Haya yalisemwa 1958 leo yametimia...

Haya yalisemwa 1958 leo yametimia...

Pia hela yetu ilikuwa na thamani ndogo sana ukilinganisha na dola, au pound, kuliko sasa hivi.
Pia aligawa rasilimali za taifa bure kwa wageni, kwa staili ya kina chief mangungo wa msovela, kuuza watu kwa kipande cha nguo, na kubadilishana debe la almasi kwa kwa debe la unga wa muhogo.

Mkuu hii unazungumzia enzi ipi? Ya Nyerere au umemix na topic zako za historia ya biashara ilivyoanza siku za kale?

Sent from Samsung tablet
 
Mkuu hii unazungumzia enzi ipi? Ya Nyerere au umemix na topic zako za historia ya biashara ilivyoanza siku za kale?

Sent from Samsung tablet

Ni mwendelezo tu wa alichokiandika niliyem-quote.
 
nadhani umemuelimisha huyo kijana...inaoneka hakuwepo kabisa wakati awamu ya kwanza , atakuwa kazaliwa awamu ya 2....wakumbuke waka wa mwl. ndio tulijenga viwanda vingi sana, Tanzania ilikuwa na viwanda zaidi ya 400....waliofuata wakavuia na kuviuza.....wawekezaji wanatakiwa kuja kujenga viwanda vipya sio kununua vyazamani na kuvifanga maghara

Sina uhakika sana kama unaifahamu nchi hii vizuri, labda kidogo nikukumbushe kwamba katika awamu nne za urais yafuatayo tuliyaona:
  1. Kipindi cha kujenga nchi baada ya ukoloni, kiliambatana na wananchi kufunga mikanda, nadhani unaelewa ilimaanisha nini.
  2. kipindi cha ruksa, kilichoambatana na watu kuacha kazi serikalini na kuanzisha shughuli/biashara binafsi, labda unaelewa ilimaanisha nini?
  3. Utandawazi na Ubinafsishaji kwa kasi kubwa, walioacha kazi serikalini walitamani kurudi, jenga hoja kichwani mwako unadhani ni kwa nini?
  4. Oh My God! Serikali haina fedha, wananchi walio wengi hawana fedha, ufisadi umeota mizizi, tumebaki kulalamika tu kutokana na uduni wa elimu yetu.
tafakari kwa makini utanielewa ni nini ninachomaanisha, wenzako tuliendesha maisha kwa kuuza sigara kwenye vipakti wakati serikali inashindwa kuwalipa wafanyakazi wake.
 
Mphhh!ni kweli tumepigika kinoma na wenyewe wanasema na mbado.
 
nadhani umemuelimisha huyo kijana...inaoneka hakuwepo kabisa wakati awamu ya kwanza , atakuwa kazaliwa awamu ya 2....wakumbuke waka wa mwl. ndio tulijenga viwanda vingi sana, Tanzania ilikuwa na viwanda zaidi ya 400....waliofuata wakavuia na kuviuza.....wawekezaji wanatakiwa kuja kujenga viwanda vipya sio kununua vyazamani na kuvifanga maghara
Asante sana Mdau, tatizo hawa madogo wanaishi kwa kutegemea takrima hivyo watasema lolote hata kama wanajuwa ni uongo ilimradi tu wamewafurahisha waajiri wao (Mafisadi, wabakaji wa maendeleo na demokrasia). amini usiamini 2013 hadi 2015 watatokea wengi sana watakaotaka kutuaminisha kuwa Shetani ana nguvu kuliko Mungu kwa vile tu wamepewa rushwa na shetani
 
Wako wapo wenye maoni kama haya, wajanja wachache waliaza na kuhodhi mali kama ardhi kama alivyotabiri mwalimu, baada ya kumaliza kuhodhi mali sasa wanahodhi madaraka ili kujilinda. Kwa hiyo kilichopo sasa ni kwamba wao wanamali na mamlaka. Kazi ipo
Njoka Ereguu
Unachosema ni sahihi.. Ni ukweli usiopingika baada ya JK Nyerere kufariki inasikitisha sana hakuna kiongozi hata mmoja mwenye nguvu ndani ya CCM anyeweza kuvaa viatu vya Baba wa taifa, JK Nyerere. Tumebaki na aina ya viongozi wanaolia na kulalamika kama wananchi wa kawaida huku wakisema "sisi bwana wakati wa Nyerere husingeona ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yanafanyika na raisi anakaa kimya". Ona nchi inavyoliwa mchana kweupe, ona wanyama wa pori wanaporwa na kupandishwa kupitia viwanja vya ndege kweupe na viongozi wa serikali, polisi, JWTZ, usalama wa taifa wapo wanaponda raha mustarehe. Wako wapi akina Bujiku, wapo wapi akina Dr. Salim Ahmed Salimu, wako wapi akina Kaduma, wako wapi akina Dr. Kitine ambao kila kukicha huku wanaimba na kutukuza fikra sahihi za Marehemu JK Nyerere bila kuchukua hatua zozote za kizalendo ili kuongoza watanzania masikini kupambana na viongozi wa serikali na CCM wanapora rasilimali na utajiri wa nchi yao. Sana sana tunachokiona ni ule msemo wa "If you cannot defeat them join them"! Tunajua sasa CCM inatumia kila njia kama vyombo kama polisi, usalama wa taifa na vyombo vya habari kuhakikisha sauti ya wanyonge na taasisi zinazojaribu kuwatetea hazifanikiwi! Pamoja na hayo watanzania wazalendo na wapenda mabadiliko hawakatishwi tamaa bali wanaendelea kuwaelimisha watanzania mijini na vijijini ili mwisho wa siku waweze kukiiondoa CCM madaraka. Kwahiyo basi watz ni lazima watambue kuwa mapambano na harakati za kuiondoa CCM hayahitaji Prof. Lipumba, Dr. Slaa, Zitto, Mbowe, Lyatonga, Mch. Mtikira, Julius Mtatiro pekee yao bali yanahitaji umoja wa watanzania wote wazalendo na wapenda nchi , masikini, wasomi, wakulima, wafugaji, wavuvi, wanafuzi mashuleni na vyuo vya elimu ya kati na juu na wanaume na wanawake. Hima shirikianeni kuakikisha CCM hairudi tena madarakani 2015!
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa utawala wa huyu mzee kulikuwa na shida sana mpaka sabuni ya kuongea/kufulia, kulikuwa hakuna.
Sote tulipanga foleni pamoja, tulisoma shule zenye hadhi sawa bure,wote tulipata matibabu humu humu nchini na dawa zilikuwa bure hata tembo na twiga walizaliana sana bila ya wasiwasi!
 
Wakati wa utawala wa huyu mzee kulikuwa na shida sana mpaka sabuni ya kuongea/kufulia, kulikuwa hakuna.
Ingawa hali ilikuwa hivyo lakini Nchi ilikuwa inaheshimika kutokana na kuwa na Kiongozi shupavu, Leo vipi tuna kiongozi shupavu kweli? pia wakati huo uchumi wetu haukuwa tofauti sana na nchi za Korea sasa tujiulize mbona wenzetu wametuzidi tatizo nini? hapo ndo tunapotakiwa kuja na jibu la kubadilisha utawala kwani CCM imeshindwa kutukomboa kutoka katika wimbi la umasikini.
 
Mkuu Nokla, si kweli kuwa Mwalimu aliacha hazina haina kitu. Tuambie Mzee Ruksa alifanya jitihada gani kujaza hiyo empty hazina. Nina hakika unaongea vise versa.
 
itafika wakati tutaufukua mwili wake tuweke picha yake itawale kwa kufuata mawazo yake tutaendelea kuliko kuwa na watawala,waheshimiwa mpaka wanajionea aibu na kuchakachua uheshimiwa na kjiita ndugu!
 
Huyu mzee ukisimkiliza maneno yake utamuona mtu wa maana sana ...
Huku akipangisha watu foleni za sukari na unga wa njano....

Hongera Mzee Ruksa kwa kuwakomboa wa-Tanzania
 
Hata aliowakataa 1995--magogoni wataiona kwenye tv-tu.-time will tell.
 
n.jpg

Wakati wa utawala wa huyu mzee kulikuwa na shida sana mpaka sabuni ya kuongea/kufulia, kulikuwa hakuna.

Upo hapo?
 
Back
Top Bottom