto ambazo kama serikali itafanyia kazi wazo langu automatically itakuwa imepiga ndege wawili kwa jiwe moja! Hapo mwalimu atabaki chini ya wizara ya Elimu tu! Mambo yake yote yatamalizwa na wizara ya elimu tu! no TAMISEMI wala Utumishi!
 
Naunga mkono Hoja. Ila kwa Selikali hii ya CCM hawawezi kufanya hivyo. Sababu Kila kukicha wanawaza namna ya kuongeza wizara ili watu wapige pesa..Kwa Kifupi Hata Nafasi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya Hazina maana.. Kazi zao zinaweza kabisa kufanywa na RAS NA DAS.. Mishahara ya wakuu wa mikoa na wilaya, madereva wao,gharama za kuhudumia Maghari, Afya zao n.k Ni pesa nyingi mno ambayo ingeleta Maendeleo kwa wanachi..Kwa Kifupi pesa nyingi za Selikali zinatumika kulipa Mishahara na Posho kwa watu wachache kuliko kuleta maendeleo kwa watu wengi.
 
True ,Ni uhuni Frani hivi labda raisi angeunda idara Maluum ambayo itakuwa inapokea maoni kama haya na kuyachakata Kwa haraka ,maana washauri wake haya hawaoni wanawaza kumlinda tuu, hili wazo la kuvunja Utumishi na Tamisemi ni zuri lakini litaishia hewani
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom