Nguli,
Kwetu mzee bila kuwa mgumu huwezi kwenda kusalimia - ni km kama 1000 hadi napoiacha barabara kubwa ya lami, then nakwenda km zingine 450 hadi kijijini kwetu, hii barabara ni mbovu saana - vumbi, mashimo na matope wakati wa masika usipime - average ni km 15 hadi 20 kwa saa ukiwa dereva mzuri.
Nipo jirani sana na waziri wangu mkuu, toka kijijini kwetu hadi kwao ni kama km 90 kwa upande wa pili - ambapo unaweza kupiga kwa baskeli tu na ukafika.
Kwetu bwana hali ni MBAYA SANA, vijana wamekata tamaa wanakunywa pombe za kienyeji - "ngogo" ambapo chupa ya orange inauzwa sh 500 na ndogo ya soda sh 250.
Class mates wangu washakuwa wazee, si kwa umri ila shida walizonazo - wasichana wa wakati ule tuliosoma shule pamoja sasa ni wabibii - hawa ndiyo wanaochuja gongo kuwauzia wenzao, ili zoezi nzima la kugawana umaskini likamilike.
Kijijini kwetu umaskini ni wa wote, hakuna nyumba nzuri watoto ambao tulibahatika kupata elimu hii ya kambarage ya bure kawaida hatutaki kurudi kuwekeza sehemu isiyo na barabara wala chochote cha kutega uchumi, kwa hiyo tumengagania mjini kujaribu kujikimu ki mtindo mtindo.
Ila kwetu bia na soda hukosi, zinauzwa ingawa bei ni mara mbili ya ile ya mkoani, zinawekwa kenye chungu maalum kwa wale wanaopenda za baridi, kuku wa kienyeji eg jogoo kubwa ni sh 1200, nyie huku mnauziwa hadi sh 15,000k. kwetu bwana kuku hata kila siku ukitaka.
Kwetu bwana usafiri ni alfajiri na BASI lipo moja tu linaondoka saa 10 na nusu – ukipenda usingizi wa asubuhi inakuwa imekula kwako linakuacha hadi kesho yake tena, nauli ni kubwa mno kiasi watu wanashindwa ku afford badala yake wanatumia baskeli na gari la ngombe - ni km 450 hadi mkoani – siku za mwisho wa mwezi linajaa sana maana walimu, manesi, bwanamganga, bwana mifugo wote ndani ya basi letu mjini kuchukua mshahara – kasheshe kupumuliana manake wengine wanakuwa wamelala nazo tena za kienyeji – mmhhh.
Mafisadi wa kule ( wenye nazo) ni waalimu, bwana mganga na wale wenye viosks, kweli hali ni ngumu mno - kwa mfano ukienda likizo ukamaliza pesa zako hadi nauli basi itakuwa imekula kwako maana hakuna benki kule mpaka usafiri hizo km nilizokwambia.
Kule kijijini kwetu bwana tuna shule ya sec ya kata moja ambapo kuna watoto wa ndugu yangu wanasoma pale, yupo mmoja form four nikamuuliza vitu basic tu hajui chochote hata test tube hajawahi kuiona.
Bwana kule kwetu ardhi ni bure kabisa ila haina rutuba - watu wanajaribu kulima tumbaku, mahindi, karanga, alizeti ila kwa heka moja ukipata gunia mbili ujue una bahati sana chief, hali ni mbaya sana, hakuna matumaini yoyote kwenye hiki kilimo.
Kijijini kwetu hakuna umeme, kwa hiyo nilivyokuwa huko nilikuwa naenda kwenye mnara wa celtel ili kucharge simu yangu ya nokia – bahati huduma hii ya simu imetufikia, nawapongeza sana hawa jamaa – mkiwaona wapeni big up.
Ukipata nafasi wakuu, njooni mtutembelee huku kijijini kwetu ili kama ikiwezekana tuugawane umaskini pamoja.