Daniel Chongolo akemea watendaji wa Serikali wanaochelewesha kuidhinisha fedha za miradi ya maendeleo nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,781
898
DANIEL CHONGOLO, KATIBU MKUU WA CCM

CHONGOLO AKEMEA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOCHELEWESHA KUIDHINISHA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Godfrey Chongolo, akiambatana na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kukagua miradi na shughuli za maendeleo mkoani Dar Es Salaam, amekemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali wanaohusika na kuidhinisha fedha za miradi ya ujenzi kutofanya hivyo kwa wakati licha ya Serikali kutenga na kuwepo kwa fedha za miradi hiyo.

Katibu Mkuu ameyasema hayo akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa soko la kisasa la Tandale Manispaa ya Kinondoni ambapo ujenzi huo unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 8.7 ulianza tangu mwezi Septemba, 2019 ukiendelea nje ya muda uliotarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2020, jambo linalosabisha kero kwa wananchi kutokana na adha ya kukosa mahali pa kufanyia biashara kama ilivyokuwa hapo awali.

Kaimu mhandisi wa Manispaa ya Kinondani Mkerewe Tungaraza akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, ameeleza kuwa, Kuchelewa kwa mradi huo, kumetokana na kuchelewa kwa hati za malipo na kusababisha hasara kwa serikali kwa kumlipa mkandarasi Shilingi Bilioni 2.5 nje ya makubaliano ya mkataba kutokana na nyongeza ya muda wa mkataba huo.

Ziara hii ni muendelezo wa Utekelezaji wa Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi Aprili Mwaka huu katika Mkutano Mkuu Maalum kwa Chama kutembelea na Kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
13 Agosti, 2021

PmC86C4G_400x400.jpg

IMG-20210802-WA0023.jpg
 
..serikali haina fedha.

..pia bajeti ya miradi na maendeleo ni ndogo sana.

..serikali imepanga kutumia 80% matumizi ya kawaida, na 20% kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
 
DANIEL CHONGOLO, KATIBU MKUU WA CCM

CHONGOLO AKEMEA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOCHELEWESHA KUIDHINISHA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Godfrey Chongolo, akiambatana na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kukagua miradi na shughuli za maendeleo mkoani Dar Es Salaam, amekemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali wanaohusika na kuidhinisha fedha za miradi ya ujenzi kutofanya hivyo kwa wakati licha ya Serikali kutenga na kuwepo kwa fedha za miradi hiyo.

Katibu Mkuu ameyasema hayo akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa soko la kisasa la Tandale Manispaa ya Kinondoni ambapo ujenzi huo unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 8.7 ulianza tangu mwezi Septemba, 2019 ukiendelea nje ya muda uliotarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2020, jambo linalosabisha kero kwa wananchi kutokana na adha ya kukosa mahali pa kufanyia biashara kama ilivyokuwa hapo awali.

Kaimu mhandisi wa Manispaa ya Kinondani Mkerewe Tungaraza akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, ameeleza kuwa, Kuchelewa kwa mradi huo, kumetokana na kuchelewa kwa hati za malipo na kusababisha hasara kwa serikali kwa kumlipa mkandarasi Shilingi Bilioni 2.5 nje ya makubaliano ya mkataba kutokana na nyongeza ya muda wa mkataba huo.

Ziara hii ni muendelezo wa Utekelezaji wa Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi Aprili Mwaka huu katika Mkutano Mkuu Maalum kwa Chama kutembelea na Kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
13 Agosti, 2021

View attachment 1891377

View attachment 1891379
Kwanini hakemei kususua ukamilishaji ujenzi wa Ikulu mpya ya jijini Dodoma, usitishwaji wa ujenzi wa barabara pete huko jijini Dodoma, kutokamilika kwa reli ya mwendo kasi (SGR) ambayo haijulikani ni lini itakamilika na kuanza kufanya kazi, kusuasua kwa upanuzi wa barabara ya kwenda, Lindi-Mtwara, kulegalega ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato Dodoma, kutoanza kwa ujenzi wa uwanja wa michezo wa kimataifa hapo Nanenane Dodoma, juhudi kabambe za kuvutia utalii nyanda za juu kusini makao yake makuu yakiwa pale Iringa, kutangaza kwamba miji ya Lindi, Kilwa, Mafia na Mikindani, Songea ndio miji mikongwe na yenye vivutio mjarabu kiutalii kwenye pwani ya kusini? Ununuzi wa ndege ya mizigo, kuruhusu boti ya mwendo kasi kufanya usafirishaji kati ya Bagamoyo-Dar Es Salaam-Mafia-Lindi na Mtwara
 
Hukuona kama juzi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa kuikagua Ikulu imefikia wapi? Uwe unaongea kwa data.
 
Hakuna hela acheni utapeli. Kukagua ni sehemu ya show off lakini heka hakuna fullstop.

..Makamu wa kwanza wa Rais wa Znz kasema serikali yao ina hali mbaya kifedha.

..Sijui huku Tanganyika hali ya kifedha ikoje.

..Sitashangaa nikisikia kwamba tumekaukiwa.
 
Tulishakaukiwa vibaya toka enzi za dhalimu, ndio maana zikaletwa hizi tozo za kulazimisha.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom