Hayati John Pombe Magufuli alitutoa kwenye giza totoro lililoleta kashfa kubwa ya Ufisadi wa Richmond na Escrow

Nimesoma tu mistari miwili ya kwanza nikajiridhisha ya kwamba nikiendelea kusoma zaidi nitapigwa ban
 
Mkuu ukweli utabaki ukweli usihofu JPM ni mzalendo halisi wa karne ya leo!

Hamna mzalendo mwizi, ngoja ufanyike ukaguzi hapo ndio uzalendo wa kweli utafahamika. Kama alikuwa anateka na kuua wote wanaohoji wizi wake, basi saa hii yuko kuzimu acha watu wajiridhishe na uzalendo wake kwa kukagua mahesabu.
 
Je Nape anamchimba Makamu wa Rais aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wakati ule? Na pia Rais aliyekuwa Makamu wa Rais. Atambue yeye amekuwa kwenye serikali hiyo kipindi fulani mbona hakuyasema kwenye Baraza la Mawaziri?
Ulitaka aseme vipi wakati mlimtolea bastola hadharani? Sasa hivi mkae kwa kutulia taarifa za lile jizi la kura zikae peupe.
 
Chifu Hangaya mara tu alipokamata usukani alisema "kazi kubwa aliyonayo ni kuifungua nchi kimataifa"Nani alifungia???
Kwanini hukumuuliza kuwa mlikuwa wote Ikulu kwanini hamkushauriana kwanza kabla ya kuifungua nchi??

Tutajuaje kama Nape alifuatwa na wale wasiojulikana na kumpa siku tatu aende kumuomba msamaha Jiwe vinginevyo wangempoteza???
Mtazamo wako uko sawa wala sina tatzo juu ya hilo ila kama uraisi ni taasisi basi lawana ziwe zinaenda kwa watu wote kuanzia rais, makamu wake, waziri mkuu na bunge letu hatuwez kutoa lawama wakati wanaotoa lawana na wao walikuwepo kweny system ya serikali kusemea kitu ambacho ulikuwa na uwezo wa kusema kwa wakati huo huo ila sasa ivi ndo unasema ni kupoteza tu muda
 
KAMA JPM ALIKULA MKOPO NA KUWAFUMBUA MACHO WATANZANIA,BASI TUWAACHE WATANZANIA WAAMUE.

Fuatana nami👇👇👇

Rais John Pombe Magufuli alitutoa kwenye giza totoro lililoleta kashfa kubwa ya Ufisadi wa Richmond na Escrow na kutupeleka kwenye nuru na mwanga kwa kutujengea Bwawa kubwa la Umeme la Rufiji litakalo zalisha Megawati 2,200,

Sasa taifa letu linatumia Megawati 1,100 tu kwa hiyo Bwawa la Umeme la Julius Nyerere linalojengwa Rufiji litazalisha megawati 2,200 yaani mara mbili ya Umeme tunaotumia sasa,hii ni faida kubwa kwa Taifa na shukrani za dhati ziende kwa Rais wetu,Ndugu John Pombe Magufuli.

Baada ya Kujenga Bwawa la Umeme,Rais John Pombe Magufuli anatupeleka kwenye ujenzi wa Viwanda vitakavyotumia Umeme huo kuviendesha,

Viwanda vitatengeneza Taifa linalojitegemea ambalo nguzo kuu ya uchumi wake ni sekta ya viwanda.

Tunataka tufike mahali ambapo Taifa letu litakuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi na kutekeleza mipango yake ya maendeleo bila kutegemea misaada.

Ndugu zangu sekta ya nishati ni uti wa mgongo wa Uchumi wa Taifa lolote lile duniani,(Power/Enegy sector is a backbone of the Economy of any country) Every country now is fighting on how to control energy sources.

Sekta ya nishati ndiyo kila kitu katika Uchumi wa Taifa lolote lile duniani,huwezi kucheza na Sekta ya nishati (power/Energy sector) nchi zote duniani hazifanyi mchezo na sekta hii, ndiyo maana Rais John Pombe Magufuli amewekeza katika Sekta hii ya nishati ili kulijenga Taifa la Viwanda la Uchumi wa kati,

-Kwa ufupi tuangalie mambo machache ambayo Rais John Pombe Magufuli ametutoa kutoka hatua moja na kutupeleka hatua mbili mbele zenye mafanikio,

1. JPM alitutoa kwenye usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani anatupeleka kwenye usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme na muda mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi.

2. JPM alitutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege mpya sita.

3. JPM alitutoa kwenye shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu.

4. JPM alitutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 mwaka 2015 mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2

5. JPM alitutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye unafuu wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

6. JPM aliwatoa akina Mama Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja, kitanda kimoja.

7. JPM alitutoa kwenye mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 89, tena kwa bei nafuu.

8. JPM alitutoa kwenye usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga na Mama Ntilie.

9. JPM alitutoa kwenye mfumo wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala rushwa na Mafisadi. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

10. JPM alitutoa kwenye mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara. Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.

11. JPM alitutoa kwenye uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo.

12. JPM alitutoa Wanazuoni wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini kabisa.

13. JPM alitutoa kwenye balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi wa umma na ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.

14. JPM alitutoa kwenye utitiri wa kodi kwenye kilimo na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh. 4000 kwa kilo.

15. JPM alitutoa kwenye usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini.

16. JPM alitutoa kwenye tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki, miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers na reli ya kisasa ya standard gauge.

17. JPM alitutoa kwenye makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.5 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali kibajeti.

18. JPM alitutoa kwenye urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali. Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site palipo shida za Wananchi wakizitatua.

19. JPM alitutoa kwenye mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala ya ardhi na sheria.

20. JPM alitutoa kwenye mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la Serikali kuhamia Dodoma. Mpaka sasa Waziri Mkuu, Wizara na idara mbalimbali zimehamia Dodoma. Tukumbuke mpango wa Serikali kuhamia Dodoma ulikuwepo na kushindikana kufanyika toka enzi za utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza.

Hayo ni baadhi tu, sisi Wananchi wa Tabaka la chini tunaelewa Rais Magufuli alipotutoa na anapotupeleka.

-Tuangalie takwimu za Utendaji wake uliotukuka hapa chini,

21. Ujenzi wa Stiegler's gorge HP Bwawa kubwa la Umeme litalozalisha Megawati 2,300

Mradi huo ambao unafahamika pia kwa jina la Julius Nyerere, unatazamiwa kuzalisha megawati zaidi ya 2,000 za umeme, hatua ambayo inaelezwa kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii.

22. SGR Treni ya Umeme toka Dar mpaka Moro hadi Dodoma mradi ambao unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa Mwaka huu.

23. Uundwaji wa meli kubwa katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa.

24. Ununuzi wa Ndege kubwa 11 Boeing,Airbus na Bomberdier na upanuzi wa viwanja vya ndege na vya kisasa kabisa.

25. Ujenzi wa miundo mbinu ya kisasa( fly overs ya Mfugale ,Interchange ya Ubunge na Madaraja Makuba mawili yatakayokatiza kwenye maji ya Busisi across lake Victoria na Tanzanite bridge katika Bahari ya Hindi, Ujenzi wa barabara nane ubungo - chalinze ambao ni ujenzi na upanuzi wa barabara wa kisasa kabisa unaoruhusu magari kupishana hata matatu hivyo kupunguza ajali.)

26. Usambazaji wa umeme kuanzia kwenye tarafa, kata hadi vijiji al maarufu kama Umeme wa Rea.

27. Vituo vya afya bwerere zaidi ya 390 Tena vya kisasa na huduma ya oparesheni ili kupunguza vifo vya uzazi ambavyo uzazi uligeuka laana na Sasa Uzazi utakwenda kuwa baraka,

28. Miradi ya maji na usambazaji wa maji maeneo mengi ukiwamo mradi wa maji ya Ziwa Victoria toka Mwanza kuja Singida hadi Dodoma.

29. Uboreshaji wa vyuo na sekondari zilizichoka tangu enzi za Mwalimu Nyerere,Shule zote zimejengwa upya na kurekebishwa vizuri na sasa zina muonekano mzuri kabisa na mazingira bora ya kusoma,

30. Wanafunzi kukaa chini imebaki historia,

31. Ufufuaji na usimamizi wa mazao na kumnufaisha mkulima( pamba, mkonge, chikichiki, korosho, ufuta.) Pamoja na uondoaji wa tozo.

32. Usimamizi wa mapato ya serikali uliowezesha serikali kuwa na akaunti moja badala ya 2000.

33. Usimamizi mzuri wa vita ya corona. Hapa kila mtanzania alijua tumeisha. JPM alitia ujasiri wa hali ya juu sana na virusi vya kupandikizwa Maabara vikashindwa.

34. Upigaji na upigwaji kwenye ardhi umepungua kwa asilimia 90.
Mengi sana najiandaa kuandika vitabu,

35.Elimu Bure kwa kila Mwanafunzi,

36.Mbuga za Wanyama, mpaka sasa chini ya Rais John Pombe Magufuli Tanzania tunaongoza tuna Hifadhi za Taifa 22 zina Wanyama wote, hata mti mrefu kuliko yote Afrika upo Tanzania, Mlima mrefu kuliko yote Afrika upo Tanzania Mlima Kilimanjaro, Mungu ametupendelea, Tanzania Hoyee

37.Upanuzi wa vituo vya Afya zaidi ya 390 umefanyika na ujenzi wa vituo 7,200 vya kutolea huduma za Afya katika vijiji,

38.Shirika la NDC limeweza kuuza matrekta 684 yenye thamani ya 30 Bilioni sawa na 83.2% ya matrekta 822 yaliyo wasili nchini.

39.Ufufuaji wa mashamba ya kwa sasa uzalishaji umeongezeka na kufikia tani 86.7 kwa kipindi cha miaka miwili ambapo hapo awali hakuna kumbukumbu zozote kutokana na muwekezaji wa awali aliyekua akisimamia shamba,

Uzalishaji umeongezeka hadi kufikia tani 86.7 zenye thamani ya shilingi 210 milioni na kuajiri Watanzania 278,katika Awamu hii ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.

Kupitia mradi huu tumetengeneza ajira zaidi ya 2000 za moja kwa moja,

Kwa kipindi cha takriban miaka miwili, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Shilingi 2.6 Bilioni hadi Shilingi 6.9 Bilioni sawa na 164.3% kutoka mwaka 2017 hadi 2019.

40.Ununuzi wa Rada 4 na kujengwa katika Viwanja vinne,hili limetusaidia kuacha kutegemea rada za Kenya,jambo ambalo lilikuwa hatari kwa usalama wa nchi.

@Nape pokea Salaam.
Haya Wai chato katambikwe kwenye kaburi lake mungu wenu
 
Back
Top Bottom